Showing posts with label Matukio. Show all posts
Showing posts with label Matukio. Show all posts

Mwanamke Aliyemng'ata Hausigeli na kumchoma Pasi Aachiwa


Mtuhumiwa wa kesi ya kujeruhi kwa kumng'ata sehemu mbalimbali za mwili  mfanyakazi wa ndani, inayomkabili Amina Maige (42) amepatiwa dhamana jana baada  ya mahakama kuthibitisha kuwa hasira kutoka kwa wananchi zimepungua.
 
Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Yohana Yongolo alisema ameridhishwa na ufafanuzi uliotolewa na Mwendesha mashitaka wa Serikali pamoja na Wakili wa mshitakiwa kuwa haki ya dhamana itolewe kwa kufuata masharti na kwamba hakuna uhalifu wowote utakaofanyika dhidi ya mshitakiwa huyo.
 
Hakimu  Yongolo alitoa masharti ya dhamana ambayo yalimtaka Maige kutoondoka nje ya Dar es salaam bila ya ruhusa ya mahakama hiyo.
 
Pia alitoa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminiwa kutoka taasisi inayotambulika hapa nchini ambapo mdhamini huyo anaweza kuwa mwajiriwa, mfanya biashara na mkulima.
 
Alisema wadhamini hao watatakiwa kusaini hati ya makubaliano kwa kila mmoja kulipa Sh milioni tatu.
 
Aliongeza kuwa kesi hiyo itasikilizwa Julai 22 mwaka huu.
 
Maige alidaiwa Januari mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alimng'ata na kumchoma na  pasi  sehemu mbalimbali za mwili wa  mfanyakazi waje wa ndani Yusta Kashinde (20) na kumsababishia maumivu mwilini.

Kondomu zakutwa kwenye ukumbi wa bunge


Inaweza kuonekana ni kituko cha aina yake, lakini ni kweli kimetokea kwenye Ukumbi wa Bunge la Kaunti ya Nairobi na kuwaacha wabunge vinywa wazi. 
 
Katika hali isiyo ya kawaida, boksi la kondomu lilikutwa ndani ya ukumbi huo na kuwashtua wabunge wote akiwamo spika wa bunge hilo.
 
Mwakilishi wa eneo la Karura, Kamau Thuo ndiye aliyekuwa wa kwanza kuliona boksi hilo na kuwashtua wabunge wengine hali iliyoibua mjadala mzito.
 
Kutokana na sintofahamu hiyo Spika Alex Ole Magelo aliwataka wahudumu kufungua boksi hilo kujua kilichomo ndani yake ndipo walipokuta kondomu.
 
“Nafahamu wote humu ni watu wazima, lakini ninachoshangaa ni nani ambaye ameleta kondomu hizi ndani ya ukumbi huu,” alihoji Spika Magelo.
 
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Afya, Manoah Mboku aliwaondoa hofu wabunge na kueleza kuwa kondomu hizo zilipaswa kuwekwa kwenye vyoo vya wanaume hata hivyo kwa bahati mbaya zikapelekwa mahali kusikohusika.

Mume wa Flora Mbasha akamatwa na kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za Ubakaji.....Ashindwa masharti ya dhamana, apelekwa Rumande

MSANII Emmanuel Mbasha (32) na mume wa Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, amefikishwa  Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka mawili likiwemo la ubakaji.

Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luago.

Wakili wa Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.

Katuga alidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam,  kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa).

Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa alimuingilia kwa nguvu  mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa).

Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo .Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana.

Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikali na mwingine kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. milioni 5.


Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alipelekwa rumande na kesi iliahirishwa hadi Juni 19, mwaka huu itakapotajwa.

Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi alisindikizwa katika basi la Jeshi la Magereza kwa ajili ya kwenda kuanza maisha mapya mahabusu ya Keko, jijini Dar es Salaam.

(UTABILI) WASANII 20 WA BONGO MOVIES KUFARIKI MWEZI HUU, SOMA HAPA

Hamida Hassan na Gladness Mallya
HUKU makovu ya maumivu ya kuondokewa mfululizo na mastaa wanne wa filamu za Kibongo katika kipindi cha mwezi mmoja yakiwa hayajapona nabii naye ameibuka na kuweka wazi utabiri wake mzito kuhusu wasanii nchini hivyo kuwa sanjari na Maalim Hassan Yahya Hussein.


Maalim Hassan Yahya Hussein akiwa kwenye ofisi za Global Publishers. Hata hivyo, kabla ya kusonga mbele, tujikumbushe kwamba mastaa waliotangulia mbele ya haki kwa kufuatana ni
Adam Philip Kuambiana, Recho Leo Haule, George Otieno Owino ‘Tyson’ na Said Ngamba ‘Mzee Small’.

Kabla ya kifo cha Mzee Small, mtabiri maarufu nchini, Maalim Hassan ambaye ni mrithi wa baba yake marehemu Sheikh Hussein Yahya alitabiri kutokea vifo zaidi hadi Aprili mwakani.
Katika mahojiano, Maalim Hassan alisema mastaa wengi duniani wataendelea kuaga dunia katika kipindi hicho cha mwaka mmoja wa utabiri, lakini alitoa masharti kwa wasanii kuyazingatia ili kujikinga na vifo hivyo.


UZITO WA UTABIRI MPYA
Achana na Maalim Hassan, safari hii ameibuka Nabii wa Huduma ya Ufufuo iliyopo Buza jijini Dar es Salaam, Yaspi Paul Bendera (pichani) ambaye amekazia kuwa vifo kwa wasanii wa Kibongo vitaendelea.
Akizungumza bila hofu na gazeti hili juzu, Nabii Bendera alisema: “Nimeona kwamba, ndani ya mwezi huu (Juni) watakufa wasanii 20. Huu si utani, ni maono.”

Nabii wa Huduma ya Ufufuo iliyopo Buza jijini Dar es Salaam, Yaspi Paul Bendera. 

MASHARTI
“Hakuna masharti magumu, Mungu anawapenda wasanii, lakini ikiwa wanataka kuepukana na vifo ninavyoviona mimi, waje kanisani kwangu niwapake mafuta matakatifu.
“Wanatakiwa kumgeukia Mungu sasa, hali siyo nzuri. Nasisitiza waje niwapake mafuta matakatifu, vinginevyo wataendelea kupukutika.”


ATUMA UJUMBE
Nabii huyo aliendelea: “Kuna msanii mmoja anasali kanisani kwangu, anaitwa Herieth (Chumila). Nilimpa huu ujumbe awafikishie wenzake. Anayepuuza na apuuze lakini nawahakikishia wakimgeukia Mungu haya mabalaa hayatawakumba kamwe.”


MAMA WA BONGO MUVI SASA
Ijumaa lilisaga lami huku na huko ili kuonana na Herieth ‘Mama wa Bongo Muvi’ kwa lengo la kuthibitisha kama kweli alipewa ujumbe huo na Nabii Bendera awafikishie wenzake.
“Ni kweli nasali pale, ni kweli pia nilitumwa na Nabii Bendera nikazungumze na wasanii wenzangu kuhusiana na maono aliyooneshwa.

Marehemu George Otieno Owino ‘Tyson’ akiwa na Mboni Masimba enzi za uhai wake “Naamini utabiri wake kwa sababu nasali pale na siku aliyotabiri mambo hayo ndiyo siku aliyofariki dunia Mzee Small, nawashauri wasanii wafuate ushauri huo, waende tu kwani wakipakwa mafuta hayatawadhuru kwa lolote kwa sababu amekuwa akitabiri mambo mengi na yametokea,” alisema Mama wa Bongo Muvi.

APINGWA NA MCHUNGAJI MWENZAKE
Licha ya utabiri huo wa aina yake wa Nabii Bendera, mchungaji mmoja wa makanisa ya kiroho ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini kwa kuhofia malumbano alipingana na utabiri huo akisema ni gia ya kutafutia waumini.
“Hakuna kitu kama hicho. Aseme anataka kupata waumini wengi. Kama kweli yeye alioneshwa hayo maono kwa nini asiishie kuwaombea tu? Kwa nini amesema waende kanisani kwake akawapake mafuta na asiwaelekeze waende kwenye makanisa yaliyo karibu nao?
“Huyo anataka waumini, asidanganye watu. Mungu ninayemwamini anaishi ndani ya nafsi ya mtu. Kama kweli aliona hayo, dawa yake yalikuwa maombi tu, siyo kwenda kupakwa mafuta, tena na yeye mwenyewe,” alisema mchungaji huyo.


Marehemu Recho Leo Haule enzi za uhai wake. Akaongeza: “Halafu itakuwaje avione vifo na kinga yake? Hapo naona kuna kitu. Hata hivyo, ninavyojua mimi kifo ni ahadi kutoka kwa Mungu, yeye ndiye anayepanga kwa sababu anatujua vizuri watu wake.”

WASANII WANASEMAJE?
Juzi, Ijumaa liliwatafuta wasanii wa filamu za Kibongo na kuwaeleza kuhusu utabiri huo ambapo walitoa maoni yao. Wa kwanza kabisa alikuwa ni Aunt Ezekiel ambaye alisema:
“Baada ya vifo vya wenzangu nimeingiwa na hofu kubwa, namuomba Mungu atuepushie mbali hilo.”


WILLIAM MTITU
“Huyo nabii ni muongo sana, naamini vifo vyote ni mipango ya Mungu mwenyewe. Kama ni mkweli basi awataje kwa majina watakaokufa na wafe kweli na wala si kutaja tu idadi.
“Kiukweli wasanii tumechoka na hawa watabiri, tunaomba serikali itusaidie kuwachukulia hatua, wakamatwe haraka, yaani tuna uchungu mpaka basi, au kama vipi tuletewe tuwapige mangumi.”
MSANII KITALE
“Naamini binadamu kufa ni mipango ya Mungu hakuna anayeongea na Mungu, ninachoamini nabii aliyekuwepo ni Musa tu ambaye alikuwa anatabiri kitu na kikatokea.”


Marehemu Adam Philip Kuambiana,enzi za uhai wake. 

HALIMA YAHYA ‘DAVINA’
“Jamani kila kukicha wanajitokeza watabiri na manabii wengi, mimi siamini katika hilo alilolisema, wengine wanataka tu biashara zao ziende, tukifa ni mpango ya Mungu.”


SIMON MWAKIFWAMBA
“Mimi naamini, maana ufuska umezidi, kuna madai kwamba watu wanasagana, ushoga, wasanii kuzungukana wao kwa wao kama kandambili kimapenzi na ushirikina.
“Kutokana na mambo haya yote lazima Mungu atuchape fimbo, hivyo mimi nitaenda na watu wangu kwa huyo nabii kwa sababu anahubiri Neno la Mungu na siyo mganga kama wasanii wengi wanavyoabudu waganga.
“Nikienda peke yangu nitaambiwa nimesikia mwenyewe sasa nitaongozana na wasanii wengine ili tukasikie wote.”


ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’
“Kiukweli inatisha na inaogopesha lakini mimi ninasali kwa imani yangu na siwezi kusema utabiri hamna au upo kwani hata kwenye Biblia upo ila siwezi kujua huyu anasema kweli au uongo kwa sababu nabii hana alama.”


Marehemu Said Ngamba ‘Mzee Small’ enzi za uhai wake. AISHA BUI
“Mimi ninachoamini hakuna binadamu anayejua kesho kitatokea nini, kama yeye mtabiri kweli basi na yeye ajitabirie atakufa lini.”


SABRINA RUPIA ‘CATHY’
“Mimi namwamini Mungu, pia kila msanii aliyekufa ni ahadi ya Mungu, nikifa leo naamini Mungu amenipenda na watu wasiwe na wasiwasi na kifo changu.
“Huyo nabii ni nani mpaka ajue tutakufa? Hakuna kitu kama hicho, mimi siamini kabisa. Kikubwa wasanii tunatakiwa tumwombe Mungu kwani ndiyo kila kitu.”


MTAZAMO
Mtazamo wa gazeti hili si kuwapa hofu wasanii bali kupeleka ujumbe kwamba Mungu ni kila kitu na si vinginevyo. Binadanu wote, wakiwemo wasanii, wanatikiwa kusali kwa imani zao ili maisha yaendelee bila kusikiliza mbiu kutoka kwa watu wengine.CREDIT: GPL

UKATILI WA KUTISHA: MTOTO AFUNGWA MINYORORO KWA MGANGA WA KIENYEJI MIEZI MNNE...!!! SOMA KISA HAPA



MATUKIO ya ukatili dhidi ya watoto, bado yameendelea kushika kasi kwenye maeneo mbalimbali nchini ambapo katika Mkoa wa Simiyu, mtoto mwenye umri wa miaka 17 (jina tunalihifadhi), mkazi wa
Bariadi Mjini na mwanafunzi wa Shule ya Msingi Bariadi, amejikuta akifungwa minyororo mikononi na miguuni kwa miezi minne nyumbani kwa mganga wa kienyeji.

Mganga huyo amefahamika kwa jina la Mdeli Msanja ambaye aliamua kufanya ukatili huo baada ya wazazi wa mtoto huyo ambaye anamatatizo ya akili, kushindwa kumlipa pesa za matibabu.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Charles Mkumbo, alisema wazazi wa mtoto huyo walikubaliana na mganga huyo kumlipa sh. 260,000 kama mtoto wao atapatiwa matibabu na kupona.
“Pamoja na wazazi kukubaliana na mganga husika, hali ya mtoto haikuweza kubadilika wala kupata unafuu hivyo waliomba kumchukua mtoto wao kitendo ambacho kilipingwa na mganga kwa madai ya kutolipwa pesa zake ambazo walikubaliana,” alisema.

Alisema mganga huyo aliamua kumchukua mtoto huyo na kumfungia chumbani kwake kwa minyororo miguuni na mikononi kwa kipindi cha miezi minne akidai pesa zake na kuwapa wakati mgumu wazazi wake.

Kutokana na msimamo wa mganga huyo, mama mzazi wa mtoto huyo Malita James (46), alilazimika kwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Bariadi kuhusu mateso anayoyapata mwanaye kwa mganga.

“Polisi walishirikiana na Dawati la Jinsia kufanya uchunguzi wa tukio hili na walipofika kwa mganga, walimkuta akiwa amemfunga minyororo miguuni na mikononi,” alisema Kamanda Mkumbo.

Aliongeza kuwa, polisi walimkamata mganga huyo ambaye hakuwa na kibali cha kutoa tiba za asili, pia alikamatwa na nyara za Serikali ambazo ni pembe moja ya swala na mikia miwili ya nyumbu ambapo uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Aua shemeji yake kwa kumkata Mapanga huko Tarime.....Kisa ni Mbwa kula Mayai



NA SAMSON CHACHA, Gazeti la Uhuru, TARIME
MKAZI wa Kijiji cha Nyamwaga wilayani hapa mkoani Mara, Mbusiro Muyuyi, ameuawa kwa kukatwakatwa kwa panga kichwani na shemeji yake.

 
Mauaji hayo yaliyowashitua wengi wilayani hapa, chanzo chake ni mbwa wa mtuhumiwa, Mwita Muyuyi (17), kula mayai ya kuku wa marehemu.
 
Habari za kuaminika zimesema kuwa, Mbusiro (45), alimtuhumu shemeji yake kuwa, mbwa wake amekula mayai ya kuku, hali iliyoibua mzozo mkubwa baina yao.
 
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Tarime/ Rorya, Justus Kamugisha, alisema tukio hilo lilitokea juzi asubuhi katika kitongoji cha Ntarachagine.
 
Alisema wakati mzozo huo ukiendelea, Muyuyi alikuwa ameshika panga na ghafla alianza kumshambulia mke wa kaka yake sehemu mbalimbali za mwili wake.
 
Kamanda Kamugisha alisema baada ya tukio hilo, Mbusiro alikimbizwa hospitali kwa matibabu, lakini akiwa kwenye zahanati ya Nyarero, hali yake ilizidi kuwa mbaya na kufariki dunia.
 
Tayari mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi kabla ya kupandishwa kizimbani kujibu tuhuma za mauaji zinazomkabili.
 
Kamanda Kamugisha alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kuacha tabia za kujichukulia sheria mkononi na badala yake wafikishe migogoro kwenye vyombo vya ulinzi na usalama kwa hatua zaidi.


Mlevi afariki dunia baada ya kunywa VIROBA vingi bila kula chakula




Michael  Silanda ( 26 )   mkazi  wa  kijiji  cha  Ibindi, tarafa  ya  Nsimbo  wilaya  ya  Mlele  mkoani  Katavi  amefariki  dunia  baada  ya  kunywa  pombe ( Viroba )  aina  ya  Zed  kupita  kiasi  bila  kula  chakula....

Kamanda  wa  polisi  mkoani  Katavi,Kamishna  Msaidizi  Mwandamizi,Dhahiri Kidavashari  amesema  tukio  hilo  limetokea  wiki  iliyopita  majira  ya  saa  sita  usiku  kijijini  hapo.....

Alisema  siku  ya  tukio  marehemu  baada  ya  kuamka  asubuhi  nyumbani kwake  hapo  majira  ya  saa  tano  asubuhi  alielekea  kwenye  baa  ambayo  ilikuwa  ikiuza  vinywaji  vya  aina  mbalimbali  zikiwemo  pombe  kali....

Alifafanua  kuwa,baada  ya  kufika  kwenye  baa  hiyo  aliwakuta baadhi  ya  wanakijiji  wenzake  wakiwa  wanakunywa  pombe  za  aina  mbalimbali  hali  ambayo  ilimfanya  marehemu  aweze  kujumuika  nao  kwa  kuagiza  pombe  aina  ya  Zed...

Alisema  Michael  aliendelea  kunywa  viroba  kuanzia  muda  huo  kwenye  baa  hiyo  bila  kula  kitu  chochote  hadi  majira  ya  saa  sita  usiku  alipoamua  kurudi  nyumbani  kwake  huku  akiwa  amelewa  pombe  kupita  kiasi....

Baada  ya  kufika nyumbani  kwake  aliingia  ndani  ya  nyumba  yake  na  kulala  bila  kula  chakula  cha  aina  yoyote  na siku  iliyofuata  majira  ya  saa  mbili  asubuhi  ndipo  walipomkuta  Michael  akiwa  amefariki  huku  akiwa  amelala  kitandani  kwake,.....

Kamanda  Kidavashari  alisema  uchunguzi  wa  awali  uliofanywa  kuhusiana  na  tukio  hilo  umebaini  kuwa  kifo  hicho  kimesababishwa  na  marehemu  kunywa  pombe  nyingi  kupita  kiasi  bila  kula  chakula....

Majambazi yaua polisi wawili mkoani Tabora....Yalivamia nyumbani kwa mfanyabiashara, Polisi walipofika walifyatuliwa risasi na kufariki papo hapo


Jeshi la Polisi limepata pigo kutokana na askari wake wawili kuuawa kwa kupigwa risasi na majambazi... Askari wawili wa jeshi hilo waliuawa kwa kupigwa risasi na majambazi katika Tarafa ya Usoke wilayani Urambo mkoani Tabora. 

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Suzan Kaganda, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 2:30 usiku katika kijiji cha Usoke. Kamanda Kaganda aliwataja askari waliouawa kuwa ni PC Shaban namba G 3388 ambaye alikufa papo hapo baada ya kupigwa risasi na majambazi hao na PC Jumanne namba F.5179 aliyejuruhiwa tumboni na baadaye kufariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete wakati akipatiwa matibabu.

Kamanda Kaganda alisema majambazi watatu walivamia nyumbani kwa mfanyabiashara, Ibrahim Mohamed, mkazi wa Usoke kisha kupora fedha tasilimu Sh. milioni 1.2. Mbali ya kufanya uporaji huo, yalipora vocha za simu zenye thamani ya Sh. 120,000. Alisema baada ya askari hao kupata taarifa ya uharifu huo, walienda eneo la tukio kwa ajili kutoa msaada, lakini wakiwa mita chache kabla ya kufika katika eneo la tukio, walikutana na majambazi hao na kuanza kuwafyatulia risasi kwa kasi na kumuua PC Shaban. “Ndugu zangu waandishi wa habari hili ni pigo kubwa sana kwa Jeshi la Polisi, lakini naapa kuwasaka hadi kuwakama wakiwa hai au wafu, sasa tumechoka na uharifu huu,” alisema Kaganda.

Kamanda huyo alisema kabla ya tukio la mauaji ya askari hao, majambazi hao yalifyatua risasi hovyo hewani mfululizo kwa lengo la kuwatisha raia na kwamba maganda 25 ya risasi aina ya SMG na SAR yaliokotwa katika eneo la tukio. Kufuatia tukio hilo jeshi la Polisi mkoani Tabora linaendesha msako na tayari watu watano wametiwa mbaroni kuhusiana na tukio hilo.

Binti aliyepigwa na Chid Benz yuko Mahututi....Kwa siku anazimia mara 5, Mama Chid atimuliwa nyumbani


MREMBO Mwanaisha Kiboye, mkazi wa Ilala, Dar anayedaiwa kupigwa na mwanamuziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, hali imekuwa mbaya kwani yu mahututi.

Juzi Jumatatu, wakati staa huyo akipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar kwa kesi hiyo, Mwanaisha alikuwa akipumua kwa tabu kwenye chumba maalum katika Hospitali iitwayo Aviation iliyopo maeneo hayo ya Ilala.
 
MAMA MDOGO ANASEMAJE?
Kwa mujibu wa mama mdogo wa Mwanaisha aliyejitambulisha kwa jina moja la Aisha, hali ya mgonjwa imekuwa tete kwani kwa siku moja amekuwa akizimia zaidi ya mara tano.

AZIMIA MARA TANO
“Mwanangu hali yake ni mbaya anazimia zaidi ya mara tano kwa siku halafu watu wananiambia nitoe kesi mahakamani si nitaonekana chizi jamani?” alisema mama huyo huku akilengwalengwa na machozi.
 
Alisema hali ya mgonjwa imekuwa ikibadilika hasa suala la presha kupanda na kushuka huku mapigo ya moyo yakiwa chini hivyo kuwatia hofu ndugu, jamaa na marafiki.
 
KIPIMO CHA KICHWA
Aliongeza kuwa siku hiyo (Jumatatu) madaktari na wauguzi walikuwa katika harakati za kumpeleka kwenye kipimo kiitwacho CT Scanning kuangalia madhara yaliyompata kichwani na kusababisha hali kuzidi kuwa mbaya.

Mwanahabari wetu alifanikiwa kuingia wodini ambapo katika kipindi cha saa kadhaa Mwanaisha hakugeuka wala kuamka kutoka usingizini.
 
TURUDI KWENYE KESI
Juzi (Jumatatu) Chid alitakiwa kupandishwa kizimbani Mahakama ya Mwanzo, Wilaya ya Ilala, Dar kwa ajili ya kesi hiyo lakini hakutokea kortini badala yake alimtuma mdhamini wake amuombee udhuru kuwa alikuwa akiumwa.
 
CHEMBA KIDOGO
Karani wa mahakama hiyo, Nusura Seleman alipoita kesi hiyo, mdhamini huyo na ndugu wa Chid Benz na ndugu wa Mwanaisha, walijongea kwenye ‘chemba kidogo’ mbele ya Hakimu Leonia Muta.
 
HAIWEZEKANI
Katika kesi hiyo ambayo mwanahabari wetu aliifuatilia hatua kwa hatua, hakimu Muta aliwaita wenye kesi hiyo lakini wote hawakuwepo ndipo hakimu huyo akasema hawezi kuendelea na kesi hiyo bila wenye kesi wote kuwepo. Shauri hilo liliahirishwa hadi Mei 5, mwaka huu.
 
MAMA CHID ATOLEWA NDUKI
Akizungumza nje ya mahakama hiyo, kaka wa Mwanaisha aliyejitambulisha kwa jina la Swedy alisema: 
 
“Hali ya ndugu yetu ni mbaya namna ile halafu wanatuambia tukayamalize nyumbani, hilo si jambo la kushangaza jamani?
Mama yake Chid Benz alikuja nyumbani kutaka kumuona mgonjwa tukamtoa nduki. 
 
“Hali ya ndugu yetu ni mbaya hivyo asijekudhurika na jambo lolote akiwa nyumbani kwetu ikaonekana tumemfanyia kusudi.
 
CHID NAYE ATOLEWA BARU
“Hata Chid Benz mwenyewe naye juzi (Jumamosi iliyopita) alikuja na kutupigia magoti naye tukamtoa baru, asitulee zake kwanza hii siyo mara ya kwanza kumpiga dada yangu kuna kipindi alimpiga kesi ilikuwa Kituo cha Polisi cha Kilwa Road.”

Source: Risasi  Mchanganyiko/ GPL