Showing posts with label Afya. Show all posts
Showing posts with label Afya. Show all posts

Kutana na Dawa ya Habbat Soda yenye uwezo wa kutibu Magonjwa 75 kama vile Kichoho, Vidonda vya tumbo, Kisukari, Kujikojolea, Utasa na mengine Mengi


Habbat Soda  au  Nigella  Sativa kwa  jina  la  kisayansi   ni  dawa  ya  asili yenye  uwezo  wa kutibu na  kuponyesha  kabisa   magonjwa  na  matatizo  mbalimbali  ya  kiafya  yanayo mkabili  mwanadamu.

Dawa  hii imeanza  kutumika  tangu  enzi  na enzi. Dawa  hii  ilikuwako  hata kabla  ya  enzi za  Pontyo  wa  Pilato  ( Pontius  Pilates ) .Kutokana  na  ufanisi  wake  katika  kutibu na  kuponyesha  kabisa  matatizo  mbalimbali  ya  kiafya  yanayo wakabili  wanadamu, wataalamu  wa kale  wa   tiba  asilia  katika  nchi za   Misri, Israel na  Arabuni  walielezea  Habbat  Soda  kama  Dawa  inayotibu  magonjwa  yote  kasoro  umauti pekee.
 
Habbat  Soda  inaweza  kuwa  katika  mfumo  wa  unga unga, mbegumbegu  au mafuta. Iaweza  kutibu  magonjwa  na  matatizo  mbalimbali  ya  kiafya  kama  ifuatavyo.
 
Kwa faida ya Afya kwa ujumla:
Kunywa kijiko kimoja cha mafuta ya Habbat-Sawdaa asubuhi na usiku, au kunywa japo asubuhi kabla ya kifungua kinywa, unaweza kunywa kijiko kimoja cha mafuta peke yake au ukachanganya na kijiko kimoja cha asali safi.
 
Uvimbe  Wa  Tumbo  (  Fibroid  )
Chukuwa unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja na kijiko cha urkusus (licorice) kasha  changanya na juisi ya pea iliotengenezwa pamoja na kokwa zake; halafu tumia  kunywa  mara  tatu  kwa  siku  asubuhi  mchana  na  jioni  kwa  muda  wa  siku  ishirini  na  moja. Tatizo  la uvimbe  wa  tumbo  litaondoka.
 
Nguvu Za  Kiume
Chukua  unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja changanya (piga ) ndani ya mayai saba ya kienyeji, kisha  koroga  halafu  tumia  mchanganyiko wako  kunywa. Utafanya  hivyo  mara  moja  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku thelathini. Basi hata kama una miaka 70 utapata nguvu za barobaro!
 
Vidonda   Vya   Tumbo
Chukua maziwa fresh na uya chemshe kisha yaipue yakipoa tia viini vya mayai ya kuku wa kienyeji mayai manne.Tia katika maziwahayo asali mbichi  ujazo sawa.Kijiko cha unga wa majani ya mkalatusi. Kijiko cha unga wa habat soda. 

Tumia dawa  hii mara 3 kwa siku  kwa muda wa siku thelathini.Tatizo  lako la   vidonda  vya  tumbo  litaondoka.
 
Kwa faida ya Afya kwa ujumla:
Kunywa kijiko kimoja cha mafuta ya Habbat-Sawdaa asubuhi na usiku, au kunywa japo asubuhi kabla ya kifungua kinywa, unaweza kunywa kijiko kimoja cha mafuta peke yake au ukachanganya na kijiko kimoja cha asali safi.
 
Vipele (chunusi) Na Ngozi:
Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ½ (nusu) kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ½ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple). Paka katika sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.
 
Upara (Alopeshia):
Sugua mafuta ya Habbat-Sawdaa katika mabaka yanayokusumuba.
 
Pumu:
Tia ½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.
 
Kuumwa kwa Mgongo (Sehemu ya Chini):
Changanya asali pamoja na ¼ (robo) kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.
 
Mwiba Wa Nyuki Na Nyigu:
Tia ½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa iliyochemshwa katika maji ya yaliyochemshwa kisha unywe moto.
 
Kibofu cha Mkojo/Figo:
Kunywa maji ya moto yaliyochanganywa na½ (nusu) kijiko cha Habbat-Sawdaa pamoja na asali kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Changanya vikombe viwili vya Habbat-Sawdaa iliyosagwa na ½ (nusu) kikombe cha asali safi.

Kunywa kijiko kimoja cha mchanganyiko pamoja na kikombe kimoja cha maji ya moto kila asubuhi kabla ya kufungua kinywa. Mchanganyiko unaweza kukaa kwa siku 15 na ni lazima uwekwe katika hali ya ubaridi.
 
Jiwe La Figo:
Kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyochanganwa pamoja na gilasi (bilauri) moja ya asali, vitunguu saumu vitatu vilivyosagwa na karafuu. Changanya vitunguu saumu pamoja na asali na Habbat-Sawdaa. Kunywa kijiko kimoja kabla ya kula chakula na kwa pendekezo kula limau (bila ya kumenywa). Rudia haya kwa wiki moja jiwe litaondoka.
 
Maathiriko Ya Figo:
Changanya baadhi ya Habbat-Sawdaa pamoja na mafuta ya alizeti. Chukua mchanganyiko na weka katika sehemu ambapo figo limeathirika. Kunywa kijiko cha Habbat-Sawdaa  asubuhi. Rudia haya kwa muda wa wiki moja maathiriko yatatibika.
 
Mafua:
Chukua mbegu za Habbat-Sawdaa 21, ziweke katika kitambaa na roweka usiku. Tumia kama matone kwenye pua siku ya pili nusa poda ya Habbat-Sawdaa iliyomo katika kitambaa.
 
Kikohozi:
Tumia matone matatu au manne ya mafuta ya Habbat-Sawdaa kwenye kahawa au chai.
 
Bawasiri:
Kula unga wa Habbat-Sawdaa pamoja na maji.
 
Shinikizo la damu (high blood pressure):
Changanya kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, kijiko kimoja cha asali safi na kitunguu kiasi kidogo. Chukua mchanganyo kabla ya kufungua kinywa kwa siku ishirini.
 
Uwasho Na Maumivu Ya Jino Na Ufizi:
Chemsha Habbat-Sawdaa katika siki na itumie kwa kusukutulia meno na ufizi. Na jikinge kutumia dawa za msuwaki za kibiashara na tumia dawa za msuwaki ambazo zinatengenezwa kutoka kwenye nyuzi za mboga za mti wa siwak ambao kwa karne ulikuwa unatumiwa na Wahindi, Waafrika na Waarabu, ni msuwaki wa kiasili.
 
Kumbukumbu (memory):
Kunywa kijiko kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa na changanya na asali mara mbili kwa siku.
 
Utaratibu  Wa Ulinzi Wa Mwili:
Kula kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa na asali mchana na usiku Kutoweza kuzuia haja ndogo (mkojo): Kunywa kijiko kimoja cha Habbat-Sawdaa pamoja na asali, kisha kunywa maji ya vugu vugu.
 
Jaundice: ( Homa  Ya  Manjano )
Tumia Habbat-Sawdaa pamoja na maziwa.
 
Maumivu Sugu ya kichwa (Maumivu ya kichwa ya upande mmoja, maumivu ya kichwa):
Kaanga Habbat-Sawdaa na iweke katika kitambaa cha pamba, funga au weka tu kitambaa katika kikomo (kipaji cha uso). Roweka Habbat-Sawdaa ndani ya siki wakati wa usiku, siku ya pili ivuruge kufanya unga. Ingiza katika pua halafu vuta pumzi.
 
Ngozi kavu:
Changanya asali pamoja na robo kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.
 
Upepo:
Changanya asali pamoja na robo kijiko cha Habbat-Sawdaa na iwe kitu cha kwanza kunywa wakati wa asubuhi kabla ya kufungua kinywa.
 
Minyoo:
Kunywa Habbat-Sawdaa pamoja na siki kuondoa minyoo.
 
Kunyonyoka Nywele
Ataukanda unga wa Habbat-Sawdaa katika juisi ya chirichiri pamoja na kijiko cha siki nyepesi na kikombe cha mafuta ya zeituni, halafu asugue kichwani kwa mafuta hayo kila siku jioni pamoja na kukiosha kichwa kwa maji na sabuni kabla ya kupaka.
 
Maumivu ya Kichwa
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa , karafuu iliosagwa nusu ya kiwango cha Habbat-Sawdaa  na anisuni (anise), halafu achanganye pamoja. Achukue kiasi cha kijiko kimoja (cha chai), wakati wa kuumwa na kichwa, na ale na maziwa lala (mala), pamoja na kupasugua mahala paumapo kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa .
 
Ukosefu Wa Usingizi
Atachukua kijiko cha Habbat-Sawdaa , achanganye na gilasi ya maziwa moto  yaliochanganywa na asali, baada ya kupoa kiasi atakunywa.
 
Chawa Na Mayai Yake
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa uliosagwa vizuri aukande kwenye siki mpaka uwe kama marhamu, halafu ajipake kichwani – baada ya kunyoa nywele au kuisugua marhamu kwenye mashina ya nywele, halafu aketi katika mwanga wa jua kitambo cha robo-saa. Na hataosha kichwa ela baada ya masaa matano. Atafanya hivyo kila siku kwa muda wa wiki moja.
 
Kisunzi Na Maumivu Ya Sikio
Tone moja la mafuta ya Habbat-Sawdaa ndani ya sikio husafisha sikio, pamoja na kuyanywa na kusugua sehemu za panda na nyuma ya kichwa, humaliza kisunzi.
 
Upaa Na Mabaka
Utachukua kijiko cha unga wa Habbat-Sawdaa, siki kiasi cha kikombe kimoja na juisi ya kitunguu saumu kiasi cha kijiko kidogo, vyote hivyo utavichanganya na vitakua namna ya   marhamu, utajipaka baada ya kunyoa sehemu  ya nywele na kuchanja kidogo – kisha utafunga bendeji, utaiacha mpaka asubuhi, baadae utajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa,utaendelea hivyo kwa muda wa wiki moja.
 
Malengelenge ya Neva katika Ngozi
Atajipaka – sehemu ya malengelenge – mafuta ya Habbat-Sawdaa mara tatu kila siku mpaka iondoke .
 
Maradhi Ya Wanawake Na Uzazi
Dawa kubwa inayosahilisha kuzaa ni Habbat-Sawdaa iliochemshwa ikachanganywa na asali na kiziduo cha babunaji (chamomile). Habat sawdaa  ni kama burashi katika uke wa mwanamke yenye faida kubwa kwao pamoja na kutumua mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kila kinywaji cha moto kwa maradhi yote ya wanawake.
 
Meno Na Maumivu Ya Mafido na Koo
Kiziduo cha Habbat-Sawdaa na kutumia kwa kusukutua kwa kugogomoa, husaidia mno maradhi yote ya mdomo na koo, vivyo hivyo pamoja na kubugia kijiko cha Habbat-Sawdaa na kumeza kwa maji yenye vuguvugu kila siku na kujipaka mafuta yake sehemu ya koo kwa nje na kuusugua ufizi kwa ndani.

Maradhi Ya Tezi
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa na aukande kwa asali na mkate wa nyuki kila siku, kwa kipindi cha mwezi mmoja.
 
Chunusi (Acne)
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa aukande katika mafuta ya ufuta (simsimu) pamoja na kijiko cha unga wa ngano. Vyote hivyo atajipaka usoni kuanzia jioni hadi asubuhi, halafu ataosha kwa maji yenye vuguvugu kwa sabuni. Ataendelea kufanya hivyo kwa muda wa wiki moja. Na awe akinywa mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kinywaji chochote cha moto.
 
Maradhi Yote ya Ngozi
Atachukua mafuta ya Habbat-Sawdaa, mafuta ya waridi (marashi jabali) na unga wa ngano asili, vyote hivyo  kwa viwango sawa, ule unga wa ngano uwe zaidi kuliko mafuta, halafu aukande vizuri. Kabla ya kujipaka, apanguse sehemu yenye ungonjwa kwa kitambaa kilichoroweshwa siki nyepesi, halafu aketi kwenye jua, baadae ajipake dawa hio kila siku. Lakini ajizuie na kila chenye kuchochea hisia kama vile, samaki, mayai, maembe na mfano wake.
 
Sugu (Chunjua) (Wart)
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa aukande katika siki nzito na asugue kwa kitambaa cha sufi au katani mahala pa sugu asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja.
 
Kuung`arisha Uso Na Kuurembesha
Ataukanda unga wa Habbat-Sawdaa katika mafuta ya zeituni, na atajipaka usoni halafu apigwe na mwanga wa jua kidogo. Tiba hiyo ataifanya wakati wowote katika mchana na siku yoyote.
 
Kuunganisha Mvunjiko Haraka
Supu ya adesi (dengu), kitunguu maji pamoja na yai la kuchemsha na kijiko kikubwa cha unga wa Habbat-Sawdaa , utachanganya na supu hiyo japo siku baada ya siku; halafu anywe. Na atasugua sehemu zilizo karibu na mvunjiko kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa, na baada ya kufungua bendeji atajisugua kwa mafuta ya Habbat-Sawdaa yenye vuguvugu; kila siku.
 
Mvilio  Wa Damu (Contusion)
Atachemsha vizuri konde moja la Habbat-Sawdaa katika chombo cha maji, kisha atakiingiza kiungo kilichovilia damu ndani ya maji hayo- yenye vuguvugu- kwa muda wa robo-saa au zaidi pamoja na kukitaharakisha kiungo hicho. Baada ya hapo atajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa bila ya kufunga kitu. Lakini hatakiwi kukipa uzito kiungo hicho au kukitaabisha. Tiba hiyo ataifanya kila siku kabla ya kulala.
 
Baridi Yabisi (Rheumatism)
Atachemsha mafuta ya Habbat-Sawdaa na atasugua kwayo ile sehemu yenye ugonjwa, atasugua kwa nguvu kama kwamba yuwasugua mfupa wala sio ngozi! Na atayanywa baada ya kuyachemsha vyema na kuyachanganya na asali kidogo. Ataendelea na tiba hiyo huku akiwa ni mwenye imani na yakini kuwa Allah Atamponya.
 
(Ki) Sukari (Diabetes)
Utachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kikombe kimoja, manemane (myrrh) iliosagwa kiasi cha kijiko kikubwa, habbarrashad nusu kikombe, komamanga iliosagwa kiasi cha kikombe kimoja, mzizi wa kabichi uliosagwa baada ya kukaushwa kiasi cha kikombe kimoja na kijiko kidogo cha mvuje. Vyote hivyo atavichanganya na atakula kabla ya kula chakula kiasi cha kijiko kimoja, atakula na maziwa lala ili iwe rahisi kumeza.
 
Shinikizo la Damu (High Blood)
Kila unywapo kinywaji cha moto, tia matone machache ya mafuta ya Habbat-Sawdaa. Pia ujipake mafuta hayo mwili wote, japo wiki mara moja.
 
Uvimbe Wa Figo(Nephritis)
Atatengeneza kibandiko (cha kitambaa) kutokana na unga wa Habbat-Sawdaa uliokandwa katika mafuta ya zeituni, atabandika sehemu yenye maumivu ya figo pamoja na kubugia funda la kijiko cha Habbat-Sawdaa kila siku kabla ya kula chakula kwa muda wa wiki moja tu; uvimbe utakwisha insha
 
Kuvunjavunja Vijiwe Vya Tumboni
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kikombe kimoja kisha aukande katika kikombe cha asali, na atasaga kitungu u saumu punje tatu; atakua akichukua nusu yake akila kabla ya kula chakula kila siku. Pia itakua bora lau atakula limau kila baada ya kula dawa; kwani husafisha kabisa.
 
Kukojoa Kwa Maumivu (Dysuria)
Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa juu ya kinena kabla ya kulala pamoja na kunywa kikombe cha mafuta hayo yaliochemshwa na kutiwa asali; kila siku kabla ya kulala.
 
Kukojoa Bila Kukusudia ( Kujikojolea/Bed wetting )
Atachukua Habbat-Sawdaa na maganda ya mayai yaliosafishwa na yakaokwa na kusagwa halafu yakachanganywa na Habbat-Sawdaa kisha yakaokwa na kusagwa halafu yakachanganywa na Habbat-Sawdaa kisha aingize kwenye maziwa; hatimae anywe kiasi cha kikombe kimoja kila siku na wakati wowote.
 
Jongo (Edema)
Ataweka kibandiko (cha kitambaa) cha unga wa Habbat-Sawdaa uliokandwa katika siki juu ya kitovu, kwanza ataweka kitambaa. Pia atakula Habbat-Sawdaa kijiko kimoja asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja.
 
Kifuko Cha Nyongo Na Vijiwe Vyake
Atachukua Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja, manemane iliosagwa robo kijiko na asali kiasi cha kikombe kimoja; vyote hivyo atavichanganya viwe mraba (kama jamu); halafu awe akila kila asubuhi na jioni.
 
Wengu
Ataweka kibandiko (kilichopashwa moto) cha Habbat-Sawdaa iliokandwa katika mafuta ya zeti katika ubavu wa kushoto; jioni. Na wakati huo huo ata kunywa kikombe cha kiziduo cha uwatu kilichochanganywa asali na mafuta ya Habbat-Sawdaa kidogo, ataendalea na dawa hiyo kwa muda wa wiki mbili mfululizo.
 
Maradhi Yote ya Kifua na Baridi
Atachukua mafuta ya Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kikubwa atie kwenye maji halafu ayaweke juu ya moto mpaka ianze kufuka moshi, hapo aanze kuuvuta ule moshi puani huku akiwa amejifunika kichwa ili ule moshi usiende upande mwingine. Atafanya hivyo kila siku kabla ya kulala, pamoja na kunywa kiziduo cha zaatari kilichochanganywa na unga wa Habbat-Sawdaa; asubuhi na jioni.
 
Moyo na Mzungukoa wa Damu
Kuwa na imani katika maneno ya Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wa sallam) Kwa sababu jambo hili ni katika muktadha wa imani. Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wa sallam) alipotuambia kuwa Habbat-Sawdaa ni dawa ya kila ugonjwa, basi hakuna shaka hata chembe kuwa ni dawa ya maradhi yote yanayomfika mwanaaadamu. Mgonjwa wa moyo asikate tamaa kutokana na rehma ya Allah; ni juu yake akithirishe kutumia Habbat-Sawdaa kwa namna yoyote iwayo; iwe ni kwa kula nzima au kwa kunywa wakati wowote uwao.
 
Mchango (Msokoto Wa Tumbo) (Colic)
Atachemsha vyema anisuni, kamun na nana kwa vipimo sawa na atatia asali kidogo, halafu atie matone saba ya Habbat-Sawdaa ; atakunywa kinywaji hicho kikiwa na vuguvugu pamoja na kupaka mafuta ya Habbat-Sawdaa mahala panaposokota. Baada ya muda mchache maumivu yataondoka.
 
Kuhara
Atachukua juisi ya chirichiri iliochanganywa na unga wa Habbat-Sawdaa kijiko kikumbwa, atakunywa kiasi cha kikombe kimoja mara tatu kwa siku.
 
Uziwi
Atachemsha Habbat-Sawdaa pamoja na karafuu, na atakunywa bila ya kuongeza kitu; mara tatu kwa siku.
 
Gesi Na Maumivu
Atabugia unga laini wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja kabla ya kula chakula akifwatisha gilasi ya maji yenye vuguvugu iliotiwa asali ya muwa kiasi cha vijiko vitatu; atakariri kila siku kwa muda wa wiki moja
 
Asidi (Acidness)
Motone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa yaliotiwa kwenye maziwa ya moto na asali; humaliza asidi.
 
Maradhi Ya Macho
Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa sehemu za panda kandokando ya macho na kope, atafanya hivyo kabla ya kulala pamoja na kunywa matone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa katika kinywaji chochote cha moto au katika juisi ya karoti.
 
Amiba (Vijidudu) (Amebiasis)
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja pamoja na kijiko cha kitunguusaumu kilichosagwa, atachangana katika kikombe cha juisi ya nyanya iliotiwa chumvi kidogo; atakunywa kila siku kabla ya kula chakula kwa muda wa wiki mbili mfululizo.
 
Kichocho (Bilharziasis)
Atakula Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja asubuhi na jioni, yawezekana kuila Habbat-Sawdaa katika chakula kama vile mkate pamoja na kujipaka mafuta yake katika ubavu wa kulia. Ataendelea na dawa hio kwa muda wa miezi mitatu mfululizo. Baadae atapata nguvu na nishati.
 
Kutoa Wadudu Tumboni
Atakula sandwichi moto ya vitu hivi: kijiko kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa, punje tatu za vitunguu, kijiko kimoja cha mafuta ya zeti, pilipilimanga kidogo na punje kumi za boga (calabash), asubuhi atakunywa kinywaji cha shimari au mafuta ya mbono mara moja pekee.
 
Utasa
Atachukua unga wa Habbat-Sawdaa, unga wa uwatu na mbegu ya figili kwa vipimo sawa, atakula kijiko kimoja asubuhi na jioni ilihali imekorogwa katika nusu kikombe cha asali, baadae atafuatisha kunywa kikombe kikubwa cha maziwa ya ngamia; basi inshaAllaah itakuwa kheri.
 
Tezikibofu (Prostate gland)
Atajipaka mafuta ya Habbat-Sawdaa chini ya mgongo na atajipaka chini ya korodani (mapumbu) na kusugua kwa mzunguko pamoja na kula unga wa Habbat-Sawdaa kijiko kimoja, na robo kijiko kidogo cha manemane katika nusu gilasi ya asali iliotiwa katika maji yenye vuguvugu; kila siku na wakati wowote apendao.
 
Pumu (Asthma)
Atanusa moshi wa mafuta a Habbat-Sawdaa asubuhi na jioni. Pia atakula unga wake asubuhi na jioni kabla ya kula chakula kila siku na pia kujipaka mafuta yake kifuani na kooni kabla ya kulala kila siku.
 
Kidonda
Atayachanganya matone kumi ya mafuta ya Habbat-Sawdaa, katika kikombe cha asali na kijiko kimoja cha maganda ya komamanga yaliyokaushwa na kusagwa. Atakula kila siku kabla ya kula chakula; baadae atakunywa gilasi ya maziwa yasiyotiwa chochote.
 
Saratani (Cancer)
Atapaka mafuta ya Habbat-Sawdaa mara tatu kila siku na kula kijiko cha unga wake kila amalizapo kula katika kikombe cha juisi ya karoti. Ataendelea hivyo kwa muda wa miezi mitatu.
 
Udhaifu kwa Ujumla
Atachukua unga wa habat sosa kiasi cha kikombe kimoja, uwatu mfano wake na ambari ilioyeyushwa kiasi cha kijiko kidogo, vyote atavichanganya katika chombo chenye asali iwe kama jamu; halafu awe akila kama jamu kila siku na wakati wowote apendao lakini kwa mkate wa ngano asili.
 
Kuleta Hamu Ya Kula
Kabla ya kuanza kula, jipatie Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kidogo na uitafune kwa meno yako, na unywe maji ya kawaida yaliochanganywa na siki kidogo.
 
Kutibu Ulegevu Na Uvivu
Atakunywa- kabla ya kula – juisi ya machungwa iliochanganywa matone kumi ya mafuta ya Habbat-Sawdaa. Ataendelea hivyo kwa muda wa siku kumi.  Baada ya hapo ataona nishati na uchangamfu.
 
Nishati akilini Na Wepesi Wa Kuhifadhi
Atachemsha nanaa (mint leaf), aichanganye na asali na aingize matone saba ya mafuta ya Habbat-Sawdaa; anywe kinywaji hiki kikiwa na vuguvugu wakati wowote apendao. Basi ataionea namna fahamu itakavofanya kazi
 
UNASUBIRI  NINI? TUMIA  SASA  DAWA  YA  HABBAT  SODA  KUTIBU  TATIZO  LA  KIAFYA  LINALOKABILI.
 
KWA  MAHITAJI  YAKO  YA  DAWA  YA  HABBAT  SODA, WASILIANA  NA NEEMA  HERBALIST  KWA   SIMU  0766538384.
 
TUNAPATIKANA  JIJINI  DAR  ES  SALAAM  KATIKA  ENEO  LA  CHANGANYIKENI  KARIBU NA  CHUO  CHA  TAKWIMU.
 
KWA  WASIO  WEZA  KUFIKA  OFISINI  KWETU  WATAPELEWA DAWA  MAHALI  WALIPO. 

KWA  WATEJA  WALIOPO  NJE YA  DAR  ES SALAAM  WATATUMIWA  DAWA  KWA  NJIA  YA  MABASI. WATEJA  WALIOPO  ZANZIBAR WATATUMIWA  KWA  NJIA  YA   BOTI.

KWA WATEJA  WALIOPO  NJE  YA  NCHI, WATATUMIWA  DAWA  KWA  NJIA  YA POSTA  AU  DHL.

Ray C Foundation yamuokoa video model wa ‘Ice Cream’ ya Noorah aliyeathirika na dawa za kulevya




Miongoni mwa watu ambao tayari wameanza kusaidiwa na taasisi mpya ya Ray C foundation iliyoanzishwa na mwanamuziki Rehema Chalamila aka Ray C mwaka huu, kwaajili ya kuwasaidia watu walioathirika na dawa da kulevya ni pamoja na video model aliyecheza kwenye video ya Noorah ‘Ice Cream’.

Model huyo aitwaye Doreen, hivi karibuni aliripotiwa kuwa hali yake ni mbaya kutokana na kuathirika na dawa za kulevya alizotumia kwa muda mrefu.
 
Baada ya Ray C kupata taarifa zake aliamua kumtafuta ili amsaidie, na baada ya kufanikiwa kumpata hivi sasa tayari ameanza tiba ya methadone.
 
Ray C amepost picha akiwa na Doreen na kuandika:
“Mungu ni mwema sana!!tena sana!!nilipotangaza kuwa nimefungua taasis yangu ya kuelimisha jamii kuhusu athari za madawa ya kulevya, nilipata emails nyingi kuhusu kumsaidia Doreen video queen aliecheza kwenye video ya Noorah iitwayo ice cream!!nilijaribu kumtafuta baada ya kuona picha yake kwenye website ya vibe magazine!!roho iliniuma sana nikamwomba Mungu anisaidie nimpate!!
 
"Namshukuru Mungu Asubuhi ya juzi Nikiwa ofisini nikaona email kutoka kwa dada yake Doreen kichwa cha habari Kikiwa Msaada,nilipoisoma chozi lilinitoka nika reply Mara moja nilimuomba anitumie namba yake tuongee,nikampigia akaniambia doren Hali yake si Nzuri kutokana na drugs,moyoni nikawa Nafikiria Huyu dada angejua jinsi nilivyomtafuta mdogo wake !!!!! 
 
"Ikawa Kama bahati,tukaongea kwa kirefu sana na nikamwambia tukutane kitengo cha madawa Mwananyamala!nilipomuona Doren Kwa Mara ya kwanza nilifurahi kupita maelezo,ila nikawa na wasiwasi kuhusu utayari wake wa kuanza Tiba ya methadone isije ikawa amelazimishwa kuja akaniambia dada yangu Nimechoka Maisha ya utumwa nisaidie!!hicho ndo nilichotaka kusikia nikamwambia Kwa uwezo wa Mungu Shetani ameshindwa!!!!!!
 
"Am soooo happy Doren ameanza Tiba ya methadone!!!wapenzi wote wa bongo flava nawaomba tumwombee mdogo wetu aweze kusimama kwenye Tiba na ashinde majaribu ya Shetani na aishi kwa amani bila utumwa wa shetani.God We Trust!!!I love You my lil sister…..
 
"Nawahamasisha wengine huko Mliko mwenye ndugu,Jamaa au rafiki,njoo Katika taasis yetu uweze kusaidiwa!usikubali Maisha ya utumwa wa madawa ya kulevya,njoo tukusaidie…Ray C Foundation pamoja na Kitengo cha Methadone We love you guys,We can help you….”
 
Tazama video ya ‘Ice Cream’ aliyocheza Doreen miaka kadhaa iliyopita

Watanzania washauriwa kufuga na kula PANYA aina ya ndezi kwa kuwa huongeza vitamini adimu mwilini


Watanzania wameshauriwa kufuga na kula panya aina ya ndezi wakieleza kuwa nyama hiyo haina mafuta mengi, ikiwa pia na virutubisho muhimu na vilivyo adimu. 
 
Rai hiyo imetolewa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) katika Maonyesho ya Vyuo Vikuu nchini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Wataalamu hao walisema kuwa ili kukabiliana na uharibifu wa kuchoma moto misitu kwa ajili ya kuwatafuta wanyama hao, ni vyema wananchi wakaanza kuwafuga kwa kuwa nyama yao ina ladha nzuri na ni laini.
 
Mhadhiri Mwandamizi wa SUA, Idara ya Uzalishaji, Mirende Matiko alisema kuwa ingawa wanyama hao wanafugwa kwa wingi katika nchi za Afrika Magharibi, hapa nchini ufugaji wake unakabiliwa na changamoto nyingi.
 
“Wakulima wetu hapa tunawapa wafuge, siku chache baadaye ukienda utaambiwa walikufa, lakini ukiwauliza majirani wanakuwambia ‘jamaa aliwachinja’, ni sawa na kumpa mkulima mbegu halafu anakula,” alisema Matiko.
 
Akizungumzia namna nyama hiyo inavyoliwa, Matiko alisema: “Nyama yake ina viinilishe vingi, yanatupwa manyoya na miguu yake tu, vitu vingine vyote vinaliwa. Tena utumbo ndiyo mtamu sana, si unajua wanakula nyasi tu.”
 
Alisema wanyama hao wana faida nyingi kiuchumi ikiwamo kuongeza pato la kaya, kuchangia uwindaji endelevu, kutunza bioanuwai pia nyama yao ni gharama nafuu, ikilinganishwa na nyingine.
 
“Mtu akitaka kufuga wanyama hao anatakiwa kuwa na banda madhubuti lenye ubora, chakula na maji safi yawepo bandani muda wote na upandishaji ufanyike katika muda mwafaka,” alisema.
 
Mhadhiri huyo alitoa hadhari kwa wafugaji akiwataka kuwakamata wanyama hao kwa umakini kutumia chandarua, kuepuka kusababisha majeraha.
 
Ndezi ni jamii ya nungunungu na pimbi, wakiwa wa aina mbili, ambapo wadogo huwa na uzito wa kati ya kilo nne hadi sita na wakubwa hufikia hadi kilo tisa. Wanyama hao hupendelea kuishi kwenye maeneo yanayolimwa mashamba ya miwa, ulezi na mpunga.
 
Hata hivyo, Dk Loth Mulungu alisema kuwa wawindaji wa ndezi porini husababisha madhara makubwa ikiwamo uchomaji wa misitu, uharibifu wa bioanuwai, kukanyaga mazao mashambani na upotevu wa muda.
 
Mmoja wa watazamaji waliotembelea Banda la SUA, Elizabeth Maro alisema kuwa ingawa kwa muda mrefu amesikia watu wakila mnyama huyo. Binafsi hawezi kula nyama yake kwa kuwa anaamini hana tofauti na panya wengine.
 
“Siwezi kumla kwa namna yoyote, huyu ni panya tu ndiyo maana hata jina lake kwa Kiingereza anaitwa ‘canerat’, maana yake panya mla miwa,” alisema.

Ipyana Mwambungu alisema mnyama huyo ameadimika katika baadhi ya mikoa kutokana na watu wengi kuipenda nyama yake.
 
“Kuna baadhi ya maeneo kule Kilimanjaro huwezi kuwaona tena ndezi, wakati zamani walikuwa wengi sana,” alisema.

Credit: Mwananchi

HATARII!!! MWANAUME SOMA HIZI DAWA ZA MENO ZINAWEZA KUHARIBU NA KUPUNGUZA MBEGU ZA KIUME



Kemikali zinazopatikana katika baadhi ya bidhaa ambazo hutumiwa kila siku kama vile dawa ya kusugua meno, sabuni na mafuta ya kujikinga kutokana na miale hatari ya jua zinaweza kuharibu mbegu za uzazi za wanaume.

Kwa mara ya kwanza watafiti wanaonya kuwa bidhaa hizo zina uwezo wa kuanthiri uwezo wa mbegu za uzazi za wanaume kuzalisha mwanamke.
Kemikali zinazopatikana katika dawa za kusugua meno zinasemekana kuharibu nguvu za mbegu za kiume kuweza kuzalisha.Wanasayansi hao wanasema kwamba bidhaa hizo zina kemikali ambazo zinachangia matatizo ya uzazi kwa wanaume katika nchi za magharibi.

Takriban mwanamume mmoja kati ya sita aliyeoa nchini Uingereza anakumbwa na tatizo la kuzalisha na tatizo la utasa ndio kiini kikubwa cha hali hiyo.
 
Uchunguzi huu ulifanywa na watafiti kutoka Uingereza na Uholanzi na walifanyia uchunguzi kemikali 100 kila siku huku wakigundua kuwa thuluthi moja ya kemikali hizo ziliathiri uwezo wa Manii kufikia katika mayai ya mwanamke.


Dawa ya meno inaweza kuathiri mbegu za uzazi
Utafiti huu uliandikwa katika jarida la afya la EMBO na watafiti wanasema nyingi ya kemikali hizo hatari zinapatikana katika mafuta yanayotumiwa kujizuia na miale hatari ya jua.
Kemikali nyingine inajulikana kama Triclosan, ambayo inapatikana katika sabuni na dawa ya kusugua meno.
Uchunguzi wa maabara ulionyesha kuwa kemikali hizo zinaathiri uwezo wa Manii ikitafuta mayai ya mwanamke kuweza kuizalisha.
Kadhalika kemikali hizo pia zinaharibu kabisa manii kiasi cha kukosa hisia kwa homoni za mwanamke.
Mabadiliko haya yanapotokea kwa mbegu za kiume, huifanya kuwa vigumu kuweza kuzalisha.
Watafiti hao wanasema kuwa mchanganyiko wa kemikali hizo ni hatari zaidi kwa mbegu hizo.
Kemikali hizi hujulikana kama kemikali zinazoathiri jinsia kwa sababu ni sehemu ya kemikali zinzzoathiri homoni za mwili wa mwanamume.
Mwaka jana shirika la afya duniani lilihusisha kemikali hizo na saratani ya matiti na pumu.

Taarifa ya Wizara ya Afya kuhusu ugonjwa wa homa ya Dengue......



TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UGONJWA WA HOMA YA DENGUE “DENGUE FEVER”



Utangulizi

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa Umma juu ya mwenendo wa ugonjwa wa homa ya dengue yaani “dengue fever” hapa nchini.Ugonjwa huu umethibitishwa baada ya sampuli zilizochukuliwa kutoka kwa watu waliohisiwa kuwa na ugonjwa huu jijini Dar es Salaam kupelekwa kwenye maabara yetu ya Taifa Dar es salaam na kuthibitisha kuwa na virusi vya homa ya dengue mnamo mwishoni mwa mwezi wa Januari 2014. Hadi sasa idadi ya wagonjwa ambao wamethibishwa kuwa na ugonjwa huuni 400 na Vifo 3. Kwa wiki iliyoshia tarehe 9 Mei 2014 ya idadi ya wagonjwa waliogundulika mkoani Dar es salaam ni 60 (42-Kinondoni, 14-Temeke na 4-Ilala) na idadi ya wagonjwa waliopo wodini mpaka sasa ni 13.

Aidha, mlipuko wa ugonjwa huu si mpya hapa nchini kwani uligundulika kwa
mara ya kwanza mnamo Juni 2010 mkoani Dar es Salaam ambapo idadi ya watu 40 walithibitika kuwa na ugonjwa. Pia, kati ya mwezi Mei hadi Julai 2013,wagonjwa 172 walithibitishwa kuugua ugonjwa huu.

Homa ya Dengue

Homa ya dengue ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes.

Dengue in ugonjwa uliosambaa duniani katika nchi za ukanda wa joto. Takribani asilimia 40 ya watu wote duniani wanaishi katika nchi zenye ugonjwa huu. Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinathibitisha kuwa takribani matukio milioni 5 ya Dengue yanatolewa taarifa kila mwaka. Watu laki 5 hulazwa hospitali kwa kuathirika na Dengue kali. Homa ya Dengue imeshatokea katika nchi zipatazo 34 barani Afrika.

Hapa Afrika Dengue ni ugonjwa unaojulikana kwa kiwango kidogo sana. Licha ya kwamba milipuko ya kwanza imetokea tangu mwanzoni wa karne ya 19. Matukio ya Ugonjwa huu yameongezeka Afrika tangu miaka ya 1980, matukio mengi yakitokea nchi za ukanda wa Mashariki mwa Afrika ikiwa ni pamoja na Msumbiji, Somalia, Kenya, Komoro, Djibouti na Tanzania. Ikumbukwe kuwa jina “Dengue” linatokana na neno “Dinga” la kiswahili linalolomaanisha ugonjwa unaotakana na pepo yaani Kudinga pepo. Mabaharia wa Kispanish walipokuja kwenye pwani ya Afrika Mashariki walirudi kwao na kuuita “Dengue”.

Dalili za ugonjwa huu ni homa, kuumwa kichwamaumivu ya viungo na uchovu Dalili hizi huanza kujitokeza kuanzia katisiku ya 3 na 14 tangu mtu alipoambukizwa kirusi cha homa ya dengue. Kwa wakati mwinginedalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria, hivyo basi wananchi wanaombwa kuwa wakati wakipata homa kuhakikisha wanapima ili kugundua kama wana vimelea vya malaria ua la ili hatua stahiki zichukuliwe.

Kuna aina 3 tofauti za namna ugonjwa huu unavyoweza kujitokeza iwapo mtu aking`atwa na mbu mwenye virusi hivi;

i.Homa ya dengue (Dengue Febrile Illness): Aina hii huambatanana dalili kuu tatu za homa kali ya ghafla, kuumwa kichwa na maumivu ya viungo au uchovu.Aidha, kwa Tanzania mpaka sasa zaidi ya asilimia 90 ya wagonjwa wamejitokeza na dalili hizi.

ii.Dengue ya damu (Dengue Haemorrhagic Fever): Aina hii yahoma ya dengue huambatana na dalili za mgonjwa kutokwa na damu kwenye fizi au puani, vile vile kutokwa na damu chini ya ngozi.Iwapo mgonjwa huyu ataumia sehemu yoyote ni rahisi kwake kupoteza damu nyingi kupitia kwenye michubuko.

iii.Dengue ya kupoteza fahamu (Dengue Shock syndrome): Aina hii ya homa yadengue huambatana na mgonjwa kupoteza damu nyingi ambayo hupelekea mgonjwakupoteza fahamu. Dalili hizi zimeonekana kwa mgonjwa 1 kati ya wagonjwa 400 waliokwisha kuthibitishwa kuwa na ugonjwa hapa nchini.
 
Kirusi cha homa ya Dengue kinaambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kwa kuumwa na mbu wa Jamii ya Aedes, na hasa Aedes aegypti. Mbu huyu anaishi katika mazingira ya makazi ya binadamu. Huuma wakati ya mchana ndani ya nyumba au kwenye maeneo yenye vivuli, hususani majira ya asubuhi na jioni kabla jua halijazama.

Mbu huyu anazaliana katika maji yaliyotuama hasa kwenye vyombo vya nyumbani, makinga maji ya paa za nyumba, matairi ya gari, ndoo, vikopo, na kadhalika. Kwa bahati mbaya mbu huyu huweza kuzaliana katika vifaa vidogo vidogo ambavyo watu wengi huvidharau. Hivi ni pamoja na makopo ya kuotesha maua, vikombe, vifuu vya nazi, na kadhalika. Majani mapana yanayohifadhi maji ni mazingira mazuri kwa kuzaliana kwa mbu huyu, hivyo maeneo ya bustani siyo ajabu kuwa mahali pazuri kwa mbu hawa.

Ugonjwa huu hauambukizi kwa kumhudumia mgonjwa au kugusa majimaji yanayotoka kwa mgonjwa. Homa ya dengue inaweza kutibika kama mgonjwa atapelekwa hospitali mapema na kupatiwa matibabu ya haraka.Hakuna dawa maalumu ya ugonjwa wala chanjo bali mgonjwa anatibiwa kutokana nadalili zitakazoambatana na ugonjwa huu kama vile homa, kupungukiwa maji au damu. Endapo mgonjwa atachelewa kupatiwa matibabu, mgonjwa anaweza kupoteza maisha.

Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya dengue

Kuangamiza mazalio ya mbu

  • Fukia madimbwi ya maji yaliyotuamaau nyunyuzia viuatilifu vya kuua viluwiluwivya mbu kwenye madimbwi hayo
  • Ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile: vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.
  • Fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
  • Hakikisha maua yandayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama
  • Funika mashimo ya maji takakwa mfuniko imara
  • ΓΌSafisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama

Kujikinga na kuumwa na mbu
  • Tumia viuatilifu vya kufukuza mbu “mosquito repellants”
  • Vaa nguo ndefu kujikinga na kuumwa na mbu
  • Tumia vyandarua vilivyosindikwa viuatilifu (kwa wale wanaolala majira ya mchana na hasa kwa watoto)
  • Weka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi


Hatua zinazochukuliwa na Wizara

(i)Hatua za Dharura

Uratibu

  • Timu ya Taifa ya Maafa inayoshirikisha wadau mbalimbali ikiwemo wa Halmashauri za Jiji na Wadau wa Maendeleo hukutana kila mara 2 kwa wiki kutathmini mikakati ya dharura iliyowekwa.
Uelemishaji na Uhamasishaji wa Jamii
  • Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilitoa tamko la Serikali kwa nyakati tofauti kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Dengue. Tamko la kwanza lilitolewa kwenye vyombo vya habari tarehe 04 Februari 2014 na Machi 2014.
  • Kuendelea kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa huu kupitia kwa Waganga Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya kwa Tanzania Bara. Aidha taarifa hii pia iinajumuisha namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa (Ainisho la Ugonjwa), “Ukweli Kuhusu Ugonjwa“(Fact sheet), Mwongozo kwa watumishi wa afya wa namna ya kuchukua sampuli. Vipeperushi vinavyoelezea jinsi ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huu vitatolewa.
  • Kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia Radio, na Runinga. Aidha Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri za jiji wameendelea kutumia Maafisa Afyaikiwemo wa kata kuwaelemisha wananchi namna ya kudhibiti ugonjwa kwakutumia vipaza sauti, uongozi wa mitaa

Mafunzo kwa watalaam wa Afya
  • Kuendelea kutoa elimu ya Afya kwa Watumishi wa Afya ikiwa pamoja na madaktari na mafundi maabara namna ya kutambua ugonjwa huu. Aidha watumishi wa hospitali za Muhimbili, Mwananyamala, Amana na Temeke wamekwisha kupewa mafunzo haya na bado wanaendelea kupewa kupitia mikutano yao ya asubuhi (Clinical meetings). Mafunzo haya pia yanaendelea kutolewa kwa vituo vya chini kupitia Halmashauri

Kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji na mawasiliano
  • Kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na mipakani kupitia mfumo wa saveilensi ya Wizara. Aidha, pamoja na Mwongozo huu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imetoa maelekezo kwa Waganga wakuu wa mikoa na wilaya hapa nchini kutoa taarifa za wagonjwa wa Dengue Fever kupitia taarifa za kila juma.
  • Kutoa miongozo ya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika maeneo ya mipakani kuhusu kutokuwepo kwa aina yoyote ya vikwazo vitakavyowekwa kwa ajili kwa wasafiri. Aidha maelekezo hayo yameainisha kuwa iwapo msafiri anayeondoka au kurudi nchini akiwa na dalili tajwa atoe taarifa kwa watumishi wa afya wa mpakani ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa
  • Kufuatilia kwa karibu ongezeko la wagonjwa wenye homa isiyo kuwa ya malaria kwa Mikoa na Wilaya zote nchini ili kuweza kufanya uchunguzi wa kina iwapo kuna ugonjwa huu. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeshafanya utafiti mkoani Kagera, Morogoro na Kigoma na kuthibitisha kuwa haijaadhirika na dengue.
  • Kuanzishwa kwa vituo maalum vya ufuatiliaji wa ugonjwa huu katika Hospitali za Manispaa za jiji la Dar es Salaam (Mwananyamala, Amana na Temeke). Aidha, Kituo cha ‘International School of Tanganyika – IST’ kilichopo Manispaa ya Kinondoni na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zinaendelea na ufuatiliaji wa ugonjwa huu. Aidha Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii itafungua pia vituo mkoani Tanga na Mtwara, mikoa imayopakana na nchi jirani yaani Kenya na Msumbiji ambako ugonjwa huu pia umetolewa taarifa.
  • ·Kupeleka taarifa ya mlipuko huu Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) kama mwongozo wa Kanuni za Afya za Kimataifa uvyaoelekeza.
Upimaji na Tiba
  • Kuimarisha uwezo wa kutambua ugonjwa huu kwa kina kupitia maabara ya Taifa (NHLQATC) iliyopo NIMR. Vile vile Wizara imepeleka vipimo sawia yaani “Dengue Rapid Test Kits” kwa vituo vya Dar es Salaam kuimarisha utambuzi. Vituo hivo ni pamoja na hospitali za Muhimbili, Amana, Mwananyamala, Temeke Hospital, na IST kliniki. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeagiza Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kuhakikisha vitendanishi hivi vinakuwepo ili kurahisisha upatikanaji wake kwa Halmashauri zote na kupelekwa kwenye vituo vya chini zaidi. Wizara imeagiza vipimo sawia 750 vya kunyongeza ambavyo tunatarajiwa kuvipata tarehe 22.5.2014
  • Wizara imeweka utaratibu wa kuhakikisha vifaa Tiba vinapatikana wakati wote katika vituo vyote kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa watakaogundulika na kuwa na ugonjwa huu.

Udhibiti wa mbu na mazalia
  • Kudhibiti mbu kupitia kwa kupulizia na kunyunyizia viuatilifu katika baadhi ya maeneo yaliyoathirika katika mkoa wa Dar es salaam ambayo wametoka wagonjwa wengi wa Dengue. Hii inalenga kuangamiza mbu wapevu na viluwiluwi.
Utafiti
Taasisi ya Utafiti ya magonjwa ya Binadamu (NIMR) iko katika maandalizi ya kufanya utafiti kuhusu dengue kwa kuangalia maaeneo makubwa mawili.
  • Ukubwa wa tatizo katika binadamu
  • Mbu waambukizao ugonjwa wa homa ya Dengue- kujua jamii husuka, tabia ya kuuma watu, wapi wanapopendelea kuuma, wapi wanakozaliana kwa wingi na mazingira yao ya kawaida.
Tafiti hizi zinaanzia Dar es Salaam na kuhusisha wilaya zote tatu (Ilala, Kinondoni, Temeke). Tafiti zitaendelea katika baadhi ya mikoa, ikiwa ni pamoja na mikoa 8 ambako vituo vyetu vipo.Takwimu zitakazopatikana zitaboresha mbinu za kupambana na ugonjwa huu

(ii)Hatua za Kudumu

  • WAUJ imeandaa Mpango wa wa namna ya kukabiliana na ugonjwa wa Homa ya Dengue. Mpango huu kwa kushirikisha sekta mbalimbali.
  • Kuimarisha mfumo wa ufuatiliaji wa ugonjwa wa Dengue

Hitimisho

Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu kuhusu ugonjwa huu kwani hauambukizwi kwa kumhudumia mgonjwa au kwa kugusa majimaji yanayotoka kwa mgonjwa. Hata hivyo tunawashauri wananchi kwenda kwenye vituo vya afya haraka pindi wanonapo dalili za ugonjwa huu.

Mlipuko wa Dengue unadhihirisha kuwa mazingira yetu tunayoishi si salama. Ikumbukwe kuwa, kwa sehemu kubwa, ugonjwa huu unachochewa na mazingira machafu. Aidha mvua hizi kubwa zinazoendelea zonachangia kuongezeka kwa mazalio ya mbu. Utupaji, uzoaji na uhifadhi wa taka katika miji yetu hauridhishi kiasi ambacho kinatoa fursa kwa mazalio ya mbu kuongezeka na hata kuwa karibu zaidi ya makazi ya binadamu.

Kwa kuwa, hadi sasa hakuna chanjo wala dawa maalumu kwa ajili ya kudhibiti au kutibu ugonjwa huu, njia kubwa ya kupambana na ugonjwa huu ni kumzuia binadamu asimwe na mbu. Hivyo basi, mbinu shirikishi za kutokomeza mbu inabidi zitiliwe mkazo katika mapambano dhidi ya homa ya Dengue. Njia bora na rahisi ni kuhakikisha mazalio yote ya mbu yanatokomezwa. Na hili laweza kufanywa na kila mtu kwa nafasi yake.Tunashauri watu wavae nguo zinazofunika mikono na miguu na dawa zinazofukuza mbu (mosquito repellent). Tunaelewa kuwa si kila mtu atakuwa na uwezo wa kununua dawa hizi na ndiyo maana tunakazania swala la kuangamiza mazalia ya mbu ambalo ni jukumu letu wote.Tunaendelea kuhamisisha watu na hasa watoto walale ndani ya vyandarua venye viatilifu wanapolala wakati wa mchana.

Ningependa kuwakumbusha wananchi wa Tanzania kuwa, huu ni muda muafaka wa kuzingatia utunzaji bora wa mazingira yetu. Tukitunza mazingira yetu, nayo yatatutunza na kutuepusha na maradhi yanayoambatana na mazingira machafu.

Charles A. Pallangyo
Katibu Mkuu
12 May 2014