Mara
nyingi tumekuwa tukiwaza mambo makubwa sana katika kuleta mvuto au
mshawasha wa mapenzi hasa pale muwapo chumbani tayari kupeana tiba
ambayo hakika humfanya kila mtu asahau shida.
Hakuna
haja ya kuumiza kichwa sana kwani yapo mambo mengi sana ya kuwafanya
mpate hamasa wewe na mpenzi wako na mujione kuwa ni watu spesho kuliko
wengine,moja ya jambo hilo ni aina ya taa iliyoko chumbani kwenu,taa
hafifu na yenye rangi ya kuvutia kama vile rangi ya kijani,zambarau au
pink ni silaha nzuri sana inayoamsha hisia za huba kwa wapendanao wawapo
chumbani kwa sababu zifuatazo:-
*Taa
za rangi na zenye mwanga hafifu huchangia kukufanya mpenzi wako awe na
muonekano wa pekee wenye kuleta hisia zinazokuongezea matamanio kwani
huonekana tofauti sana na awapo sehemu zinginekama vile awapo nje.
*Mwanga
hafifu husaidia kupendezesha mavazi ya mpenzi wako kama vile night
dress,briefs au knickers na kukufanya umuone kama malkia ambaye amekupa
fursa ya pekee ya kuwa nae kwa usiku huo.
*
Mwanga hafifu na wenye rangi ya kupendeza humfanya mwanamke/mwanaume
wako kudeka na kutoa kauli zenye kuvutia zilizojaa maneno matamu kama
vile ooh husband,swetlove,laaziz nk. hakika hayatakauka na hivyo
kufanya shughuli yenu kuwa spesho na yenye upekee wa hali ya juu.
Utafiti
unaonesha kuwa kwenye mwanga mkali ni rahisi zaidi kumfanya mtu
kujiamini kupita kiasi hivyo huweza kuchangia kutoa kauli zisizokuwa na
dalili ya upole hivyo hupoteza raha kwa wale wakati huo maalum unapokuwa
na mwandani wako.
Ni
Jambo la msingi sana kuwa mbunifu katika mapenzi ili kuleta mahaba
yatakayochangia kumteka mpenzi wako na kumfanya amiss uwepo wako pale
anapothubutu kuwa mbali nawe hata kwa siku moja.