Showing posts with label Vituko. Show all posts
Showing posts with label Vituko. Show all posts

Sakata la Mwanamke aliyehukumiwa KUNYONGWA na KUCHAPWA VIBOKO 100 kwa kubadili dini na kuolewa na mume Mkristo




Mahakama nchini Sudan imemuhukumu kifo mwanamke mmoja anayedaiwa kubadili dini yake na kuolewa na mwanaume mkristo. Daktari Mariam Yahya Ibrahim Ishag ambae baba yake ni muisilamu alishitakiwa kwa kosa la kuasi dini pamoja na kufanya zinaa kwa kuolewa na mwanamume mkristo kitu ambacho dini ya kiisilamu imeharamisha kwa Wanawake.
BBC wamesema Mariam mwenye umri wa miaka 28 pia ni mjamzito na ataadhabiwa kwa kuchapwa mijeledi 100 kwa kosa la zinaa. 
 
Unaambiwa Mariam alilelewa na mama yake mzazi ambae ni Mkristo lakini maafisa wa Sudan wanasema yeye bado ni Muislamu kwa sababu ndio dini ya baba.
 
Alipewa siku tatu baada ya kuhukumiwa aweze kurejea katika dini ya kiisilamu lakini akakataa na ndio maana adhabu ikabaki palepale kwa kuwa Wanawake Waislamu hawaruhusiwi kuolewa na Wanaume Wakristo ingawa Wanaume Waisilamu wanaruhusiwa kuwaoa wanawake wakristo.
 
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International linasema kuwa Ishag alilelewa kama Mkristo muorthodoxi kwa sababu baba yake hakuwepo naye maishani mwake.
 
Kesi ya Ibrahim ni ya kwanza ya aina yake kusikika nchini Sudan kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters na Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wamelaani uamuzi huo wa Mahakama na kuitaka serikali ya Sudan kuheshimu haki na uhuru wa watu kuabudu.
 
Maafisa wa balozi za mataifa ya magharibi pia wamekemea vikali kesi hiyo na kuelezea asiwasi wao na kuwataka maafisa wa sheria nchini humo kuangalia kesi hiyo upya na kuhakikisha kuwa Mariam anatendewa haki.
 
Waziri wa mawasiliano amesema kuwa sio Sudan peke yake ambako sheria za kiisilamu zinafuatwa na ambako sio sawa kwa mtu kubadili dini yake, hali hiyo pia ipo nchini Saudi Arabia na katika nchi nyngine zinazofata sheria za kiisilamu.
 
Serikali ya Rais Omar al-Bashir inakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi na kisiasa hasa baada ya kujitenga na Sudan Kusini ambako mafuta yake yalikuwa yanatoka mwaka 2011.


Girlfriend wa Cristiano Ronaldo ashambuliwa kwa kupost picha akiwa Uchi na bango lililoandikwa #bringbackourgirls



Tangu wasichana 276 wa Nigeria walipotekwa nyara na kundi la Boko Haram, watu mbalimbali maarufu duniani wamepost picha kwenye mitandao ya kijamii wakiwa na mabango yaliyoandikwa ‘Bring back Our Girls’, ikimaanisha wanajiunga na kampeni ya raia wa Nigeria.
 
Mwana mitindo Irina Shayk ambaye ni mpenzi wa mchezaji wa mpira wa miguu Christian Ronaldo yeye amepost picha kwenye twitter na Instagram akiwa amepoz mtupu huku akiwa ameshikilia bango linaloonesha amejiunga na kampeni hiyo, na bango hilo ndilo lililofunika kifua chake.
Hata hivyo kitendo chake hakikuungwa mkono na baadhi ya followers wake ambao walionesha moja kwa moja hisia kwa kumshambulia kuwa ameenda kinyume na maadili.
 
“Pretty tasteless and disrespectful. No class. This is exactly the justification terrorists are probably using to prevent women from receiving 'western education.” Aliandika mtu mmoja.
 
Mwingine aliona kama amefanya dharau kwa kuwa tatizo hilo sio la nchi kubwa kama Marekani na kuhoji kama angediriki kufanya hivyo siku ya tukio kubwa la shambulizi la kigaidi la September 11 nchini Marekani.
 
“Would you stand there n*ked wishing sorrow on the 9/11 victims? Would you do it for the tsunami? This is a tasteless attitude to 200 missing girls.”
Hata hivyo sio wote waliomshambulia, wengine walimsapoti na kueleza kuwa alikuwa na nia njema ya kuvuta umakini zaidi wa watu kuifuatilia kampeni hiyo kwenye mitandao ya kijamii.

Aunty Lulu Avua Nguo Hadharani Ukweni baada ya pombe kupanda kichwani



Msichana wa mjini asiyeishiwa na matukio Bongo, Lulu Mathias Semagongo ‘Aunty Lulu’, kwa mara nyingine amefanya kituko cha aina yake baada ya kuzua timbwili kisha kusaula nguo zote hadharani bila kujali yupo ukweni. 

Aunty Lulu ana uhusiano wa kimapenzi na kijana anayejulikana kwa jina moja la Amani.
 
Habari zisizokuwa na chembe ya ‘dauti’ zilidai kuwa hivi karibuni, Aunty Lulu na Amani walikuwa wakipata kinywaji kwenye baa moja iliyopo jirani na nyumbani kwa wakwe zake maeneo ya Majohe, Dar ndipo ukaibuka ugomvi kati yao na kusababisha pachimbike.
 
Chanzo hicho kutoka ndani ya familia ya wakwe zake Aunty Lulu, kilidai kwamba mwanadada huyo alizua timbwili alipokuwa akipigana na Amani.
 
Ilisemekana kwamba katika hali ya kushangaza, Aunty Lulu alikwenda mbali zaidi alipovua nguo hadharani na kubaki mtupu hivyo kuwalazimu watu wenye busara kumshika na kumsihi avae nguo kisha walimpeleka nyumbani wanakoishi maeneo hayohayo ya jirani na wakwe zake.
 
“Yaani Aunty Lulu anamng’ang’ania kwa nguvu ndugu yetu Amani wakati familia nzima haimtaki kwa sababu ya tabia zake hizo, hii ni mara ya pili kuvua nguo hadharani.
 
“Ukweli hata baba mkwe hataki kumsikia, ameshampigia sana kelele mwanaye aachane naye,” kilisema chanzo hicho.
 
Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, Ijumaa Wikienda liliwasaka wahusika kwa kuanzia na Aunty Lulu ambapo alikiri kwamba ni kweli ugomvi ulitokea lakini hakuvua nguo.
 
“Ni kweli tuligombana hapo baa lakini sikuvua nguo na kuhusu kila siku kupigana, jamani hayo ndiyo mapenzi. Wanaosema mimi ndiye namng’ang’ania Amani siyo kweli kwani wote tunapendana,” alisema Aunty Lulu.
 
Kwa upande wake Amani alifunguka: “Habari hizo siyo za kweli kabisa ndugu mwandishi.”

>>Ijumaa Wikienda


Kutovaa nguo za ndani kwamuumbua Naomi Campbell....!




Mwanamitindo  wa  kimataifa  wa  Marekani, Naomi  Campbell  mwishoni  mwa  wiki  jana  alikumbwa  na  tukio  la  aibu  baada  ya tatizo  lake  la  kusahau  kuvaa  chupi  kumsababishia  tatizo  kubwa  wakati  akishuka  kwenye  gari  lake  na  kukumbana  na  camera  za  wapiga  picha  za  kidaku....!

Kutokana  na  kutovaa  nguo  hiyo  ya  ndani, Naomi  wakati  akishuka  kwenye  gari  lake  hilo    alijikuta  nguo  zake  zikifunuka  na  kuacha  wazi  kabisa  nyeti  zake, na  wapiga  picha  hao  wakafanikiwa  kumpiga  picha  kadhaa  ambazo  zimesambaa  mtandaoni....
Wengi  wa  walioziona  picha  hizo  wameibua  mjadala  mtandaoni  kwa  kumtuhumu  mwanamitindo  huyo  kwa  kutojitunza  kwenye  nyeti  zake.