Ray C Foundation yamuokoa video model wa ‘Ice Cream’ ya Noorah aliyeathirika na dawa za kulevya




Miongoni mwa watu ambao tayari wameanza kusaidiwa na taasisi mpya ya Ray C foundation iliyoanzishwa na mwanamuziki Rehema Chalamila aka Ray C mwaka huu, kwaajili ya kuwasaidia watu walioathirika na dawa da kulevya ni pamoja na video model aliyecheza kwenye video ya Noorah ‘Ice Cream’.

Model huyo aitwaye Doreen, hivi karibuni aliripotiwa kuwa hali yake ni mbaya kutokana na kuathirika na dawa za kulevya alizotumia kwa muda mrefu.
 
Baada ya Ray C kupata taarifa zake aliamua kumtafuta ili amsaidie, na baada ya kufanikiwa kumpata hivi sasa tayari ameanza tiba ya methadone.
 
Ray C amepost picha akiwa na Doreen na kuandika:
“Mungu ni mwema sana!!tena sana!!nilipotangaza kuwa nimefungua taasis yangu ya kuelimisha jamii kuhusu athari za madawa ya kulevya, nilipata emails nyingi kuhusu kumsaidia Doreen video queen aliecheza kwenye video ya Noorah iitwayo ice cream!!nilijaribu kumtafuta baada ya kuona picha yake kwenye website ya vibe magazine!!roho iliniuma sana nikamwomba Mungu anisaidie nimpate!!
 
"Namshukuru Mungu Asubuhi ya juzi Nikiwa ofisini nikaona email kutoka kwa dada yake Doreen kichwa cha habari Kikiwa Msaada,nilipoisoma chozi lilinitoka nika reply Mara moja nilimuomba anitumie namba yake tuongee,nikampigia akaniambia doren Hali yake si Nzuri kutokana na drugs,moyoni nikawa Nafikiria Huyu dada angejua jinsi nilivyomtafuta mdogo wake !!!!! 
 
"Ikawa Kama bahati,tukaongea kwa kirefu sana na nikamwambia tukutane kitengo cha madawa Mwananyamala!nilipomuona Doren Kwa Mara ya kwanza nilifurahi kupita maelezo,ila nikawa na wasiwasi kuhusu utayari wake wa kuanza Tiba ya methadone isije ikawa amelazimishwa kuja akaniambia dada yangu Nimechoka Maisha ya utumwa nisaidie!!hicho ndo nilichotaka kusikia nikamwambia Kwa uwezo wa Mungu Shetani ameshindwa!!!!!!
 
"Am soooo happy Doren ameanza Tiba ya methadone!!!wapenzi wote wa bongo flava nawaomba tumwombee mdogo wetu aweze kusimama kwenye Tiba na ashinde majaribu ya Shetani na aishi kwa amani bila utumwa wa shetani.God We Trust!!!I love You my lil sister…..
 
"Nawahamasisha wengine huko Mliko mwenye ndugu,Jamaa au rafiki,njoo Katika taasis yetu uweze kusaidiwa!usikubali Maisha ya utumwa wa madawa ya kulevya,njoo tukusaidie…Ray C Foundation pamoja na Kitengo cha Methadone We love you guys,We can help you….”
 
Tazama video ya ‘Ice Cream’ aliyocheza Doreen miaka kadhaa iliyopita