Penny afunguka: Sitaki kusikia habari za Diamond....Nina mpenzi wangu mwingine





Zilipendwa wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Penniel Mungilwa ‘Penny’,  amefunguka kuwa hataki kumsikia mpenzi wake huyo wa zamani kwa madai kuwa amefungua ukurasa mpya wa uhusiano na mtu ambaye hata hivyo hakuwa tayari kumweka wazi. 
 
Penny alisema hayo hivi karibuni jijini Dar wakati akizungumza na Risasi lililotaka kujua anazungumziaje tuzo saba za Kilimanjaro alizojizolea Diamond ambapo  majibu yaliyopatikana yalikuwa: “Wanaotakiwa kuzungumzia hili ni mkewe na ndugu zake, mimi sitaki.”
 
Alipoulizwa mke wa Diamond ni nani alisema: “Mnamjua” na kuicha historia ikibaki kuwa Penny na msanii huyo waliwahi kuwa katika mapenzi mazito ya njiwa kabla ya kumwagana na mwanamuziki huyo kumrudia mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu, ambaye mwenyewe anapenda aitwe mke mtarajiwa.