Showing posts with label udaku. Show all posts
Showing posts with label udaku. Show all posts

Irene Uwoya amtaka Ndikumana Yanga, mwenyewe aogopa kulogwa.....Asema Uwoya bado ni Mke wake na wanapendana sana


BINTI aliyejaliwa uzuri wa sura anayeng’ara kwenye filamu za Kibongo, anamshawishi mumewe Hamad Ndikumana aje kucheza Yanga ya chini ya kocha, Marcio Maximo.
 
Ndikumana ambaye kwa sasa anaichezea Vital’o ya Bujumbura, Burundi ameweka wazi kwamba binti huyo, Irene Uwoya ambaye ni mkewe ni shabiki wa Jangwani na amekua akimshawishi kila mara kwamba atue Jangwani ili awe naye karibu zaidi kwani hana mpango wa kuondoka Dar es Salaam kwenye kazi zake za filamu.
 
Mchezaji huyo amekiri kushawishiwa mara nyingi lakini alisema hawezi kujipeleka Yanga mpaka timu hiyo itakapomfuata, kama hiyo haitoshi aliongeza kwamba anaogopa kuishi Dar es Salaam kutokana na mambo ya ushirikina yaliyomtokea alipoanza maisha na mkewe ambaye ameshangaa watu wanaozusha kwamba wameachana.
 
“Ananitaka nije kucheza Tanzania alikuwa ananiambia nije Yanga, unajua anaipenda sana Yanga lakini nikamwambia mimi ni mchezaji ninayejiamini siwezi kuja kuomba Yanga wanisajili acha waje wao tuzungumze, yuko tayari kufanya hata ushawishi kwa wadau,” anasisitiza Ndikumana ambaye awali alikuwa akiichezea APOP Kinyras Peyias ya Cyprus.
 
Ndikumana alisema kilichomtoa Cyprus na kuja Burundi pamoja na uhusiano wake na Uwoya.
 
“Kweli nilikuwa Cyprus kama unavyosema lakini kikubwa ambacho kilinirudisha Tanzania ni pale mke wangu alipokaribia kujifungua, niliporudi tu baada ya muda nikaanza kuumwa sana na hivyo kushindwa kurudi Cyprus,” anasimulia.
 
“Tatizo hilo naweza kusema ni mambo yetu ya Kiswahili na ni huko Tanzania ndiyo kulikuwa chanzo, kuna vitu vilikuwa vinanitokea mwilini kiasi kwamba nilikuwa najikuna sana mwili mzima, hospitali nilikwenda na kupima vipimo vyote hakukuonekana kitu, kuna wakati wakaniambia ni fangasi.
 
“Nikaona hapana bora nigeukie upande wa pili wa tiba asilia, nako hali haikuwa rahisi nilizidi kuteseka ilifikia hatua najikuna mpaka vidonda vinatoka miguuni nikaona sasa na vidonda hivi nitarudije Cyprus bora nitibiwe kwanza kabla ya kuondoka.
 
“Ukweli ni kwamba nilizunguka sana kwa wataalamu mbalimbali kiu yangu ilikuwa ni kuhakikisha nakuwa sawa, nakumbuka mwanzoni kama ndani ya miezi miwili nilitumia hadi Sh6milioni kusaka tiba lakini bado ikashindikana, nilikuwa nataka kuhakikisha napona haraka ili niwahi kurudi kazini.
 
“Nilizunguka sana nakumbuka baada ya kuona Tanzania ni vigumu nikaondoka na kuja hapa Rwanda nako nilitibiwa hali haikuwa sawa, nikaenda DR Congo kidogo nikapata nafuu lakini baadaye kuna mtalaamu mmoja akanisaidia tena kwa kiasi kidogo maradhi yakapungua.
 
“Kuna mtu namjua kwamba alikuwa akifanya haya yote, hili nililiamini baada ya kumrudia Mungu, ukiacha ya Mungu pia hata hao wataalamu karibu wote nilipokuwa napita walikuwa wakimtaja sioni kama walikuwa wanadanganya kwani ni watu tofauti wote wamemtaja mtu mmoja, namuachia Mungu na nashukuru sasa nimeanza kurudi katika hali yangu.
 
“Baada ya misukosuko yote hiyo Baba yangu (Ndikumana Kitenge) kule nyumbani ana timu yake ndogo ya vijana, nikawa natumia muda huo kumsaidia majukumu ya kuwafundisha vijana na hapohapo na mimi nafanya mazoezi, nilipoona hali imeimarika nikaenda Vital’O kuwaomba nifanye nao kazi wakakubali na nashukuru walinielewa na kuniamini sasa nipo nao kwa muda.


“Sijasaini mkataba na Vital’O unajua kuna wakati  nafanya mazoezi kuna timu za Ulaya zilikuwa zinataka kunifuata nikaona niende Vital’O ili nijiweke sawa endapo watakuja wanikute katika hali nzuri lakini hao jamaa walivutiwa na mimi wakati nacheza kama beki na sasa hapa natumika kama kiungo mkabaji sijajua kama wakija watanikubali.”
 
Alikutana wapi na Uwoya?
“Unajua Irene nilimpenda kupitia filamu nilipomuona nikataka siku moja nikutane naye, nashukuru Mungu kuna siku wakati nataka kwenda Kigoma katika harusi ya dada yangu nilipitia Dar es Salaam nikakutana naye pale uwanja wa ndege.
 
“Sijabadili dini, ni kweli kwamba tulifunga ndoa ya kanisani lakini sikubadili dini nilitajwa kwa jina la Hamad Ndikumana, tulikubaliana na mke wangu tufunge ndoa mbili ya Kikristo na Kiislamu ikatangulia ile hii nyingine tukasema tutaifunga baadaye lakini muda ukawa mdogo ila tutaifunga hakuna shida.
 
Ni kweli wameachana na Uwoya?
“Kwanza nashangaa hao wanaodai nimeachana na mke wangu wanajua nani amempa talaka mwenzake? Sijaachana na Uwoya, yule ni mke wangu isipokuwa kwa sasa ni kama tumetengana na huko si kuachana labda watu wanachanganya mambo.
 
“Kuna mambo tulishindwa kukubaliana, alikuwa hataki kuja kuishi na mimi kule Cyprus, alikuwa anataka tuishi Tanzania tu, sasa mimi kazi yangu ni soka siwezi kuacha kazi ili nirudi Tanzania niishi na familia yangu bila ya kuwa na kazi hilo lilitufanya tutengane kidogo.
 
“Achana na mtoto nipo na maelewano mazuri na Uwoya hadi sasa tunawasiliana ngoja nikuthibitishie (Anainua simu na kumpigia lakini haipokelewi) nadhani atakuwa katika kazi zake, yupo safarini Afrika Kusini amekwenda kurekodi filamu na hata Krish ni mwanangu kila ninapotaka kumuona namuona bila shida.
 
“Sasa ana miaka mitatu na tumeshamwanzisha shule, anasoma (ananionyesha video fupi Krish aliyorekodiwa akihesabu namba kwa Kiingereza) nadhani sasa utaniamini unajua watu hawajui mimi na Irene ni wapenzi na tunaonana kila tunapopata nafasi.
 
“Hayo ni maneno ya watu tu, unajua Tanzania maneno ni mengi sana, kweli kuna wakati yanasemwa mengi sana ninaposikia nakutana na mwenzangu namuuliza anakataa lakini ukiacha kukataa kwake hata mimi nimeshindwa kuthibitisha hayo madai kwa hiyo nayaacha maisha yanaendelea.
 
“Kila kitu kina muda wake bado naamini siku moja nitarudi kuwa karibu na familia yangu, kwa sasa acha kwanza kila mmoja afanye yake ya kikazi, baadaye tutatulia na kuwa pamoja, watu waache kutugombanisha,”anasisitiza.

Chanzo:  Mwanaspoti

Dayna Nyange asimulia jinsi anavyoshambuliwa na Mashabiki kwa Lugha Chafu baada ya kuamua Kujichubua


Mwimbaji wa kike Dayna Nyange amezungumzia jinsi alivyokutana na changamoto nyingi baada ya kuamua kubadili rangi ya  ngozi yake na kuwa nyeupe.
 
Akiongea katika The Jump Off ya 100.5 Times Fm, Dayna ameeleza kuwa amekuwa akikosolewa na watu wengi huku wengine wakitumia lugha mbaya dhidi yake lakini yeye ameipokea vizuri kwa kuwa anaamini ni watu wanaompenda.
 
“Ni sawa kwa sababu mimi naamini ni watu wangu wa karibu na ni watu ambao wananipenda ndio maana wanakuwa wanasema japo wengine wanatumia kauli mbaya. Lakini pia ni sawa kwa sababu mimi najua hao ni binadamu na kila binadamu anajua jinsi ya kupresent kwa mtu vile ambavyo anajisikia kwa hiyo ni mimi kutumia tu akili nakipokeaje.” Amesema Dayna Nyange.
 
Ameeleza kuwa yeye anaamini hakuna kitu ambacho aliwahi kukifanya kabla kikawa gumzo au tatizo kwa watu na ndio maana watu wanaamua kulichukulia hili kama tatizo kubwa.
 
Mwimbaji huyo alitangaza uamuzi aliouchukua kufuatia changamoto hizo alizokutana nazo ingawa anaamini kila mtu anauhuru wa kufanya maamuzi kama alivyoamua yeye.
 
“Kwa hiyo mimi naweza kusema ni sawa, inawezekana kweli nimekosa. Lakini mimi kama binadamu pia nina maamuzi yangu na nina sababu nyingi tu za kufanya kile ninachokifanya. Japo nimesikia maneno mengi sana mpaka Lol..’nimeacha.!
 
“Siwezi kusema kuwa nimeacha kabisa lakini nimetoka kule nilikokuwa, sasa hivi narudi kuwa Dayna yule ambaye mnataka awe. Japo pia binadamu pia mnakitu kimoja, sifieni kile kilicho bora kabla hakijakuwa sio.” Ameaongeza.

Rose Ndauka Amkimbia Mumewe


Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka hivi karibuni aliamua kumkimbia mumewe Malick Bandawe, kisa mfungo wa Ramadhani ambapo sasa anaishi Kigogo na mama yake mzazi. 

Akipiga stori na mwanahabari wetu, Rose alisema amelazimika kwenda nyumbani kwao ili kumpisha mumewe atimize nguzo hiyo ya Uislam bila kipingamizi kutokana na kutokufunga ndoa.
 
“Mimi sifungi hivyo nimeona pia ni jambo la busara kumpa nafasi mwenzangu kwa ajili ya kufanya ibada hiyo, mwezi ukiisha nitarudi na maisha yetu yataendelea kama kawaida,” alisema Rose ambaye awali alikuwa akiishi na mumewe huyo Tandale jijini Dar.

VJ Penny Achumbiwa.....Sasa kuanza Maisha Mapya baada ya kutemana na Diamond


Mtangazaji maarufu nchini VJ Penny ambaye alikuwa mpenzi wa Diamond Platnumz amechumbiwa.  Kupitia Instagram Penny ameweka picha akiwa amevaa pete ya uchumba  na  kuandika  ujumbe  huu: “Road trip ….site her we come…cc @halimakimwana1.” 
Pia juzi  tulisikia   kuwa Penny amechumbiwa ingawa hatukupata habari kwa kina mpaka Penny mwenyewe alipoweka picha Instagram  akiwa  amevaa  pete  ya  Uchumba.

VJ Penny ambaye  inadaiwa alikuwa chaguo la kwanza la mama Diamond Platinumz ameweka picha hiyo siku moja baada ya Wema Sepetu kupost picha nyingi kwenye Instagram akiwa na mama Diamond kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kuzipa caption mbalimbali huku nyingine zikiwa na vijembe.
Tunampa hongera zote VJ Penny kwa  kuchumbiwa.

WATU WAZIDI KUMSHAMBULIA FROLA MBASHA, KUMBE MDOGO WAKE ANAYEDAIWA KUBAKWA NDO ALIREKODIWA AKIFANYA MAPENZI NA NGASA???

Copy paste by Coco master. Hili suala naliwaza sn nahisi kuna kitu nyuma ya pazia isijekua Mali mlizochuma zikasababisha kumpoteza mmoja Kwa style hii . Binafsi kuhusu suala la Mbasha sidhani na siamini kama alibaka ila tabia ya mdogo wa Frola Mbasha si nzuri, alishawahi kuonekana kwenye magazeti na video yake ya ngono aliyoicheza na mchezaji maarufu Tanzania, Sasa kama yule mchezaji hakuchukuliwa hatua yeyote ilihali huyu binti alikuwa mwanafunzi na alitoroka shule, basi Mbasha hastahili kuwa hatiani, nimemshangaa sana dada Yangu Frola Mbasha kwa kwenda kwenye Television na kumuaibisha mume wake akisahau kuwa yeye ni ubavu tena wakushoto na anayemuaibisha ni mume wake na wamebahatika kupata mtoto,maandiko yameandika mwanamke atawaacha wazazi wake na kumfuata mumewe, pia kilichounganishwa na MUNGU kamwe hakuna atakayeweza kukitengua ina maana hamkuunganishwa na MUNGU?, mdogo wako ni pornstar na wewe unafahamu, kwanini umpe ukaribu na mumeo?sumu hawaonji kwa kuilamba? Tubu msamehe mwenzio, hayo yote yanapita na maisha yanaendelea!

WAJUE WANAUME ZAIDI YA 15 WALIOWAHI KUMFAIDI KIM KARDASHIAN…

Vitu ambavyo watu wanavifanya chumbani ni siri yako na mwezi wako lakini mara nyingi  unapokua maarufu basi vitu hivi sio siri tena.Hivi sasa kim ameshaolewa na bwana Kanye lakini mikasa aliyoipata katika maisha yake ya mapenzi ndio imetufanyavibe Tanzania kuangalia kwa jicho la pili mahusiano aliyopitia bibie Kim Kardashian.Akiwa tayari ana miaka 31 , Kim amepitiwa na wanaume wengi huku wengine wakiwa ni mpango wa kando wakati tayari ana mtu mwingine. Hii ni list ya wanaume  (wanaojulikana na maarufu)ambao wameshawai kumpitia kim tokea mwaka 1994 :-
Kim-Kardashian-Featured
TJ Jackson (1994-1998)
katika interview yake na Oprah, Kim alisema alianza kutumia njia za uzazi akiwa na miaka 14 ambapo alikua ataki kushika mimba akiwa na mdogo. TJ Jackson kama ulikua hujui, huyu ni mpwa “nephew” wa Michael Jackson ambapo inasemekana ndio alikua sio tu wa kwanza kutoka naye bali wa kwanza pia kufanya naye mapenzi.
TJ-Jackson-Kim-Kardashian
Damon Thomas (2000-2004)
Unafikiri kim hakuwahi kuolewa kabla? basi kama ndio , habari ni kwamba kim akiwa na umri wa miaka 20 aliolewa na producer , Damon Thomas , ndoa iliyodumu kwa miaka minne tokea mwaka 2000 hadi mwaka 2004. Ndoa yao ilivunjika kutokana na kim kupigwa mingumi na mwanaume huyu . Pia Kim alikua akifuatiliwa kila dakika anapopumua.
Kim-Kardashian-and-Damon-Thomas
Julian St. Jox (2001)
Huyu Jamaa ambaye ni muigizaji wa muvi za kikubwa (pornstar) ambaye  alimmaliza kim wakati kim akiwa yupo kwenye ndoa katika party moja waliokua nae. Julian alisema kim alitokea katika  hoteli ya Wyndham na mwanaume mweusi ambae anahisi alikua mme wake kipindi hicho, Damon ambapo alimfuata kim huku akiwa na pornstar mwenzake wa kike Emily Ann ambapo walianza kucheza na mizuka kupanda ambapo watatu hao walitafuta chumba na mengine yakabaki kua story.
Julian-St-Jox--Kim-Kardashian
Ray J (2002 – 2003)
Hivi kunaaja ya kuielezea hii kitu ? kwa wale wanaopenda picha za ngono , mtakua mmeshaona mkanda wa ngono kati ya Ray J na Kim Kardashian uliovuja. Kipindi mkanda huo unarekodiwa , Kim Kardashian alikua bado yupo kwenye ndoa yake na Damon. Duh! jamaa alikua bwege kweli…Kumbuka mkanda huu wa ngono ulivuja mwaka 2007 japokua ulirekodiwa mwaka 2003. Kama ulikua hujui mwaka 2007 ndio ulikua mwanzo wa kipindi cha Keeping up with the kardashians na wataalamu wanasema kipindi hiki kililenga kumsafisha kim bila kujua mafanikio ambayo kingepata.
Kim-KArdashian-and-Ray-J
Nick Lachey (2006)
Mwanamuziki huyu kutoka bendi ya 98 Degrees alitoka na Kim Kardashian kwa wiki moja tu na mahusiano yake yakavunjika. Nick alikua ametoka kuvunja ndoa yake na mwanamuziki Jessica Simpson na muda mchache akaanza kutoka na kim. Nick anadai Kim alimtumia kujipatia umaarafu baada ya kusema kim aliwalipa mapaparazi zaidi ya 30 kumpiga picha walipokua wanatoka movies. Nick anasema picha zake kati yake na Kim ndio ulikua mwanzo wa mafanikio ya Kim.
Nick-Lachey-and-Kim-Kardashian

Nick Cannon (September 2006- January 2007)
Hehehe, unajua kwanini Nick Cannon alimtosa Kim kardashian ? wapenzi hawa walikua wakiishi vizuri hadi pale Kim alipoulizwa na Nick kuhusu kuwepo kwa mkanda wa ngono kati yake na Ray J na Kim kumdanganya na kumwambia hamna kitu kama hicho. Nick alisema hataweza kumsamehe Kim kwa uwongo aliyomwambia.
Nick-Cannon-and-Kim-Kardashian
 Reggie Bush (2007)
Huyu ni mchezaji wa mpira (NFL) wa marekani ambae alikua na mahusiano na kim kwa zaidi ya miaka miwili hadi mwaka 2009 lakini mahusiano yao yalikua yakutosana na kurudiana baadae.
reggie-Bush-and-Kim-KArdashian
Evan Ross (2007)

Huyu ni mtoto wa mwanamuziki wa zamani na maarufu kabisa nchini marekani, Diana Ross. Wawili hawa walitoka pamoja kipindi kardashian alipuamua kupumzisha penzi la Reggie Bush.
Evans-Ross-and-Kim-Kardashian
Christiano Ronaldo (April 2010)
Hiki kipindi mrembo Kim alikua nchini Hispania kimapumziko ndipo alipokutana na Christiano Ronaldo. Kipindi hicho christiano akiwa na miaka 25 huku Kim akiwa na 29 , wawili hao walionekana kwa mara ya kwanza wakipeana mahaba ndani ya siku 3 ambazo kim alikua nchini humo.
Christiano-Ronaldo-Kim-Kardashian
Shengo Deane (April 2010)
katika interview yake ya Piers Morgan kim alieleza jinsi alivyohuzunika kuhusu sex tape yake ya mwaka 2007 lakini chaushangaza aliweza kuonyesha mahaba yake na Shengo Deane katika kipindi cha keeping up with the Kardshians. Kumbuka mu-Australia huyu alikua ni bodyguard wa Kim Kardashian.
Shengo-Deane-and-Kim-Kardashian
Miles Austin (June 2010)
Huyu naye ni mchezaji wa American Football. Wawili haya walidumu kwa miezi na hakuna sababu ya msingi ya kutengana kwao zaidi ya long distance.
Miles-Austin-and-Kim-KArdashian
Michael Copon (October 2010)
huyu ni muigizaji aliyemjua Kim kwa zaidi ya miaka 11 na baadae wakafanya yao japokua uhusiano wao haukudumu kabisa kwa alichokisema Michael kwamba Kim anatabia za kitoto.
Michael-Copon-and-Kim-Kardashian
John Mayer (October 2010)
Hii ilikua mwishoni mwa mwezi October ambapo kim aliamua isiwe tabu na kumuachia mwanamuziki na producer , John Mayer ale mema ya nchi
Jon-Mayer--and-Kim-Kardashian
Gabriel Aubrey (November 2010)
Huyu ni model kutoka nchini Canada na kipindi anatoka na Kardashian alikua ana mtoto wa miaka miwili aliyezaa na msanii Halley Berry.
Gabriel-Aubrey-and-Kim-Kardashian
Kris Humphries (2010-2013)
Hii ilikua ndoa ya pili kwa kim Kardashian. Hii ndoa kati ya Kris Humphries na Kim Kardashian ni maarufu kwasababu iliweza kudumu kwa siku 72 tu ! Ndoa ya mcheza kikapu huyu wa NBA na Kim ilifika mwisho baada ya Kim kuhisi kwamba hamna jema litakalotokea baadae na Kris pia kuhisi Kim anachepuka kwa rapper Kanye West.
kris-humphries-and-kim-kardashian
Kanye West (2007 hadi leo)
Unashangaa nini sasa ? Kim Kardashian alikua akichepuka kwa Kanye kipindi ana mahusiano na Reggie Bush na Kris Humpries.Kwasasa Kim na Kanye ni wanandoa na wanamtot mmoja, North West.
Kim-Kardashian-And-Kanye-West
Duh, hivi kwa hii list wewe ungekubali kumuoa Kim kwa mara ya tatu kama alivyofanya kanye tena ukizingatia kuna wengine waliopita sema bila uhakika kama 50cent, The Game, Brett Lockett, Scot Storch  na wenine wasio celebrities ?

LULU AGEUKA BONDIA, AMTEMBEZEA KICHAPO BONGO MOVIE MWENZAKE, SOMA FULL STORY HAPA


MASTAA wa kike wanaotingisha Bongo, Elizabeth Michael ‘ Lulu’ ( pichani) na Husna Maulid, ilibaki kidogo wazichape Kabla ya tukio hilo, awali wawili hao waliwahi kuingia kwenye bifu baada ya kudaiwa walikuwa wanamgombea pedeshee mmoja wa mjini, kila mmoja akijipa uhalali wa kumilikiwa.

Tukio hilo bichi kabisa lilitokea Juni 16, mwaka huu , Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo chanzo kinasema , wadada hao walikuwa wakirekodi sinema ambayo haijajulikana jina lake . “Ni kweli walikuwa wakirekodi filamu , lakini kuna muda walizinguana ila watu wanasema bado wanakasirikiana kutokana na ile ishu ya kunyang’ anyana mwanaume . “Joti ( Lucas Mhuvile – yule komediani wa Kundi la Orijino Komedi ) alikuwepo eneo la tukio na ndiye aliyewapatanisha, ” kilipasha chanzo hicho. Joti alipotakiwa kuzungumzia ishu hiyo , alikiri kutokea lakini kwenye kurekodi filamu huku akikataa kufafanua.

 “We’ jua kuwa ilikuwa filamu , si ugomvi serious,” alisema Joti . Lulu hakupatikana kuzungumzia ishu hiyo lakini Husna alipopatikana alisema : “Tulitofautiana kikawaida tu kama wanawake lakini hatukufika kwenye mambo ya kupigana. ”

NDOA YA FLORA MBASHA CHALI

BAADA ya kudumu kwa zaidi ya miaka 10, imebainika kuwa ndoa ya mwanamuziki mahiri wa muziki wa Injili Bongo, Flora na mumewe Emmanuel Mbasha ipo chali kwa maana ya kuanguka huku ikidaiwa kuwa, kusimama imara tena inawezekana lakini ni kazi kubwa, Amani limefukunyua mazito.
Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha.
Hilo limejitokeza wiki moja baada ya madai ya mwanaume huyo kudaiwa kumbaka shemeji yake na kesi ipo polisi.
Imeelezwa Flora na mumewe ambao walifunga ndoa Agosti 22, 2002 wamepita katika migogoro mizito lakini wawili hao walikuwa wakiyamaliza kifamilia hadi kufikia hili la hivi karibuni ndilo lililoziba mataumaini ya wawili hao kuishi kama mume na mke.
Chanzo kilicho karibu na wawili hao kimeeleza kuwa, mzizi wa wawili hao kugombana ulichochewa na mwanamke mmoja (jina tunalo) ambaye alikuwa akikinzana na ushauri wa Mbasha mara kwa mara.
“Kuna vitu Mbasha alikuwa akimshauri huyo mama lakini walikuwa wakipishana Kiswahili  na hapo ndipo tatizo lilipokua hadi kufikia hatua ya kumwagana,” kilisema chanzo.
Flora na mumewe Emmanuel Mbasha wakiwa kwenye pozi.
TUJIUNGE NA MBASHA
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Emmanuel alizungumza na mwandishi wetu ambapo alikiri ndoa yake haina uhai tena na si rahisi kurejea katika hali ya kawaida licha ya kudai kuwa bado anampenda mkewe.
“Tulikuwa tunagombana sana na Flora lakini tulikuwa tukipatana ila mama… (anamtaja jina) alichangia ugomvi,
Flora naye alikuwa na nyendo zake mbaya, kuna wakati alikuwa anatoka kwenda gym (sehemu ya mazoezi) anachelewa kurudi ikafika wakati na nguvu ya ndugu wa mke ikawa kubwa kiasi cha kunizidi mimi na hapo ndipo mambo yalipofikia pabaya kabisa.”
FLORA ATIMKA NYUMBANI
Mbasha anaendelea: “Ugomvi ulizidi, ilifika wakati tulipishana kiasi cha yeye kuondoka nyumbani na kwenda kuishi katika nyumba ya wageni kwa miezi kadhaa wakati huo.
“Ndani ya ugomvi huo nilisikia mengi, baadhi ya watu wananiambia mke wangu anaonekana na Prado na mwanaume mwingine mwenye pesa, iliniuma sana ingawa sijawahi kumuona moja kwa moja,” alisema Emmanuel.
Kuhusu ugomvi huo, hivi karibuni Flora alikaririwa katika vyombo vya habari akisema hana tatizo na mumewe na ameshasamehe na kusahau yote yaliyopita hivyo ajitokeze tu ili akajibu mashitaka ya kudaiwa kubaka binti wa miaka 17 yaliyofunguliwa.
“Mimi sina tatizo kabisa na mume wangu, nimeshasamehe yote yaliyopita, kuhusu mashitaka ningeweza kuyafuta kama ningekuwa mimi ndiye niliyemshitaki,” alisema Flora.
FLORA ADAIWA KUHAMIA KWA GWAJIMA
Wakati gazeti hili likiendelea kusaka undani juu ya sakata hili, kuna chanzo kingine kilipenyeza data kuwa baada ya ugomvi kuwa mzito, Flora alihamia kwa Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dar, Josephat Gwajima ambako ndiko alikuwa akisali kila Jumapili.
“Kwani nyinyi Global hamna habari? Flora amehamia kwa Gwajima Jumapili iliyopita, kwanza alihudhuria ibada jioni akaenda kuishi maana Gwajima ni mchungaji wake kwa sasa,” kilisema chanzo.
GWAJIMA ACHOMOA
Ili kupata mizani ya madai hayo, juzi Amani lilimpigia simu Mchungaji Gwajima na kumuuliza kama kweli Flora amehamia kwake kufuatia ugomvi kati yake na mumewe ambapo alikataa katakata.
“Flora hayupo hapa…mnataka niwaambiwe yuko hapa  halafu vyombo vya habari muanze kuandika vibaya? Hakuna kitu kama hicho,” alisema Gwajima.
KWA NINI CHALI?
Ndoa kuwa chali ni ile ambayo imeanguka lakini inaweza kusimama tena tofauti na ndoa kuvunjika. Global iliwahi kuandika NDOA YA THEA CHALI baadaye ikasimama tena. Thea ni msanii wa filamu alifunga ndoa na Michael Sangu ‘Mike’ ambaye pia ni mwigizaji.
Flora na mumewe Emmanuel Mbasha wakilishana keki.
Wakati Emmanuel akizungumza na mwandishi wetu, alikiri kuwa Flora ameshamgeuka na nguvu kubwa imemuingia ndani ya moyo wake hivyo kuna ugumu sana wa kurudiana.
“Flora ambaye nilitegemea awe msaada katika hili lakini amefikia steji ya kuacha kunisikiliza, anasema haniamini, kwamba ninaweza kumfanyia lolote, sasa si bora kama anataka tuachane kwa heri kuliko kuniundia zengwe ambalo linataka kunipeleka mimi jela?” alihoji Mbasha.
Kutokana na mvutano huo pamoja na kesi hiyo ya kudaiwa kubaka inayomwandana Mbasha ni dhahiri kwamba kila mmoja hana imani na mwenzake tena hivyo suala la wawili hao kuishi kama zamani linakuwa gumu kuliko ngamia kupenya kwenye  tundu la sindano.
Emmanuel Mbasha alishitakiwa katika Kituo cha Polisi cha Tabata Shule, Mei 30, mwaka huu kwa madai ya kumbaka shemejie.Uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea hadi sasa shitaka ambalo mwenyewe amelikanusha.

IRENE UWOYA MAPENZI HADHARANI, PICHA ZAO WAKILA (URODA) ZAWEKWA INSTAGRAM,





Msanii kutoka Tanzania House of Talent Msami Giovanni ambaye kwa wakati huuana hit na ngoma yake ya Sound Track kwa wakati huu inasemekana eti yuko katika dimbwi zito la mahaba na muigizaji maarufu wa Bongo Movie Irene Uwoya
Baada ya kuulizwa Msami mwenyewe, alikataa kujihusisha kimapenzi na Uwaoya lakini girlfriend wake ambae wamegombana kwa sasa juu ya swalahilo, amefunguka yote.
Rehema ambaye pia ni Dancer mkali sana maarufu akatiririka kuwa ni kweli taarifa hizo anazo ila ana uhakika Msami atarudi kwake wala hana Wivu na Uwoya
na anachofahamu Irene Uwoya alimlaghai Msami kwa kumwambia anataka kuwa meneja wake kwa kuusimamia muziki wa Msami, sasa tangia hapo wawili hao wakazama kwenye Dimbwi zito la mahaba

UCHAWI watajwa kutawala katika penzi la Ray na Chuchu Hans

Batuli afunguka..."Sijawahi kumpenda mwanaume kama nilivyompenda Mtunis"



KWA mara nyingine, staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf  ‘Batuli’ amemwaga data za kimapenzi akidai hajawahi kumpenda mwanaume kama alivyompenda Nice Mohammed ‘Mtunis’.
 
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Batuli alisema licha ya kuwa walimwagana na staa huyo lakini hatokuja kupenda mwanaume kama alivyompenda Mtunis.
 
“Nilivyompenda Mtunis ni ngumu sana kumpenda mwanaume mwingine kama hivyo na kwa kawaida kupenda huwa ni mara moja tu mengine tutadanganyana,” alisema Batuli.
 
Hivi karibuni Batuli aliripotiwa kutikisa ndoa ya Mtunis ikidaiwa kuwa bado ana uhusiano naye lakini cha ajabu mtoto wa kike hakuonesha dalili zozote za kukanusha taarifa hizo.

Penny afunguka: Sitaki kusikia habari za Diamond....Nina mpenzi wangu mwingine





Zilipendwa wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’,  amefunguka kuwa hataki kumsikia mpenzi wake huyo wa zamani kwa madai kuwa amefungua ukurasa mpya wa uhusiano na mtu ambaye hata hivyo hakuwa tayari kumweka wazi. 
 
Penny alisema hayo hivi karibuni jijini Dar wakati akizungumza na Risasi lililotaka kujua anazungumziaje tuzo saba za Kilimanjaro alizojizolea Diamond ambapo  majibu yaliyopatikana yalikuwa: “Wanaotakiwa kuzungumzia hili ni mkewe na ndugu zake, mimi sitaki.”
 
Alipoulizwa mke wa Diamond ni nani alisema: “Mnamjua” na kuicha historia ikibaki kuwa Penny na msanii huyo waliwahi kuwa katika mapenzi mazito ya njiwa kabla ya kumwagana na mwanamuziki huyo kumrudia mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu, ambaye mwenyewe anapenda aitwe mke mtarajiwa. 


Wema awagombanisha Diamond na Prezzo.....Prezzo ajisifu kumvua nguo Wema,Diamond awa mbogo


HUU NDIO UKWELI KUHUSU MAHUSIANO YA BOND NA WASTARA...!



ANATOKA KIMAPENZI NA WASTARA?
Nakukubali sana kaka Bond lakini napenda kukuuliza kwamba kuna madai kuwa unatoka kimapenzi na Wastara Juma (mwigizaji).

BOND: Siyo kweli. Mimi ni meneja wa Wastara. Pia ni mwongozaji wake wa filamu kwa hiyo tuna mikataba mingi ya kufanya kazi muda mrefu sana. UHUSIANO NA AUNTY LULU
Kiukweli kama una uhusiano na Aunty Lulu (Semagongo) mwache tu kwa sababu hutamuweza, skendo zake zinatisha lakini mimi nakushauri usimuache hivihivi, mshauri vizuri, awe mwelewa kwani anatakiwa kuwa na msimamo mzuri. Msomaji, 0764158569.
BOND: Asante, Aunty Lulu nilishaachana naye muda mrefu lakini huwa naendelea kumshauri vitu vingi kwa hiyo yeye ndiye anayeamua kuchukua ushauri au kuacha. OA SASA
Kuwa na uhusiano ni sawa kwani umri unakata mbuga, kwa maoni yangu uoe sasa. Msomaji, 0785606175.

BOND: Asante nitalifanyia kazi hilo, namuomba Mungu anijalie. USHAURI
Mimi napenda kuigiza na kipaji ninacho lakini bado mchanga kisanaa ila natamani kutimiza ndoto yangu nifanyeje? Naomba nisaidie. James Salamba, 0768558834.

BOND: Ongea vizuri na wazazi wako kwa sababu siku hizi kuna shule nyingi zinazofundisha sanaa ujiunge nazo au uende kwenye vikundi vya sanaa, naamini utatimiza ndoto yako. FILAMU NGAPI? ANA MCHUMBA?
Mpaka sasa una filamu ngapi na je, una mchumba? Msomaji, Mwanza, 0765757273.

BOND: Nina filamu saba mpaka sasa na nina mchumba.

UTULIVU
Nakukubali sana kaka ila naomba utulie. Mariam Said, Gairo, 0656977555.

BOND: Asante sana na mimi siku zote nimetulia huwa sihangaiki. ALISHAKUWA TEJA?
Nasikia ulishawahi kuwa teja, ni kweli? Frank, Mwanza, 0752157695.

BOND: Sijawahi na ninamuomba Mungu aninusuru. AUNTY LULU TENA Kwa ushauri wangu achana na umsahau kabisa huyo Aunty Lulu. Specioza, Mwanza, 076507479.

BOND: Asante ila kwa pamoja ninaomba tumuombee Aunty Lulu abadilike pia tuendelee kumshauri. ILIKUWAJE?
Ilikuwaje mpaka ukaachana na Aunty Lulu maana mlikuwa mnapendana sana? Salumu Kabunda, Iringa, 0763236597.

BOND: Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho, naona mwisho wetu ulikuwa wa hapahapa duniani. WALIMWAGANA KITAMBO

Vipi kaka bado mnaendelea na uhusiano wa kimapenzi na Lulu Semagongo au mmeshamwagana? Zamrata Makame, Dar, 0688909490.

BOND: Tulishamwagana siku nyingi. 

NAOMBA AWE MCHUMBA WANGU
Bond namkubali kwenye mambo yake na kwa vile hajaoa naomba achukue namba yangu, nahitaji awe mume wangu. Ashura, Mtwara, 0712231020. 
BOND: Nashukuru na nimefurahi kwa kunikubali ila nina mchumba tayari, nakuombea kwa Mungu akupatie mume mwema. 

Avunja Ndoa yake kwa kutamani maisha ya Wema Sepetu.....