Mwanadada
huyo alijikuta akifunua chupi yake kwa kaka huyo anayeuza njegere
kutokana na ubize wa mume wake uliosababishwa na shughuli zake za
kibiashara ambazo humfanya mara nyingi awe nje ya nchi na kushindwa kupata muda wa kutosha kukaa mke wake.
Tangu
Mrembo huyo afunge ndoa na mumewe mwaka 2010 alieleza kuwa hajawahi
kukaa na mumewe wiki moja nzima kwani mume wake huja na kuondoka kwa
muda mfupi sana na apomwambia kuhusu kukaa muda mrefu Mume huyo hudai
kuwa biashara zake zinaweza kutetereka hivyo zinahitaji usimamizi wa
karibu kutoka kwake.
Ndipo
katika harakati za kuondoa upweke huo na kutuliza hamu yake kimapenzi
alijikuta akiingia mikononi mwa kijana mmoja muuza njegere
aliyekutananae siku moja mwanadada huyo alipokuwa anatoka na gari
yake nje ya geti la nyumba yake na aliposhindwa kuzuia hisia zake ni
pale alipoweka gari pembeni na kumwomba kijana huyo aingie ndani ya
nyumba ili ampimie njegere.
Dada
huyo alijikuta akimsimulia kaka huyo habari ya ubize wa mumewe na
kumwomba kaka huyo ampe raha kwa kumpa penzi pale atakapokuwa anahisi
kuzidiwa na hamu ya kufanya mapenzi.
Kaka huyo alijikuta ameingia majaribuni kwa kumkubalia dada huyo jambo
ambalo lilizua gumzo kwa marafiki na majirani waliposhtukia suala hilo
kutokana na kushamiri kwa penzi la wawili hao huku Mume akiwa hana hili
wala lile.