Showing posts with label Kimataifa. Show all posts
Showing posts with label Kimataifa. Show all posts

Hali ni mbaya Kenya: Al- Shabaab wameua watu wengine 10 usiku wa kuamkia leo , Jana walivamia na kuua watu 50




Shambulizi  jingine limetokea katika eneo la Mpeketoni karibu na Lamu , pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya watu 10.
 
Shambulizi la leo limetokea siku moja tu baada ya Al Shabaab kukiri kufanya mashambulizi yaliyowaua watu 50 Jumatatu.
Polisi wanasema kuwa washambuiaji hao walivamia kijiji kimoja usiku kucha. 
 
Kundi la Al Shabaab lilikiri kufanya mashambulizi hayo na kuambia shirika la Reuters kuwa operesheni yao ya mashambulizi itaendelea nchini Kenya.
 
Takriban watu 50 waliuawa katika mashambulizi yaliyofanyika usiku wa kuamkia Jumatatu huku washambuliaji wakishambulia hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari.

Credit: BBC

Muigizaji mrembo wa Ghana aahidi kumpiga busu mfungaji wa goli la kwanza



Wakati Ghana inajiandaa kukabiliana na Marekani leo katika Kombe la Dunia, mcheza filamu maarufu wa Ghana Nikki Samonas amesema atampa busu zito mchezaji yeyote wa Ghana atakayefunga bao la kwanza hii leo.

Kwa mujibu wa Nikki, busu hilo litakuwa zito na tamu kwa sababu yeye ni 'mbusuji' mzuri na hiyo ni ahadi ametoa.
 
Amesema kwa kuwa hayupo Brazil kwa sasa busu hilo litatolewa wakati wachezaji wa Black Stars watakaporejea.
 
 “It is unfortunate I couldn’t be at Brazil with the Black Stars to offer my support to them but I promise a very good kiss to the first Ghanaian player who scores against the U.S.

“My offer is genuine and it is my way of telling the Stars to go for gold and nothing less. I know the Black Stars will beat the U.S and win their subsequent matches but as I have said, the Black Stars player to score first against the U.S today gets a romantic kiss from me at any place of his choice”,Nikki aliiambia Showbiz :