Showing posts with label Habari za Kitaifa. Show all posts
Showing posts with label Habari za Kitaifa. Show all posts

Ukawa wateka manispaa Dar es Salaam



mikoani. Vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimefanikiwa kushinda kata nyingi katika jiji la Dar es Salaam na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuongoza mabaraza ya madiwani katika halmashauri za manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke.
Mbali ya kusimamia mabaraza hayo, pia Ukawa unaweza, kwa mara ya kwanza, kuongoza halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
Tangu mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa mwaka 1992, CCM imekuwa ikishinda kata nyingi na hivyo madiwani wake kuunda halmashauri, lakini mwaka huu imepokonywa kata nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita baada ya Ukawa unaoundwa na vyama vya NLD, CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi kunyakua ushindi katika kata hizo.
Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huo yanayoendelea kutangazwa Ukawa umenyakua viti 53 vya udiwani katika majimbo ya Kinondoni, Ukonga, Ilala, Segerea, Temeke, Kibamba, Kawe, Ubungo, Mbagala na Kigamboni wakati CCM ikipata viti 38.
Moja ya Halmashauri ambazo Ukawa wataziongoza ni ya Kinondoni ambako umetwaa kata 22 kati ya 34. Katika halmashauri hiyo yenye majimbo ya Kawe, Ubungo, Kibamba na Kinondoni, Chadema imenyakua kata 17, CUF imeshinda kata 6, na CCM imetwaa kata 9 huku yakisubiriwa matokeo ya kata mbili.
Halmashauri ya Ilala yenye majimbo ya Ilala, Ukonga na Segerea, matokeo yanaonyesha kwamba Chadema ina kata 19, CCM kata 15 na CUF kata mbili. Madiwani wa kata hizo ndio watakutana kuteua meya na naibu meya wa halmashauri ya Ilala.
Halmashauri ya Temeke inayoundwa na majimbo ya Temeke, Kigamboni na Mbagala ina jumla ya kata 31. Katika jimbo la Temeke CCM ina kata 7, Chadema 5 na CUF 1; Kigamboni: CCM kata 6, Chadema 2 na CUF 1, wakati Mbagala CCM kata 7 na CUF tatu.
Aidha, upinzani umefanikiwa kutwaa majimbo sita kati ya 10. Majimbo hayo na majina ya wabunge wake kwenye mabano ni Kawe (Halima Mdee – Chadema), Kinondoni (Maulid Mtulia – CUF), Temeke (Abdallah Mtolea – CUF), Ukonga (Mwita Waitara –Chadema), Ubungo (Saed Kubenea – Chadema), Kibamba (John Mnyika- Chadema).
Waitara amepata ubunge baada ya kumbwaga aliyekuwa meya wa Ilala, Jerry Slaa (CCM); Mtolea amemshinda Abbas Mtemvu (CCM); Mdee amemwangusha Kippi Warioba (CCM), na Kubenea amemshinda aliyekuwa meya wa jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi (CCM).
Mnyika amembwaga Fenella Mkangalla (CCM), Mtulia amemshinda Idd Azzan (CCM). Bonna Kaluwa wa CCM ndiye mbunge wa Segerea, Faustine Ndungulile wa CCM amefanikiwa kutetea jimbo la Kigamboni sawa na Mussa Hassan Zungu aliyetetea jimbo la Ilala.
Matokeo ya mikoani
Jimbo la Ndanda lina kata 16; CCM (15), Chadema (1); Tandahimba: kata 30, CCM (10), CUF (16), Chadema (1); Kalenga: kata ni 15, CCM (13), Chadema (3); Iringa Mjini kata 18, Chadema (14), CCM (4); Isimani kata 14, CCM (11) Chadema (3); Ushetu kata 20, CCM (20); Serengeti kata 30, CCM (12), na Chadema (18).
Jimbo la Dodoma Mjini kata 41, CCM (34), Chadema (6); Mpwapwa lina kata 13, CCM (13); Kibakwe kata 18, CCM (18); Mbozi kata 11, CCM (7), Chadema (4); Mtwara Mjini kata 18, CUF (8), CCM (7), Chadema (3); Mwibara kata 12, CCM (7), Chadema (2), TLP (2) na CUF (1); Bunda Mjini kata 14, CCM (10) na Chadema (4); Bunda Vijijini kata 7, CCM (5) na Chadema (2).
Handeni Mjini kata 12, CCM (11), CUF (1); Handeni Vijijini kata 21, CCM (20), Chadema (1), Kilindi kata 21, CCM (20) kata moja haijafanya uchaguzi; Vunjo kata 16, NCCR (8), CCM (4), Chadema (4); Sikonge kata 17, CCM (14), Chadema (3); Kahama Mjini kata 20, CCM (19) Chadema (1).
 Momba kata 14, CCM (8), Chadema (6); Mbeya Vijijini kata 29, CCM (21), Chadema (7); Kisarawe: CCM (14), Chadema (2), CUF (1); Nanyumbu CCM (15), CUF (2), na Bagamoyo kata zote 11 zimechukuliwa na CCM.

Rais Kikwete: Uchaguzi Serikali za Mitaa kusogezwa mbele


RAIS Jakaya Kikwete amesema uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ulikuwa ufanyike mwezi Oktoba mwaka huu, huenda ukasogezwa mbele kutokana na kutokamilika kwa mchakato wa rasimu ya mabadiliko ya Katiba.
 
Kauli hiyo ameitoa kwenye mkutano wa majumuisho ya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tanga.
 
Alisema kulingana na hali ilivyo hivi sasa ambapo Bunge la Katiba halijakamilisha kazi zake, ni dhahiri kwamba uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi huo kwa kutumia Katiba mpya haupo.
 
“Kwa mfano, wabunge endapo wataamua wapitishe kwamba katiba itambue serikali 3 ni lazima kwanza itungwe katiba ya Tanganyika ambayo itaainisha taratibu zitakazotoa mwongozo wa uchaguzi…hata kama itabaki kama ilivyo …. bado muda wa kuandaa huo utaratibu wa uchaguzi wa serikali za mitaa hautatosha kwa sasa”, alisema.
 
Aidha aliongeza, “Nimeona niliseme hili japo kwa ufupi kwamba uchaguzi huu huenda utalazimika kusogezwa mbele kutokana na kutokamilika kwa mchakato wa Rasimu ya mabadiliko ya Katiba“, alisema.
 
Katika hatua nyingine, Rais amewataka Maofisa Kilimo kwenye halmashauri kujiendeleza kitaaluma na kuwa mabingwa waliojikita katika taaluma ya mazao yanayostawi kwenye maeneo yao badala ya kuyashughulikia kwa ujumla mazao yote yanayolimwa na wananchi.
 
Alisema utekelezaji wa agizo hilo utaongeza mavuno kwa zao husika, utapanua wigo wa uzalishaji pamoja na utaalamu katika kushughulikia zao, aina ya zao na kuleta tija katika sekta ya kilimo.
 
Alisema hatua ya maofisa kilimo kuendelea kujishughulisha kwa ujumla na mazao yote yanayostawi bila kuwa na lengo la kusimamia mazao maalumu, kunaifanya sekta hiyo kudumaa na hivyo kushindwa kuwakwamua kiuchumi wananchi.
 
“Nimegundua kwamba watu wetu wengi hawana utaalamu uliobobea…hata maofisa kilimo wetu hawana taaluma maalumu zilizojikita kwenye aina ya mazao mengine zaidi ya mpunga na mahindi, hatua ambayo inawasababisha washindwe kusimamia vizuri uzalishaji wa mazao mengine ambayo yangeweza kuwakwamua kiuchumi wakulima kwenye halmashauri husika,” alisema.
 
Aliongeza, “Kwa hiyo ni jukumu lenu viongozi wa halmashauri kuwachukua maofisa kilimo wenu na kuwapeleka SUA kwa ajili ya ku-specialize (kujikita) kulingana na vipaumbele vyenu vya mazao kwa sababu sio wote wanao ubingwa katika kila zao…tukifanikiwa kwenye hilo tutapata mafanikio zaidi”, alisema.
 
Aidha aliwataka viongozi kwenye mkoa wa Tanga kuhakikisha shughuli za kilimo zinajikita kwenye uzalishaji endelevu wa mazao ya matunda na mboga, kwa kuwa mkoa huo uko katika fursa nzuri kiuzalishaji zaidi ya mazao ya nafaka.

Mwanamke Aliyemng'ata Hausigeli na kumchoma Pasi Aachiwa


Mtuhumiwa wa kesi ya kujeruhi kwa kumng'ata sehemu mbalimbali za mwili  mfanyakazi wa ndani, inayomkabili Amina Maige (42) amepatiwa dhamana jana baada  ya mahakama kuthibitisha kuwa hasira kutoka kwa wananchi zimepungua.
 
Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Yohana Yongolo alisema ameridhishwa na ufafanuzi uliotolewa na Mwendesha mashitaka wa Serikali pamoja na Wakili wa mshitakiwa kuwa haki ya dhamana itolewe kwa kufuata masharti na kwamba hakuna uhalifu wowote utakaofanyika dhidi ya mshitakiwa huyo.
 
Hakimu  Yongolo alitoa masharti ya dhamana ambayo yalimtaka Maige kutoondoka nje ya Dar es salaam bila ya ruhusa ya mahakama hiyo.
 
Pia alitoa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminiwa kutoka taasisi inayotambulika hapa nchini ambapo mdhamini huyo anaweza kuwa mwajiriwa, mfanya biashara na mkulima.
 
Alisema wadhamini hao watatakiwa kusaini hati ya makubaliano kwa kila mmoja kulipa Sh milioni tatu.
 
Aliongeza kuwa kesi hiyo itasikilizwa Julai 22 mwaka huu.
 
Maige alidaiwa Januari mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alimng'ata na kumchoma na  pasi  sehemu mbalimbali za mwili wa  mfanyakazi waje wa ndani Yusta Kashinde (20) na kumsababishia maumivu mwilini.

Mbio za Urais 2015: Fredrick Sumaye Asema yeye ndo Tumaini pekee la Watanzania


WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, amesema yeye ni tumaini la Watanzania na mpambanaji wa vita dhidi ya maovu.
 
Kutokana na hali hiyo, amesema ni jemadari hodari aliyeungana na askari wapiganaji hodari wa vita ambao wataleta ushindi usio na shaka.
 
Kauli hiyo aliitoa jijini Mwanza jana, katika hotuba yake ya uzinduzi wa taasisi ya Vijana ya Tanzania Youth (TYDC), ambako alipinga hatua ya baadhi ya wanasiasa kununua wapiga kura kwenye uchaguzi na kufanikisha kitendo hicho ni sawa na uroho wa  madaraka. 
 
Alisema hali hiyo ni hatari, kwani wanasiasa wa aina hiyo wanapaswa kuangaliwa kwa umakini wa hali ya juu, wanaweza kulisambaratisha Taifa.
 
Sumaye ni mmoja wa makada sita wa CCM waliopewa onyo kutokana na kile kilichoelezwa kuanza kampeni za kuwania urais kabla ya wakati.
 
Akizungumza na MTANZANIA baada ya uzinduzi wa taasisi hiyo, Sumaye alisema yupo tayari kugombea urais iwapo ataombwa kufanya hivyo.
 
Akijibu maswali kwa waandishi wa habari, alisema dhamira yake katika kujitosa kuwania urais ipo, lakini pale atakapoombwa kugombea.
 
“Nikiombwa kugombea urais nitagombea, hilo wala halina tatizo…na mjue kutangaza nia siyo kosa kwa mujibu wa kanuni za CCM, ila kosa ni kufanya kampeni kabla ya muda, wakati rais anapomaliza muda wake wagombea wengi hujitokeza kuwania nafasi hiyo, sasa hata mimi nikiombwa nitagombea,” alisema Sumaye.
 
Sumaye, anayetajwa kuwa miongoni mwa wanasiasa ndani ya CCM wanaotaka kuwania urais mwaka 2015, akizungumza katika uzinduzi huo wa TYDC, alisema kuna watu wamekuwa wakitumia nguvu ya fedha kusaka madaraka na kuwafananisha na watu wafupi wanalazimisha kupanda juu ya stuli ili waonekane mbele ya jamii kwa kutumia nguvu kubwa ya fedha.
 
Alisema watu hao ni hatari iwapo wakichaguliwa na kushuka juu ya stuli kwa vile hawataonekana tena kuwasaidia wananchi na kubainisha wamekuwa wakiwatumia vijana vibaya ili kukidhi malengo yao binafsi, yakiwemo ya kisiasa.
 
Katika kongamano hilo, Sumaye alitangaza kuwa mlezi wa vijana nchini na kuwaahidi maisha ya matumaini kwa miaka ijayo.
 
“Mimi nataka niwe mlezi wa vijana wa Tanzania nzima ili wawe na maisha ya matumaini. Ninyi vijana mtu akiwaleteeni hela chukueni kuleni halafu mnamchagua mwingine. Yaani hata Sumaye akileta msikatae hela, chukueni kuleni msimchague, maana mtu anayetumia nguvu ya fedha kusaka madaraka ya Serikali za Mitaa, udiwani, ubunge na hata urais huyo hafai na ni dhaifu,” alisema Sumaye, huku akieleza hakuja kwenye kongamano hilo kwa sababu za kisiasa.
 
Aliwaasa vijana wote, hususan waliopo masomoni wasidanganyike wala kutegemea kupata ajira za ofisini na kwamba wasiopata ajira wasikubali kutumiwa kisiasa, vijana watakaotumiwa watakuwa wamejiunga katika kundi la wala rushwa na wapokea rushwa, watakuwa wamejiunga kwenye kundi la mafisadi na la maangamizi kwa taifa.
 
Alisema kwamba vijana ni jeshi muhimu la taifa kwa maslahi ya taifa na wananchi wake na siyo jeshi la kuleta maafa katika jamii, hivyo atakuwa mlezi wa vijana kwa mambo yote na sifa anayoipenda ni mtu kuwa mzalendo wa kweli, kusimamia haki ya umma na siyo maslahi binafsi.
 
Alisema kwamba, hivi sasa Watanzania wanaelekea kwenye uchaguzi na fedha nyingi zinatembezwa kwa vijana ili watoa rushwa wachaguliwe katika nafasi wanazoomba na kudai siku hizi kumeibuka mtindo wa watoa fedha kuitwa wakarimu na wasiotoa kuhonga wao huitwa wachoyo.
 
“Mliponitaka niwe mlezi wenu nilikubali kwa sababu mimi ni mpambanaji wa vita dhidi ya matatizo na maovu hayo ambayo TYDC imeyaweka kama malengo yake makuu.
 
“Hivyo niliona nimepata wapiganaji wenzangu katika vita hii na kwa bahati nzuri wapiganaji wenyewe ni vijana ambao ni wengi, ni wenye nguvu na ndio wenye uchungu na nchi yao. 
"Mimi ninawaahidi kuwa mmempata jemadari hodari wa kuongoza vita hii na yeye jemadari amepata askari mashujaa wa kupigana vita hiyo,” alisema.
 
Alisema muunganiko huo wa wawili wa jemadari hodari na askari wapiganaji hodari wa vita utaleta ushindi usio na shaka.
 
“Kama unavyoambiwa wewe na wenzako wengine wasiokuwa na mahesabu nao huambiwa vivyo hivyo. Lakini la msingi ujue kuwa kama mtu anatumia njia hizo za mkato kutaka kuingia madarakani, huyo mtu hajiamini na wala hana uhakika na uwezo wake wa kumudu hayo madaraka anayoyatafuta, vinginevyo asingehangaika kuhonga watu,” alisema Sumaye.
 
Awali akimkaribisha Sumaye kuzungumza na halaiki ya vijana zaidi ya 300, Mwenyekiti wa TYDC, Lengai Thomas Ole Sabaya, alionekana wazi kumpigia ‘debe’ Sumaye katika harakati zake za kisiasa, kwa kusema wakati wa utawala wake na Mkapa fedha ya Tanzania ilikuwa na thamani kuliko ilivyo leo hii.
 
Sumaye alikuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 katika Serikali ya Rais Benjamin Mkapa.
Februari 18, mwaka huu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia Kamati Ndogo ya Udhibiti na Nidhamu katika kikao chake ilipendekeza kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa makada wake ambao wameanza kampeni ya kuwania urais wa mwaka 2015.
 
Uamuzi huo wa kamati hiyo ya maadili ulibarikiwa na Kamati Kuu (CC) ya CCM, iliyokutana Februari 17, mwaka huu mjini Dodoma, chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.
 
Makada waliopewa adhabu ya mwaka mmoja kwa tuhuma za kuanza kampeni za kuwania urais kabla ya wakati ni January Makamba, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
 
Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu) Steven Wassira pamoja na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini ambaye ni Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.
 
Katika adhabu hiyo, makada hao walizuiwa kujihusisha na masuala ya kisiasa ndani ya chama hicho kwa miezi 12, huku mwenendo wao wa kisiasa ukifuatiliwa chini ya uangalizi mkali katika kipindi chote cha kutumikia adhabu hiyo.
 
Kabla ya adhabu hiyo, makada hao waliitwa na kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili ambayo iliwatia hatiani kwa kutumia Kitabu cha Kanuni ya Uongozi na Maadili ya CCM, toleo la Februari 2010, Ibara 6 (7)(i).

Credit: Mtanzania

Hii ni Aina Mpya ya Uhalifu wa Kimtandao inayokuja kwa Kasi nchini Tanzania


Miongoni mwa makosa yanayofanyika  mtandaoni  ni hili  lijulikanalo kama “Phishing” ambapo kosa hili limekuwa likidumu na  kukua  kwa  kasi  sana  katika nchi mbali mbali.

Nchi mbali mbali zimechukulia uhalifu huu kuwa ni hatari kwani unaweza kuwa na madhara makubwa kwa mtendewa ikiwa ni pamoja na kupelekea kumfilisi mtu, kupata taarifa za watu kinyume na sheria au makubaliano na hata wakati mwingine kupelekea kuleta madhara mengine kama kutumika kuhatarisha mifumo mbali mbali.

Kwa kuzingatia hili nchi mbalimbali zimekuwa na sheria kali dhidi ya uhalifu huu , huku nchi za afrika kupitia umoja wa wataalam wa maswala ya usalama mtandaoni wamekubalina  kuanzisha kamati yenye watu maalaum itakayoangazia macho uhalifu huu na kutoa taarifa huku hatua zikichukuliwa.

Makampuni ya Ati-vurus nayo yametoa uzito kwenye hili na kuhakikisha  wanaunda nyezo madhubuti za utambuzi wa aina hii ya uhalifu na mara kwa mara wakiwasilisha ripoti zao.
 
Changamoto bado zipo kutokana na upungufu wa uelewa kwa wananchi mbali mbali juu ya uhalifu huu inayo sababisha  waathirika kueendelea kuwa wengi kila kukicha.

Uchunguzi umeonyesha mara nyingi panapokuwa na jambo linalo fuatiliwa na wengi, wahalifu  nao  hujipenyeza hapo na kuanza kusambaza aina hii ya uhalifu.

Kwa upande wa Tanzania, Serikali  imekuwa  ikizungumza  mara  nyingi    na  kutoa  tahadhari  mbalimbali  juu  ya  uharifu  wa  kimtandao.

Ni vizuri tukakumbushana kuwa  Tanzania imesha kamilisha rasimu ya sheria za mitandao ambazo zitatoa fursa kwa wahalifu kushughulikiwa ipasavyo na hivi karibuni TCRA nayo ilizungumzia mpango wake wa kushughulikia watumiaji vibaya wa mitandao. Hili likiwa linafuatia kampeni yao ya Futa delete kabisa.

Wakati hili linajiri, kumekuwepoa na wimbi la wahalifu wa uhalifu huu wa "Phishing" ambao   hudukua na kuchukua akauti za mitandao za watu na kuanza kusambaza taarifa zitakazo wawezesha kupata taarifa za  wengine na mara nyingine wanatengeneza akaunti feki za mitandao wakitumia majina ya watu maarufu na kuanza kuzitumia vibaya.

Waharifu  hao  wamekuwa  wakitumia majina ya watu mashuhuri na kutumia watu ujumbe wakiwataka wabonyeze link ili kujiunga na huduma kama Vikoba, Pia wamekua wakituma ujumbe wakiwataka watu wafungue tovuti n.k

TAHADHARI: Kila mmoja anapaswa kuwa makini na unapo hisi ya kuwa unaweza ukawa muathirika wa uhalifu  wa  huu kimtandao basi badilisha neno la siri na siku zote jiepushe kujibu au kufuata maelekezo yatakayo kutaka ufanye kitu Fulani.

Tajiri adaiwa kumbaka mtumishi wake (house girl) mwenye umri wa miaka 14 siku 4 baada ya kuanza kazi na kisha kukimbilia mafichoni


Mfanyakazi wa ndani, miaka 14 mkazi wa kijiji  cha Mdenge, Kata ya Likombe katika Wilaya ya Mtwara, amebakwa na mwajiri wake usiku wa kuamkia jana na kumsababishia maumivu makali na kisha kutokomea kusikojulikana.

Akiongea na FikraPevu jana Jumatatu Juni 16, 2014, Mama mzazi wa mtoto huyo, mwenye umri wa miaka 36, amesema mtoto wake amekumbana na masahibu hayo siku nne tangu aanze kufanya kazi kwa mwajiri wake aliyemtaja kwa jina moja la, Sharifu (42), mfanyakazi katika kiwanda cha kuzalisha saruji cha Alosko mkoani humo.

Amebainisha kuwa, mtoto wake alipata kazi ya kufanya kazi za ndani kwa mwajiri huyo Juni 12, 2014 ambapo ilipofikia usiku wa kuamkia leo mtoto huyo aliamua kutoroka nyumbani kwa mwajiri wake anayeishi na mke wake bila kuaga kutokana na hofu ya kuzuiwa kwenda kwao au kufanyiwa unyama zaidi na kukimbilia nyumbani kwao.

“Alivyopata kazi anasema hii sio mara ya kwanza kufanyiwa hivyo hii ni mara ya pili, usiku wa kuamkia Jumamosi ya Juni 14, 2014 alimuingilia mtoto wangu na alipomwambia atatoa taarifa akamwambia asiseme kwa mtu yeyote kwani atamfanya kama mtoto wake, sasa leo tena amemuingilia.

"Nimemkuta yule mama aliyekuwa anafanya kazi kwake amesema alihisi kuwa kuna huo mchezo lakini aliogopa kuniambia tangu Jumamosi” alisema  mama  wa  mtoto.

Kwa upande wa mtoto huyo, amesema ,“Nilikuwa nimelala usiku wa manane ndipo niliposhtuka, nilipotaka kupiga kelele alinikataza kuwa nisiseme kwa mtu kwani atanifanya kama mtoto wake, na usiku wa kuamkia leo alikuwa ameenda kuangalia mpira nilivyoshtuka alikuwa ameniingilia kimwili ndio nikaondoka asubuhi kwenda kwetu kwa maana alisema nisipige kelele”

Taarifa yatolewa Polisi
Mama mzazi wa mtoto huyo amesema wameripoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi Mtwara, kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba Mt/RB/2198/2014 ambapo mtoto huyo amefanyiwa vipimo katika kituo cha Polisi kilichopo wilayani humo na kugundulika kuwa alibakwa na kupata majeraha makubwa.

FikraPevu ilimtafuta Kamanda wa Polisi wa mkoani humo, Zelothe Stephen, ambaye hakupatikana kupitia simu yake ya mkoni baada ya kuita bila kupokelewa, huku upande wa ndugu wa mtuhumiwa wakigoma kuongelea suala hilo wakidai hawajui alipo ndugu yao licha ya kushangazwa na tukio hilo.

Chanzo: Fikra Pevu

Mwanaume aharibu mali zote za mpenzi wake baada ya kunyimwa tendo la ndoa



RB nambari TBT/RB/3478/2014  ya Kituo cha Polisi Tabata, jijini Dar es Salaam ina kesi ya dereva taksi aliyepatikana kwa jina moja la Lindoya akidaiwa kuharibu mali za Asia Hakika kwa sababu eti alinyimwa unyumba.
 
Asia Hakika anayedai kuharibiwa mali zake na dereva taksi aitwaye Lindoya.
Mlalamikaji Asia, mkazi wa Tabata – Chama na mtuhumiwa Lindoya mwenye makazi yake Mbezi – Makabe ni wapenzi wa muda mrefu sasa, lakini baada ya Asia kugundua kuwa mwenzake ana mke na watoto, akagoma kumpa tendo la ndoa, jambo lililoibua kisanga hicho.
 
Akizungumza na Uwazi, Asia alisema: “Lindoya ni mpenzi wangu, tulikuwa tunaelekea kuwa mume na mke, maana tumeishi kwa miaka miwili sasa, lakini siku zote amenieleza kuwa hana mke wala watoto, lakini nimegundua kuwa alinidanganya.

“Ana mke na watoto wawili, nikaamua nimuache aendelee na familia yake. Akakataa, anataka kunitumia tu. Nilipomkatalia ndiyo akaamua kuniharibia vitu vyangu.  Alinikuta nina vitu vya ndani nilivyonunua kwa fedha zangu,  nimepanga chumba kwa pesa yangu na aliniomba tuishi pamoja nikamkubalia.
 
“Baadaye akaanza kujenga nyumba huko Mbezi ya Makabe, nilifurahi sana niliamini kuwa tukioana tutakua tunaishi huko lakini cha kushangaza baada ya kumaliza kujenga alimfuata mkewe huko Mbeya, wakahamia na watoto wake.”
 
Alisema, mpenzi wake huyo zilipendwa, alimwambia asikanyage nyumbani kwake kwa kuwa mkewe amekuja, jambo ambalo alikubaliana nalo kwa sharti kuwa wasitishe uhusiano wao lakini Lindoya akaonekana kutoridhika.
 
Baadhi ya mali za Asia Hakika zilizoharibiwa.
“Siku moja nikiwa kazini, alifika nyumbani kwangu akafungua mlango kwa funguo wake, maana kila mmoja alikuwa na wake; akaharibu mali zote ndani, akaacha kitanda tu. Nimeumia sana kwa kweli,” alisema Asia.
 
Kwa sasa kesi hiyo ipo katika Kituo cha Polisi Tabata kwa uchunguzi ambapo jalada la uchunguzi limeandikishwa kwa namba TBT/IR/2032/2014.

Chanzo: Uwazi/GPL

Tabora: Walimu 298 walala sakafuni kwa siku 4 kufuatilia mishahara Igunga.......Hawajalipwa mishahara tangu mwezi Aprili

Walimu  wakiwa wamelala sakafuni katika ofisi za halmashauri.

JUMLA ya Walimu 298 wa shule za msingi na sekondari walioajiriwa mwaka huu Wilayani Igunga mkoani Tabora, wameendelea na mgomo wa kubaki katika na kulazimika kulala katika viti na meza katika ukumbi wa Halmashauri hiyo siku nne mfululizo wakishinikiza serikali ya Wilaya ya Igunga kuwalipa mishahara yao.

Wakizungumza na FikraPevu leo Jumatatu Juni 16, 2014 baadhi yao wakiwa na watoto wachanga wamelalamikia maisha magumu wanayolazimika kuishi kwa kuomba omba kufuatia serikali ya Wilaya kushindwa kuwalipa mishahara yao tangu mwezi Aprili mwaka huu, na serikali ya Wilaya hiyo kuwa na kauli tata kwa kile wanachodai ni kuwadanganya kuwa wangewalipa fedha zao Juni 13, mwaka huu agizo ambalo uongozi wa Wilaya hiyo lakini leo wanadaiwa kulitupilia mbali.

Aidha, wamesema tamko lililotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Rustica Turuka kuwa wangelipwa fedha kutokana na mapato yatokanayo na makusanyo ya Halmashauri hiyo, lakini leo wamelitupilia mbali tamko hilo kwa kuwapiga danadana kuwa fedha hazitoki katikahalmashauri hiyo bali zinatoka hazina.

Baadhi ya waalimu hao, Joseph Ndonga, amesema wamekubaliana kwa pamoja na kusisitiza kuwa wataendelea kuishi katika ukumbi wa halmashauri hadi malipo yao yatakapofanyika, kwani baadhi yao wamefukuzwa kwenye nyumba zo walizopanga kutokana na kushindwa kulipa kodi ya nyumba.

“Hapa tulipo ni siku ya nne kuanzia Ijumaa Juni 13, 2014, tutaendelea kuwabana hadi watupe hela zetu kwamaana sisi maeneo tunayoishi tunakabiliwa na ukata wa hela umekopa unajua mwisho wa mwezi unapata hela lakini hadi sasa hawasikilizi kilio chetu tumeitwa na DED kuwa tukubali kupokea shilingi laki moja tumeikataa kwamaana sio hela tunayodai”  alisema Ndonga

Kaimu Afisa Utumishi wa Halmashauri hiyo, Fredi Mhecho, amesema kuwa sababu ya kucheleweshwa malipo ya waalimu hao ni zoezi la kuhakiki majina kuendeshwa kwa awamu na kuanzia Aprili hadi mwezi huu zoezi hilo bado linaendelea na hadi sasa bado wanajaribu kuangalia namna ya kutatua tatizo hilo.

Polisi wazingira eneo walilopo walimu
Katika hali ya kushangaza walimu hao wamedai kuzungukwa na Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) mjini humo, hali ambayo imetajwa kuwafanya baadhi ya walimu hao kuingiwa na hofu baada ya kusimamia msimamo wa kutoondoka katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.

“Wakuu wa idara wamepiga simu Polisi kuomba msaada ili waweze kutuondoa hapa gari la Polisi liko hapa na polisi wa Kikosi Kutuliza ghasia (FFU) wapo na mabomu ya machozi wakiwa wanazunguka katika maeneo tuliyopo” alikaririwa mmoja wa walimu hao.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Susan Kaganda, amesema “Hakuna Polisi waliopo katika ukumbi wa Halmashauri, ninachojua waalimu wapo pale tangu Ijumaa hadi leo lakini kwa upande wa Polisi kuwepo katika hilo eneo hakuna”.

Tafiti zinaonyesha kuwa, walimu wa shule za msingi na sekondari mkoani humo wakati mwingine hulazimika kuacha kufundisha kutokana na tatizo la ukosefu wa maji kiasi cha kuwalazimu kwenda kutafuta huduma hiyo kwa muda mrefu bila kuingia darasani.

 
Polisi  wakiwa  wamezingira  eneo  hilo.

 Chanzo: Fikra  Pevu

Magazeti ya Leo Jumanne ya tarehe 17 June 2014

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Wanaovaa Vibaya marufuku Mahakamani Kinondoni......Mavazi ambayo hayatakiwi ni Vimini,yanayobana, yanayoacha mgogo wazi na mengine


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam imeweka kibano kwa watu wenye mavazi yasiyo na staha kuingia makahamani hapo kwa kuwazuia mlangoni. 
 
Miongoni mwa mavazi ambayo akivaa mtu anazuiwa kuingia si tu ndani ya vyumba vya Mahakama, bali pia kwenye viwanja vyake, ni yanayobana, yanayoacha mgongo wazi, fupi na mashati au blauzi za mikono mifupi. 
 
Hatua hiyo ilianza kutekelezwa takribani wiki tatu zilizopita. Kibano hicho kinamuhusu mtu yeyote mwenye shughuli mahakamani hapo wakiwemo mashahidi, wasikilizaji wa kesi na wanahohitaji huduma mbalimbali. 
 
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kweyi Rusemwa aliliambia gazeti hili jana Dar es Salaam kuwa mavazi hayo yanashusha heshima na hivyo watahakikisha wanaofika mahakamani hapo wanabadilika kimtazamo.
 
“Kama mtu anakuja kwa ajili ya Mahakama lazima avae mavazi ambayo si kero kwa mwingine. Wanaofika hapa wakiwa na mavazi yasiyostahili wataishia nje,’’ alisema Rusemwa.
 
Alitahadharisha anayefika mahakamani kuwa na khanga ili akibainika vazi alilovaa halistahili, aweze kujisitiri kwa kufunga khanga hiyo na kuingia mahakamani kupata huduma. 
 
Alisema tatizo la mavazi yasiyostahili limekuwa kubwa hususani miongoni mwa wanawake ambao baadhi hawatambui thamani yao kwa kuamua kuvaa mavazi yasiyo na heshima.
 
Hata hivyo, alisema kwa upande wa washitakiwa, ipo changamoto kubwa kwao katika kudhibiti uvaaji usiofaa. 
 
Alitoa mfano wa watu wanaofikishwa mahakamani kwa mashitaka ya kuuza miili yao, kwamba wengi hukamatwa wakiwa nusu uchi na kwamba inapotokea wakafikishwa mahakamani, hushindwa kuwarudisha. 
 
Mwandishi wa habari hii alishuhudia baadhi ya wanawake waliorudishwa langoni ambao baadhi walikuwa wakihaha kuomba khanga ili waruhusiwe kuingia mahakamani.
 
Pamoja na walinzi kudhibiti mavazi hayo mlangoni, vile vile matangazo yamewekwa kuelekeza wageni wanaofika hapo kuzingatia masharti hayo ya uvaaji.

Simulizi la Kusisimua: Mwanamke Msagaji Ameniambuka Virusi vya UKIMWI


Zuwena ( sio jina lake halisi ), ni mwanamke wa kitanzania mwenye umri wa miaka 43. Kwa sasa mwanadada huyu anaishi na virusi vya ukimwi.

Mwanadada huyu anabainisha namna alivyo pata maambukizi ya VVU kwa kujamiiana na mwanamke mwenzake, ama kwa lugha nyingine, Zuwena anaeleza namna ambavyo mwanamke msagaji alimuambukiza v.v.u wakati wakiwa na uhusiano wa jinsi moja... 

Fuatilia kisa hiki cha kufundisha na kusikitisha.

"Nakumbuka ilikuwa mwezi wa kumi na mbili mwaka 2007, nilipata tenda ya u MC katika sherehe ya kumuaga binti wa jirani yangu kule Buza Cape Town. Sherehe hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Mihogoni Pub kulekule Buza.

"Saa moja usiku nilikuwa nimeshafika ukumbini na kutoa maelekezo kwa wageni waalikwa, watu walikuwa wengi kiasi ambacho hata mama mwenye sherehe alifurahi kwa jinsi watu walivyo muitikia. Kama kawaida niliendelea na matangazo ya hapa na pale, watu walicheza na kufurahi.

"Muda wa chakula ulipowadia nilikaa pembeni nikiwa naangalia watu wanavyo kwenda kuchukua chakula. Ghafla alitokea mama mmoja mtu mzima kwa kumkadiria alikuwa na miaka kama 48 – 50 hivi. 

"Alinifata pale nilipokuwa nimesimama na kuanza kutoa sifa za hapa na pale mara umependeza , mara unaongea vizuri, mara vazi ulilovaa limekupendeza, mwisho aliniomba namba ya simu akaniambia kuwa ana sherehe ya kumuaga binti yake kwa hiyo angependa niwe MC katika shughuli yake. 

"Kwa kweli mimi nilikuwa kazini, sikukataa kumpa namba yangu. Kesho yake alinipigia simu ya kunisalimia, kwa kuwa kiumri alinizidi nilimuamkia, ila nilichokisikia masikioni mwangu ni neno ' Ahsante baby '.
 
"Nilishituka lakini nikaona ni vitu vya kawaida , kadri siku zilivyokwenda tulizidi kufahamiana nilimwambia kuwa nina saluni yangu, alinitumia vocha na mwisho alliniambia anataka kuja kupajua ofisini kwangu, nilimuelekeza akawa anakuja kutengeneza nywele, akitoa 10,000/= nikimrudishia chenji ananiambia “ utakunywa soda “ , siku nyingine anafika ofisini kwangu ananipa hela anaondoka. 

"Nikaanza kuwa na mawazo juu ya huyu mama lakini sikupata jibu. Siku moja akanipigia simu akaniambia anataka kufungua saluni yake, kwa hiyo angeomba tukutane Cape Town Bar tuongee mimi na yeye. Ilikuwa siku ya Jumapili, wateja walikuwa wengi alinisubiri kama saa moja akanipigia
kuniulizia nimekwama wapi? Nikamwambia bado nina wateja ,akaniambia funga saluni njoo nikulipe hela ya siku hiyo yote. 

"Nilifika pale akaniagizia kinywaji na baada ya hapo akatoa shilinge 50,000/= . Nilishindwa kumuelewa huyu mama akaanza kunihoji naishi na nani, nikamwambia naishi na watoto wangu watatu, baba yao baba yao amefariki  miaka miwili iliyopita . Nikamuuliza saluni anataka kufungulia wapi?

"Akanijibu achana kwanza na mambo hayo tutaongea baadaye . Tuliendelea kunywa hadi saa mbili usiku nikamwambia nawawahi watoto wangu nyumbani akaniambia nitakupeleka na gari, kusema kweli sikuelewa nia yake ni nini hivyo hata nyumbani kwangu sikutaka apajue. 

"Nilimuaga tena kwa mara ya pili akaniruhusu , kesho yake aliniletea viroba vya unga na mchele akavishusha saluni kwangu, akaniambia atanipigia simu kesho yake kuna kitu anataka kunieleza. 

"Nilianza kupata hofu, ilibidi niwaeleze rafiki zangu wa karibu ,ushauri walionipa waliniambia usikubali kutoka naye kwenda popote mbali ya pale Buza kwa sababu nia yake hatuielewi.
 
"Kesho yake akafika pale bar akanipigia simu, nikaenda ila nikapanga na rafiki yangu mmoja anifuate pale . Alipokuja nilitoa hela ili nimuagizie kinywaji, Yule mama alinizuia akatoa hela na kumuambia muhudumu alete kinywaji ila alimuomba yule rafiki yangu akae meza nyingine. 

"Kusema kweli alizidi kunichanganya, sikumuelewa.  Yule
rafiki yangu alikunywa bia ya kwanza na ya pili na akaja kutuaga akaondoka. Nilimtumia meseji kuwa asicheze mbali.

"Baada ya kama lisaa limoja hivi alipigiwa simu, akaniaga akatoa Sh. 10,000/= akanibusu akaondoka.  Yaani hapo ndipo alinifanya niwe na mawazo sana, nikaenda kuwahadithia wenzangu ....wengine wakasema labda ni msagaji, wengine wakasema ametokea kukupenda tu au anataka kaka yake akuoe. 

"Kesho yake akaja na dereva mwanamke, binti mdogo mwenye umri kati ya miaka 20 au 25, akaniambia nimsindikize mjini nikamchagulie nguo za biharusi mtarajiwa. 

"Tukaondoka wote hadi Kariakoo, akamwambia Yule dada apaki gari pembeni ili akajisaidie, Yule binti akajitambulisha kwangu kuwa anaitwa Angel, akaniuliza huyu mama mmeanza kufahamiana toka lini, nikamwambia yapata mwezi mmoja sasa. 

"Nikamuuliza mbona unaniuliza hivyo akaniambia nilikuwa nakuuliza tu. Akaniuliza unajishughulisha na nini , nikamwambia nina saluni na ni MC, akaniomba namba ya simu, Yule mama alipokuja akatuuliza mlikuwa mnaongea nini? Mimi nikamjibu kuwa dereva wako ananiuliza ile saluni ni yangu au nimeajiriwa ?

"Tukaja mpaka mtaa wa Tandamti akamwambia apaki gari atusubiri, tukaanza kuingia madukani, badala ya kutafuta nguo ya bi harusi akawa ananiambia mimi nichague nguo niliyoipenda nikawa namkatalia , tukaja mpaka mtaa wa Agrrey kuna duka linauza nguo za kutokea usiku, tukaingia pale kuna nguo nzuri tuliikuta inauzwa 120,000/= akaniambia niichukue nikakataa, tulipotoka nje kuna kaka alikuwa anauza viatu simple akaniambia nichague nikaona nisimkatishe tamaa nikachagua naye akachagua , Mara ikaingia meseji kwenye simu yangu , meseji ilikuwa  inasema hivi “ Huyo mama unamtambua vizuri au haumtambui, ni msagaji mzuri pole Aunty nakuhurumia, “ by Angel .
 
"Kwa kweli nilishtuka nikahisi nazimia , akaniambia mbona umesoma sms ukaonekana umeshtuka . Nikamwambia kaka yangu amenitumia sms mtoto wake anaumwa sana.Akaniambia twende nikupeleke , akili yangu ilishahama, nilimuambia tu hapana acha niende nikapande daladala niwahi hospitali. 

"Alitoa shilingi 10,000/= akanipa kama nauli, nilitoka speed mithili ya mshale, nilivuka mtaa wa uhuru, nusu nigongwe na gari, sikuamini macho yangu, nilifungua tena ile sms nikaisoma , ghafla akanitumia vocha ya sh. 5000/= na ujumbe uliosema “ I love you baby “.... Nilipofika nyumbani nikawapigia rafiki zangu simu nikawaeleza, walishtuka sana, wengine waliniambia namsingizia .
 
"Rafiki yangu Hawa akanishauri nibadilishe laini siku hiyo hiyo na pale saluni nisikae. Nikanunua laini mpya , nikaenda kutafuta kazi ya saluni Yombo pale kwangu nikaweka msichana.

"Nikamwambia mtu yoyote akiniuliza amwambie nimesafiri na simu sina. Na kweli huyo mama alikuwa anakuja mara kwa mara saluni kwangu kuniulizia , lakini hakupata mafanikio yoyote. 

"Matokeo yake niliamua kuhama nikapangisha nyumba yangu nikahamia Tandika nyumbani kwetu. Nilicho hofia ni kwamba kwa sababu nilishakula pesa yake nyingi, angefikia kunitaka kimapenzi, matokeo yake ningemkatalia angeweza kunifanyia chochote….
 
Je Ni Kitu gani kiliendelea? Jipatie  nakala  yako  sasa, wasiliana  na  wasambazaji  wa  kitabu  hiki  kwa  simu  namba.  0766101669.

Pia  waweza  kuwasiliana  na  mwandishi  kupitia  barua  pepe  yake : restitutamashauri@gmail.com

MAKUBWA HAYA: KABURI LA SHEHE YAHYA LAJENGWA KIKRISTO..FAMILIA YAJA JUU, KUBOMOLEWA TENA..!




MAKUBWA! Kaburi la aliyekuwa Mnajimu Mashuhuri Afrika Mashariki, marehemu Shehe Yahya Hussein limejengwa tena baada ya hivi karibuni kubomolewa na watu wasiojulikana, lakini sasa limedaiwa kujengwa Kikristo na chini ya kiwango!


Kaburi la aliyekuwa Mnajimu Mashuhuri Afrika Mashariki, marehemu Shehe Yahya Hussein baada ya kujengwa tena. Akizungumza na Risasi Jumamosi juzi jijini Dar, msemaji wa familia ya Shehe Yahya, Maalim Hassan Yahya Hussein alisema kaburi hilo lipo kwenye Makaburi ya Tambaza karibu na Hospitali ya Muhimbili, Dar sanjari na lile la marehemu Shehe Kasim Bin Jumaa.
Alisema makaburi yote yalibomolewa wakati wa Operesheni Safisha Jiji ambapo serikali kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik alikataa jiji kuhusika.
Hata Maalim Hassan alikiri si serikali iliyoyabomoa makaburi hayo bali ni wahuni wachache, lakini akasema mkuu wa mkoa aliahidi kwamba serikali itayajenga upya tena kwa kuyaboresha.

Familia hiyo ikasema inashangazwa makaburi hayo kujengwa katika mfumo wa makaburi ya Kikristo jambo ambalo halitoi picha nzuri kwa sababu wako watu wanatoka nje ya nchi kuja Tanzania kutaka kuliona kaburi la Shehe Yahya.

FAMILIA KUBOMOA
“Makaburi yale yalitakiwa kujengwa kwa kutumia kokoto maalum ziitwazo ‘mable’ na kulikuwa hakuna sababu ya kujenga ngazi ambazo watu wanaweza kukaa kama kaburi la marehemu Steven Kanumba.

“Kama marehemu alipokuwa hai hakukaliwa kwa nini akiwa amekufa akakaliwe akiwa ndani ya kaburi? Kule ni kumkosea heshima.

“Sisi kama familia tumeamua kwamba, lazima tuyabomoe makaburi yote, la baba na lile la marehemu Shehe Kassim siku ya Jumamosi (leo) na kuyajenga upya tutakavyo sisi tena kwa gharama zetu, serikali ibomoe matofali yao,” alisema Maalim Hassan.




Marehemu Sheikh Yahya Hussein enzi za uhai wake. SHILINGI MILIONI 4.5 ZATAJWA
Akifafanua zaidi, Maalim Hassan alisema Manispaa ya Ilala jijini Dar ilitoa shilingi milioni 4.5 kwa kila kaburi kama gharama za ujenzi kwa kupitia ile ahadi ya mkuu wa mkoa baada ya kubomolewa usiku wa Aprili 12, mwaka huu lakini thamani ya ujenzi uliofanywa haufikii fedha hizo.
Aliendelea kudai kwamba anaamini kuna ufisadi mkubwa uliofanyika kwenye ishu hiyo na kwamba kitendo hicho ni sawa na kuwadhulumu marehemu hao.

Alipoulizwa ni nani aliyekabidhiwa jukumu la kusimamia ujenzi wa makaburi hayo, Maalim Hassan alimtaja Shehe Mohamed Mtulya ambaye ni kiongozi kwenye Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam.

Naye mtoto wa Shehe Kassim Jumaa, Mahmud Kassim alipozungumza na Risasi Jumamosi kuhusu hali ya makaburi hayo alisema na yeye hakubaliani na ujenzi huo akisisitiza kuwa yamejengwa tofauti na makubaliano na yanaonesha tofauti na ya Kiislamu kwa sababu yana sura ya Kikristo.

“Hata mimi sikubaliani na jinsi makaburi yale yalivyojengwa. Kwanza yana sura ya Kikristo. Hatukukubaliana hivi,” alisema.

USHUHUDA WA MTU BAKI
Naye mkazi mmoja wa jijini Dar ambaye alikutwa na waandishi wetu eneo la makaburini, alisema ni kweli ujenzi wa makaburi hayo ni sawa na ule wa Kikristo kwa vile hata sehemu ya wazi iliyoachwa juu ni ndogo sana wakati kaburi la Kiislamu linatakiwa sehemu yote ya juu kuwa wazi na kuwa la chini.


“Shehe Yahya alikuwa mtu mkubwa sana. Kama mnakumbuka alikuwa akiongoza kwa kukariri Aya za Kuran Afrika Mashariki, kaburi lake lilitakiwa kuwa linalotambulisha Uislamu wake safi,” alisema mtu huyo aliyejitambulisha kwa jina la Ally Maulidi.

SHEHE MOHAMED MTULYA ANASEMAJE?
Gazeti hili lilimtafuta Shehe Mohamed ambaye anatajwa kuhusika na jukumu la kusimamia ujenzi wa makaburi hayo. Alipopatikana alisema hakuna kaburi la Kiislamu linaloweza kujengwa kwa shilingi milioni 4.5 bila kufafanua maana ya kauli yake hiyo.

Alipoulizwa gharama alizotumia kujenga makaburi hayo, alisema:
“Unajua mimi si msemaji wa serikali, andika unavyoona na mimi nitajibu.”

Msemaji wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadik hawakupatikana kwenye simu zao licha ya kupigiwa mara kadhaa. 

TUREJEE NYUMA
Shehe Yahya alifariki dunia Mei 20, 2011 jijini Dar es Salaam na kuzikwa Mei 21 kwenye makaburi hayo.
Shehe Kassm alifariki dunia mwaka 1994 na kuzikwa papohapo, wote walikuwa marafiki wakubwa.

-GPL