Showing posts with label Fumanizi. Show all posts
Showing posts with label Fumanizi. Show all posts

Jamaa anusurika Kunyofolewa Jicho baada ya kufumaniwa akingonoka na Mke wa Mtu ......Alivizia mwenye mke kasafiri, akazama Chumbani


Mkazi wa Mtaa wa Lagos, Wazo Mivumoni, Msitu wa Pande jijini Dar es Salaam, Nuru Makala ‘Baba Eliza’ (42) Jumatano iliyopita alikumbwa na majanga baada ya mwanaume aliyejulikana kwa jina la Yusuf Ally ‘Mgosi wa Ndima’ kudai amemfumania Baba Eliza akiwa na mkewe ambaye jina halikupatikana.

Tafrani hiyo ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita, Juni 18, mwaka huu kwenye nyumba yake iliyopo Mtaa wa Lagos, Msitu wa Pande.
Akizungumzia  tukio  hilo  mbele  ya  wanahabari  waliokuwa  eneo  hilo  wakisaka  habari, Yusuf  Ally  ambaye  ni  mume  wa  mwanamke  aliyefumaniwa  alisema:
 
“Nilikuwa katika harakati za kumchunguza mke wangu kinyemela kwa siku nyingi kama anachepuka, nikabaini kuna mawasiliano yenye shaka kati yake na huyo jirani yangu.

“Nilipomuuliza mke wangu alikiri, akasema amekuwa akimwambia jirani yangu kwamba haiwezekani lakini jamaa anakomaa tu anamwambia wakutane, tena wakutane humu ndani.
 
“Ndipo nilipoamua kumuandaa mke wangu kwa mtego amwambie jamaa kuwa leo (siku ya tukio) sitakuwepo na sitarudi ili kumpa nafasi jamaa kuja kujinafasi. Baada ya kukamilisha mtego niliwasiliana na kamanda wa sungusungu wa eneo hilo, Kapteni Makumba na kumuelezea kinagaubaga.

“Kapteni Makumba aliwaandaa vijana wake ambapo kuanzia mishale ya saa mbili usiku walijibanza kwenye kichaka kilichopo mbele ya nyumba huku akifanya mawasiliano na mimi.”
 
Mgoni  akiomba  Msamaha.

Yusuf aliendelea kudai kuwa, ilipotimu saa tano usiku kukiwa kumetulia, Baba Eliza alionekana akikaribia nyumba ya jirani yake huyo kwa hatua za kunyata na kuangalia kulia na kushoto kisha akazama ndani huku mkononi akiwa ameshika kifurushi kilichobainika baadaye kwamba kilikuwa na machungwa kadhaa.

Alisema muda mfupi baada ya kuingia, sungusungu mmoja alikwenda kujibanza kwenye dirisha la chumba na kupiga chabo kilichokuwa kikiendelea ambapo alimshuhudia Baba Eliza akichojoa nguo chapchapu tayari kwa mtanange, sungusungu huyo akawatonya wenzake.
 
Yusuf akazidi kusema kwamba wote walitoka kichakani na kwenda kuvamia chumbani ambapo walimkuta mkewe aliyekuwa bado hajaanza kuvua nguo kwa sababu alijua majanga yatatokea muda si mrefu akiwa anajiandaa kufanya hivyo kiaina.

Baada ya hali kuwa shwari, Kamanda wa Sungusungu, Kapteni Makumba alianza kumsomea mashitaka jirani huyo aliyekuwa mtupu muda huo mbaye hakuwa na la kusema zaidi ya kuomba radhi na kumtupia lawama ibilisi kwamba ndiye aliyemshawishi na haikuwa amri yake.
 
Raia aliyeshuhudia mkasa huo akionesha sehemu ya kitanda  iliyochafuliwa na mgoni kwa kinyesi.
 
Sungusungu walimtaka Baba Eliza kumlipa fidia ya shilingi milioni moja mwenye mke kwa kitendo cha kumdhalilishia ndoa yake.

Source:  Ijumaa  Wikienda/ GPL

SMS ZA KIMAPENZI ZA LULU ZANASWA, YADAIWA ALIKUWA AKIZITUMA KWA KIGOGO MUME WA MTU

"Ni  muda  mrefu  nimekuwa  nikifuatilia  mienendo  ya  mume  wangu  kutokana  na  tabia  yake  kubadilika  sana  siku  za  hivi  karibuni, nikabaini  kuwa  kuna  msichana  anawasiliana  naye  kwa  kutumiana  meseji  za  mapenzi, sikuwa  na  haraka  nikaamua  kufanya  uchunguzi  wangu  kimyakimya"
"Wiki  iliyopita  mume  wangu  akiwa  amekwenda  kuoga  akasahau  kuzima  simu  yake,na  siyo  kawaida  yake  kuacha  simu  yake  bila  kuizima,mara  meseji  ikaingia,nikaangalia  nikaona  jina  la  mtumaji amesevu  Lulu, moyo  ukalipuka"
Ndivyo  alivyoanza  kuongea  mama  mmoja  wa  makamo  anayefanyakazi  katika  ofisi  moja  nyeti  katikati  ya  jiji  la  Dar  alipokuja  kuongea  na  mwandishi  wetu  wiki  iliyopita  baada  ya  ndoa  yake  kuingiliwa  na  mdudu  mbaya....
Akiongea  kwa  masikitiko  makubwa, mama  huyo  ambaye  hakupenda  kutaja  jina  lake  kutokana  na  unyeti  wa  kazi  anayoifanya, alidai  kuwa  msichana  huyo  anayetaka  kuiharibu  ndoa  yake  yenye  miaka  25  jina  lake  ni  Elizabeth  Michael....
Mama  huyo  alidai  kuwa  jina  hilo  alilibaini  baada  ya  kukuta  meseji  za  mapenzi  kwenye  simu  ya  mume  wake  na  yeye  kuamua  kuifuatilia  namba  hiyo  kwa  kufanya  kama  anataka  kumtumia  pesa  msichana  huyo  na  kukugundua  jina  hilo....
Akiongea  kwa  upole, mama  huyo  alidai  kuwa katika  simu  ya  mume  wake, jina  la  mtumaji  lilikuwa  Lulu, lakini  alipofanya  uchunguzi  wake  wa  kujifanya  kama anatuma  pesa  kwa  namba  ya  msichana  huyo  ndipo  alipobaini  kuwa  mmiliki  wa  namba  hiyo  ni  Elizabeth  Michael...
Mwandishi  alimuuliza  mama  huyo  kama  anadhani  kuwa  msichana  huyo  anayetaka  kuiharibu  ndoa  yake  ni  muigizaji  maarufu  wa  filamu  hapa  nchini  Elizabeth  Michael  "Lulu", lakini  alikataa  kuthibitisha  hilo  kwa  madai  kuwa  tangu  siku  hiyo  namba  ya  binti  huyo  imekuwa  haipatikani....
"Baada  ya  kugundua  siku  ile ,  nilichukua  simu  yake  na  kutaka  kuwasiliana  naye  ili  niweze  kumuonya  mwenyewe  kimyakimya  kwa  wakati  wangu, wala  sikuwa  na  lengo  la  kuja  kwenye  vyombi  vya  habari , lakini  sikuwahi  kumpata  hewani  tena  kila  nilipojaribu  kumpigia"Alisema  na  kuongeza:
"Huenda  mume  wangu  alishtikia  kuwa  nimeona  ujumbe  ule, kwa  sababu  mimi  nilipoisoma  meseji  ile  sikuifuta, ili  akiona  meseji  imesomwa  aelewe  nimeshajua  kila  kitu, pengine  ndiye  aliyemwambia  binti  huyo  abadili  namba  yake"
Mwandishi  alimuomba  mama  huyo  ampatie  namba  ya  huyo  msichana  ili  kuweza  kujua  kama  ni  Lulu  muigizaji  ama  siyo ( mwandishi  anazijua  namba  zote  za  Lulu ), lakini  namba  hiyo  ni  tofauti  na  anazotumia  Lulu  Mwenyewe....
Mwandishi  alipojaribu  kama  kumtumia  pesa  msichana  huyo, jina  lililotokeza  ni  Elizabeth Michael, na  alipojaribu  kuipiga  namba  hiyo  ilikuwa  haipatikani  hewani....
Juhudi  za  kumsaka  Lulu   ili  kuona  kama  anaitambua  namba  hiyo  hazikuzaa  matunda  kutokana  na  namba  zake  mbili  kutopatikana  na  nyingine  ikiita  bila  kupokelewa....
 
Angalizo:
Baadhi  ya  wasichana  wa  mjini  wamekuwa  wakitumia  majina  ya  wasanii  maarufu  katika  nyendo  zao  ili  kuwatapeli  watu. Miongoni  mwa  njia  wanazotumia  ni  pamoja  na   kujisajili  kwenye  mitandao  ya  kijamii  kwa  majina  ya  watu  maarufu  ili  kuwatapeli  watu.

Source: Gazeti la Visa