Unapokuwa
umempata mpenzi mpya lazima utafute muda wa kuzungumza naye mambo ya msingi
yanayokuhusu wewe kwa mfano tabia za ndani ulizonazo,mambo unayyapenda nk.hapo
utakuwa mtu mwenye kujiamini sana katika uhusiano wenu.Mweleze mambo
yafuatayo:-
MWELEZE MAMBO UNAYOYAPENDA
Kujua uwezo wako na
sifa zako nzuri kutafanya ujiamini zaidi. Kila mmoja wetu ana vipawa
mbalimbali. Kwa mfano, watu fulani wana kipawa katika uchoraji au muziki,
ilhali wengine wana uwezo mzuri katika michezo au wengine wanauwezo mkubwa sana
darasani. Ikiwa ni vigumu kwako kutaja sifa uliyo nayo kwa wasiwasi labda
utaonekana unajisifia waweza kumwambia mpenzi wako kwamfano,mimi napenda sana
kuimba badala ya kumwambia mimi najua sana kuimba.
MWELEZE KUHUSU UDHAIFU
WAKO
Hili ni jambo la msingi
sana kwa wapenzi kufahamiana tangu siku za mwanzo,kufahamu mapema udhaifu wa
mpenzi wako kunasaidia kulinda makosa utakayomfanyia ambayo yamesababishwa na
udhaifu wako na kwamba halikuwa kusudio lako.Hata kama unapenda sana ngono we
usione aibu mwambie kwa sababu kweli ni kitu unachokizimia kupita kiasi, usiposema
ukweli ni tatizo kwani itafika wakati unaogopa kusema kwamba unanyege eti kisa
atakufikiria vibaya kwa sababu jana tu ulifanya nae,matokeo yake unaanza kuwaza
kuwa na mtu mwingine wa pembeni jambo ambalo si sahihi.
UWEZO WAKO KIUCHUMI
Lazima mwanzoni kabisa wa
mapenzi yenu mpenzi wako afahamu uwezo ulionao kiuchumi,kama unafanya kazi basi
kazi gani ili suala la kipato chako liwe wazi ili kuepuka kukubebesha majukumu
yaliyo nje ya uwezo wako.Kudanganya kwamba unapesa za kutosha na kazi nzuri sio
jambo la busara kwani mpenzi wako atakubebesha majukum akitambua kuwa wewe ni
mtu mwenye pesa na kazi nzuri sasa kama ulidanganya kumbe wewe ni kapuku
utakoma, mwenzio anataka umtoe out kila weekend,mara anataka Samsung galaxy
nk.utakuwa na wakati mgumu sana.
MSIMAMO WAKO MAISHANI
Suala la kitu gani
unakipa sana kipaumbele ni muhimu mpenzi wako afahamu kwani asipofahamu itakuwa
rahisi sana kukukwaza na kujikuta akiambulia kupigwa hata makofi kumbe hafahamu
wewe ni kitu gani hasa unathamini katika maisha yako,kuna watu kipaumbele chao
ni wazazi kwamba ni bora umkorofishe yeye kuliko wazazi wake hivyo ni vizuri
sana mpenzi wako akitambua mambo ya msingi kuhusu wewe na hakuna mwingine wa kumwambia
bali ni wewe mwenyewe,ukifanikisha hili mapenzi yenu yatadumu kwa muda mrefu na
mtaishi kwa furaha daima.