KIZAAZAA: AUNTY LULU AJUTA KUMVULIA NGUO AMANI, ADAI HAKUJUA KAMA ANA WIVU KIASI HICHO



MSANII wa filamu Bongo,Lulu Semagongo 'Aunty Lulu' anadai kuwa anajuta kumvulia nguo mwandani wake aliyemtaja kwa jina la Amani ambaye hivi karibuni alimshushia kipigo kikali baada ya kutaka kwenda kujirusha usiku kwenye kumbi za starehe....

Akizungumza na Mpekuzi wetu,Aunty Lulu alisema katika siku ya tukio ni kweli alitaka kwenda kupata raha mwenyewe kwenye moja ya klabu za
starehe usiku na alimpa taarifa jamaa yake huyo lakini akamgomea kwenda kwani alihisi angeenda kumsaliti....

Msanii huyo aliendelea kusema kuwa jamaa yake huyo ana wivu balaa na hilo limekuwa likimpa shida kwani wakati mwingine anashindwa kuongea na wanaume ambao mpenzi wake hawafahamu maana huwa anahisi ni hawala zake....

"Najuta kumpa penzi Amani kwani sikujua ana wivu mkubwa kiasi hiki,hataki kunipa uhuru wa kwenda kujirusha kama ilivyokuwa siku za awali.Si kweli kwaba nikienda kwenye kumbi za starehe naweza kumsaliti kwani binafsi huwa sipendi kuchanganya wanaume"Alisema msanii huyo.
SOURCE: Mpekuzi