Abiria wa Bodaboda wageuziwa Kibao.....Abiria Ukikutwa umepanda pikipiki isiyo na lesini utafikishwa mahakamani




Meya  wa  jiji  la  Dar es Salaam, Dr Didas Massaburi  amesema  abiria  wataokutwa  wakiwa  wamepanda  Pikipiki  maarufu  kama  Boda boda  katika  maeneo  ambayo  pikipiki  hizo  hazina  leseni  ya  kufanya  biashara  watakamatwa  na  kufikishwa  mahakamani  pamoja  na  dereva.....

Alisema  pia  wafanyabiashara  wadogo  wataokutwa  wakifanya  biashara  katika  maeneo  yasiyoruhusiwa  kisheria  ikiwemo  maeneo  ambayo  yamefanyiwa  usafi  na  Halmashauri  ya  jiji  la  Dar  es Salaam  hivi  karibuni  watakamatwa  na  kufikishwa  mahakamani.....

Meya  huyo  aliyasema hayo  jijini  Tanga  hivi  karibuni  alipokuwa  akizungumza  na  waandishi  wa  habari  ambao  walitaka  kufahamu  msimamo  wa  Jumuiya  ya  Tawala  za  Mitaa  Tanzania   ( ALAT )  kuhusu  kunyanyaswa  kwa  waendesha  bodaboda  katika  maeneo  mbalimbali nchini