UKAWA Waigomea Serikali Kuhamishwa Machinga Katikati ya Jiji la Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi...

Sakata la kuhamishwa kwa wafanyabiashara wadogo katikati ya Jiji la Dar es Salaam limeingia mdudu baada ya madiwani wa Ukawa kugomea uamuzi uliotolewa na uongozi wa jiji hilo.

Uamuzi huo uliotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi, unadaiwa kutowashirikisha wadau hao na wafanyabiashara wenyewe.

Mwenyekiti wa madiwani wa Ukawa, Manase Mjema amesema Mngurumi ametoa umuzi huo bila pia kumshirikisha hata Meya wa Ilala, Charles Kuyeko.

Wamesema masoko ya Kivule, Tabata Muslim, Ukonga na Kigogo Fresh ambayo mkurugenzi huyo amesema yametengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao, hayajaboreshewa miundombinu yake ikiwamo ujenzi wa vyoo na mabomba ya maji.

Wamemtaka kusitisha mchakato huo mpaka watakapo jadiliana tena.

KOCHA WA TOTO AFRICANS AWAAGA RASMI WACHEZAJI NA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA

 Kocha mkuu wa timu ya Toto Africans mjerumani Martin Grelics jana amewaaga wachezaji na mashabiki wa Toto African mara baada ya mchezo kati ya Toto Africans dhidi ya Mgambo Shooting ambao ulimalizika kwa Toto kuibuka na ushisndi wa goli 1-0.

Grelics amesema huo ndio ulikuwa mchezo wake wa mwisho yeye kuifundisha Toto kama kocha mkuu na tayari ameshabwaga manyanga na akatumia fursa hiyo kuwaaga wachezaji wake na mashabiki wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo kwenye uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

“Huu ulikuwa ni mchezo wangu wa mwisho nikiwa kwenye jiji zuri la Mwanza, najisikia vibaya kuondoka kwenye jiji hili lakini kama nilivyowaambia wiki iliyopita inabidi niondoke”, alisema Grelics baada ya kuzungumzia mchezo kati ya Toto Africa dhidi ya Mgambo Shooting.

Wiki iliyopita Grelics aliuandikia barua uongozi wa timu ya Toto Africans ya kujiuzulu nafasi ya ukocha mkuu kutokana na timu hiyo kuwa na mgogoro na wachezaji hali iliyopelekea wachezaji kugoma kufanya mazoezi kwa ajili ya michezo ya ligi iliyokuwa mbele yao wakidai pesa za mishahara na posho zao.

Toto Africans imecheza mechi tisa, imeshinda mechi tatu, imetoka sare michezo minne na kupoteza mechi mbili huku ikishikilia nafasi ya nane kati ya timu 16 kwenye msimamo wa ligi kuu ya VodacomTanzania bara

Ukawa wateka manispaa Dar es Salaam



mikoani. Vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimefanikiwa kushinda kata nyingi katika jiji la Dar es Salaam na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuongoza mabaraza ya madiwani katika halmashauri za manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke.
Mbali ya kusimamia mabaraza hayo, pia Ukawa unaweza, kwa mara ya kwanza, kuongoza halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
Tangu mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa mwaka 1992, CCM imekuwa ikishinda kata nyingi na hivyo madiwani wake kuunda halmashauri, lakini mwaka huu imepokonywa kata nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita baada ya Ukawa unaoundwa na vyama vya NLD, CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi kunyakua ushindi katika kata hizo.
Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huo yanayoendelea kutangazwa Ukawa umenyakua viti 53 vya udiwani katika majimbo ya Kinondoni, Ukonga, Ilala, Segerea, Temeke, Kibamba, Kawe, Ubungo, Mbagala na Kigamboni wakati CCM ikipata viti 38.
Moja ya Halmashauri ambazo Ukawa wataziongoza ni ya Kinondoni ambako umetwaa kata 22 kati ya 34. Katika halmashauri hiyo yenye majimbo ya Kawe, Ubungo, Kibamba na Kinondoni, Chadema imenyakua kata 17, CUF imeshinda kata 6, na CCM imetwaa kata 9 huku yakisubiriwa matokeo ya kata mbili.
Halmashauri ya Ilala yenye majimbo ya Ilala, Ukonga na Segerea, matokeo yanaonyesha kwamba Chadema ina kata 19, CCM kata 15 na CUF kata mbili. Madiwani wa kata hizo ndio watakutana kuteua meya na naibu meya wa halmashauri ya Ilala.
Halmashauri ya Temeke inayoundwa na majimbo ya Temeke, Kigamboni na Mbagala ina jumla ya kata 31. Katika jimbo la Temeke CCM ina kata 7, Chadema 5 na CUF 1; Kigamboni: CCM kata 6, Chadema 2 na CUF 1, wakati Mbagala CCM kata 7 na CUF tatu.
Aidha, upinzani umefanikiwa kutwaa majimbo sita kati ya 10. Majimbo hayo na majina ya wabunge wake kwenye mabano ni Kawe (Halima Mdee – Chadema), Kinondoni (Maulid Mtulia – CUF), Temeke (Abdallah Mtolea – CUF), Ukonga (Mwita Waitara –Chadema), Ubungo (Saed Kubenea – Chadema), Kibamba (John Mnyika- Chadema).
Waitara amepata ubunge baada ya kumbwaga aliyekuwa meya wa Ilala, Jerry Slaa (CCM); Mtolea amemshinda Abbas Mtemvu (CCM); Mdee amemwangusha Kippi Warioba (CCM), na Kubenea amemshinda aliyekuwa meya wa jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi (CCM).
Mnyika amembwaga Fenella Mkangalla (CCM), Mtulia amemshinda Idd Azzan (CCM). Bonna Kaluwa wa CCM ndiye mbunge wa Segerea, Faustine Ndungulile wa CCM amefanikiwa kutetea jimbo la Kigamboni sawa na Mussa Hassan Zungu aliyetetea jimbo la Ilala.
Matokeo ya mikoani
Jimbo la Ndanda lina kata 16; CCM (15), Chadema (1); Tandahimba: kata 30, CCM (10), CUF (16), Chadema (1); Kalenga: kata ni 15, CCM (13), Chadema (3); Iringa Mjini kata 18, Chadema (14), CCM (4); Isimani kata 14, CCM (11) Chadema (3); Ushetu kata 20, CCM (20); Serengeti kata 30, CCM (12), na Chadema (18).
Jimbo la Dodoma Mjini kata 41, CCM (34), Chadema (6); Mpwapwa lina kata 13, CCM (13); Kibakwe kata 18, CCM (18); Mbozi kata 11, CCM (7), Chadema (4); Mtwara Mjini kata 18, CUF (8), CCM (7), Chadema (3); Mwibara kata 12, CCM (7), Chadema (2), TLP (2) na CUF (1); Bunda Mjini kata 14, CCM (10) na Chadema (4); Bunda Vijijini kata 7, CCM (5) na Chadema (2).
Handeni Mjini kata 12, CCM (11), CUF (1); Handeni Vijijini kata 21, CCM (20), Chadema (1), Kilindi kata 21, CCM (20) kata moja haijafanya uchaguzi; Vunjo kata 16, NCCR (8), CCM (4), Chadema (4); Sikonge kata 17, CCM (14), Chadema (3); Kahama Mjini kata 20, CCM (19) Chadema (1).
 Momba kata 14, CCM (8), Chadema (6); Mbeya Vijijini kata 29, CCM (21), Chadema (7); Kisarawe: CCM (14), Chadema (2), CUF (1); Nanyumbu CCM (15), CUF (2), na Bagamoyo kata zote 11 zimechukuliwa na CCM.

Trafiki Anusurika kufa baada ya Kuvaana Uso kwa Uso na Gari Dogo eneo la Bamaga Mikocheni jijini Dar es salaam


Askari mmoja wa kikosi cha usalama barabara ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja amenusurika kufa baada ya kupata ajali akiwa anaendesha pikipiki ya polisi ambayo ilikosa mwelekeo na kugongana uso kwa uso na gari dogo lenye namba za usajili T 681 CUX eneo la Bamaga Mikocheni jijini Dar es salaam ambapo gari hilo lilikuwa likiandeshwa na mwanamke mmoja huku mashuhuda wa ajali hiyo kila mmoja akiwa na mtazamo tofauti juu ya ajali hiyo.

Irene Uwoya amtaka Ndikumana Yanga, mwenyewe aogopa kulogwa.....Asema Uwoya bado ni Mke wake na wanapendana sana


BINTI aliyejaliwa uzuri wa sura anayeng’ara kwenye filamu za Kibongo, anamshawishi mumewe Hamad Ndikumana aje kucheza Yanga ya chini ya kocha, Marcio Maximo.
 
Ndikumana ambaye kwa sasa anaichezea Vital’o ya Bujumbura, Burundi ameweka wazi kwamba binti huyo, Irene Uwoya ambaye ni mkewe ni shabiki wa Jangwani na amekua akimshawishi kila mara kwamba atue Jangwani ili awe naye karibu zaidi kwani hana mpango wa kuondoka Dar es Salaam kwenye kazi zake za filamu.
 
Mchezaji huyo amekiri kushawishiwa mara nyingi lakini alisema hawezi kujipeleka Yanga mpaka timu hiyo itakapomfuata, kama hiyo haitoshi aliongeza kwamba anaogopa kuishi Dar es Salaam kutokana na mambo ya ushirikina yaliyomtokea alipoanza maisha na mkewe ambaye ameshangaa watu wanaozusha kwamba wameachana.
 
“Ananitaka nije kucheza Tanzania alikuwa ananiambia nije Yanga, unajua anaipenda sana Yanga lakini nikamwambia mimi ni mchezaji ninayejiamini siwezi kuja kuomba Yanga wanisajili acha waje wao tuzungumze, yuko tayari kufanya hata ushawishi kwa wadau,” anasisitiza Ndikumana ambaye awali alikuwa akiichezea APOP Kinyras Peyias ya Cyprus.
 
Ndikumana alisema kilichomtoa Cyprus na kuja Burundi pamoja na uhusiano wake na Uwoya.
 
“Kweli nilikuwa Cyprus kama unavyosema lakini kikubwa ambacho kilinirudisha Tanzania ni pale mke wangu alipokaribia kujifungua, niliporudi tu baada ya muda nikaanza kuumwa sana na hivyo kushindwa kurudi Cyprus,” anasimulia.
 
“Tatizo hilo naweza kusema ni mambo yetu ya Kiswahili na ni huko Tanzania ndiyo kulikuwa chanzo, kuna vitu vilikuwa vinanitokea mwilini kiasi kwamba nilikuwa najikuna sana mwili mzima, hospitali nilikwenda na kupima vipimo vyote hakukuonekana kitu, kuna wakati wakaniambia ni fangasi.
 
“Nikaona hapana bora nigeukie upande wa pili wa tiba asilia, nako hali haikuwa rahisi nilizidi kuteseka ilifikia hatua najikuna mpaka vidonda vinatoka miguuni nikaona sasa na vidonda hivi nitarudije Cyprus bora nitibiwe kwanza kabla ya kuondoka.
 
“Ukweli ni kwamba nilizunguka sana kwa wataalamu mbalimbali kiu yangu ilikuwa ni kuhakikisha nakuwa sawa, nakumbuka mwanzoni kama ndani ya miezi miwili nilitumia hadi Sh6milioni kusaka tiba lakini bado ikashindikana, nilikuwa nataka kuhakikisha napona haraka ili niwahi kurudi kazini.
 
“Nilizunguka sana nakumbuka baada ya kuona Tanzania ni vigumu nikaondoka na kuja hapa Rwanda nako nilitibiwa hali haikuwa sawa, nikaenda DR Congo kidogo nikapata nafuu lakini baadaye kuna mtalaamu mmoja akanisaidia tena kwa kiasi kidogo maradhi yakapungua.
 
“Kuna mtu namjua kwamba alikuwa akifanya haya yote, hili nililiamini baada ya kumrudia Mungu, ukiacha ya Mungu pia hata hao wataalamu karibu wote nilipokuwa napita walikuwa wakimtaja sioni kama walikuwa wanadanganya kwani ni watu tofauti wote wamemtaja mtu mmoja, namuachia Mungu na nashukuru sasa nimeanza kurudi katika hali yangu.
 
“Baada ya misukosuko yote hiyo Baba yangu (Ndikumana Kitenge) kule nyumbani ana timu yake ndogo ya vijana, nikawa natumia muda huo kumsaidia majukumu ya kuwafundisha vijana na hapohapo na mimi nafanya mazoezi, nilipoona hali imeimarika nikaenda Vital’O kuwaomba nifanye nao kazi wakakubali na nashukuru walinielewa na kuniamini sasa nipo nao kwa muda.


“Sijasaini mkataba na Vital’O unajua kuna wakati  nafanya mazoezi kuna timu za Ulaya zilikuwa zinataka kunifuata nikaona niende Vital’O ili nijiweke sawa endapo watakuja wanikute katika hali nzuri lakini hao jamaa walivutiwa na mimi wakati nacheza kama beki na sasa hapa natumika kama kiungo mkabaji sijajua kama wakija watanikubali.”
 
Alikutana wapi na Uwoya?
“Unajua Irene nilimpenda kupitia filamu nilipomuona nikataka siku moja nikutane naye, nashukuru Mungu kuna siku wakati nataka kwenda Kigoma katika harusi ya dada yangu nilipitia Dar es Salaam nikakutana naye pale uwanja wa ndege.
 
“Sijabadili dini, ni kweli kwamba tulifunga ndoa ya kanisani lakini sikubadili dini nilitajwa kwa jina la Hamad Ndikumana, tulikubaliana na mke wangu tufunge ndoa mbili ya Kikristo na Kiislamu ikatangulia ile hii nyingine tukasema tutaifunga baadaye lakini muda ukawa mdogo ila tutaifunga hakuna shida.
 
Ni kweli wameachana na Uwoya?
“Kwanza nashangaa hao wanaodai nimeachana na mke wangu wanajua nani amempa talaka mwenzake? Sijaachana na Uwoya, yule ni mke wangu isipokuwa kwa sasa ni kama tumetengana na huko si kuachana labda watu wanachanganya mambo.
 
“Kuna mambo tulishindwa kukubaliana, alikuwa hataki kuja kuishi na mimi kule Cyprus, alikuwa anataka tuishi Tanzania tu, sasa mimi kazi yangu ni soka siwezi kuacha kazi ili nirudi Tanzania niishi na familia yangu bila ya kuwa na kazi hilo lilitufanya tutengane kidogo.
 
“Achana na mtoto nipo na maelewano mazuri na Uwoya hadi sasa tunawasiliana ngoja nikuthibitishie (Anainua simu na kumpigia lakini haipokelewi) nadhani atakuwa katika kazi zake, yupo safarini Afrika Kusini amekwenda kurekodi filamu na hata Krish ni mwanangu kila ninapotaka kumuona namuona bila shida.
 
“Sasa ana miaka mitatu na tumeshamwanzisha shule, anasoma (ananionyesha video fupi Krish aliyorekodiwa akihesabu namba kwa Kiingereza) nadhani sasa utaniamini unajua watu hawajui mimi na Irene ni wapenzi na tunaonana kila tunapopata nafasi.
 
“Hayo ni maneno ya watu tu, unajua Tanzania maneno ni mengi sana, kweli kuna wakati yanasemwa mengi sana ninaposikia nakutana na mwenzangu namuuliza anakataa lakini ukiacha kukataa kwake hata mimi nimeshindwa kuthibitisha hayo madai kwa hiyo nayaacha maisha yanaendelea.
 
“Kila kitu kina muda wake bado naamini siku moja nitarudi kuwa karibu na familia yangu, kwa sasa acha kwanza kila mmoja afanye yake ya kikazi, baadaye tutatulia na kuwa pamoja, watu waache kutugombanisha,”anasisitiza.

Chanzo:  Mwanaspoti

Baba amuingilia bintiye kinyume cha maumbile

Kanisa lawataka wachungaji wajiuzulu CHADEMA


Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini ambaye pia ni Mchungaji wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Joseph Matare amejiuzulu nafasi yake hiyo kutokana na kanisa lake kuwataka wachungaji wake ambao ni viongozi wa vyama vya siasa kuachana na nafasi zao za kisiasa. 
 
Joseph Matare akizungumza na waandishi wa habari mjini Songea amesema kuwa ameamua kujiuzulu nafasi yake ya uongozi wa Chadema Kanda ya Kusini inayojumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma baada ya kanisa lake katika mkutano wake wa kanda kuagiza wachungaji wake ambao ni viongozi wa siasa kuachia nafasi zao na badala yake wasimamie kazi ya Mungu katika makanisa yao.
 
“Kufuatia maagizo ya mkutano huo wa kanisa uliofanyika Njombe nimeamua kutii... nimeamua kujiuzulu na katibu wangu mkuu, Dk Willibrod Slaa nilimjulisha tangu tarehe 4 Juni mwaka huu,” alisema Matare katika taarifa yake ya kujiuzulu.
 
Amefafanua kuwa muda wa viongozi wa kanda ulikuwa ni wa muda na wa mpito hadi uchaguzi wa kanda utakapopita ambao ulipaswa kufanyika Juni 2014 na kwamba muda umeongezwa hivyo ameona aheshimu maagizo yaliyomweka madarakani.
 
Hata hivyo, Matare anasema kuwa anawatia moyo makamanda wote wa Chadema waliobaki kuendelea kupigania nchi ili iondokane na uovu unaotendeka sasa na kwamba Mungu atakuwa nao wale wote wanaotafuta haki kwa ajili ya wananchi walio wengi.

Rais Kikwete: Uchaguzi Serikali za Mitaa kusogezwa mbele


RAIS Jakaya Kikwete amesema uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ulikuwa ufanyike mwezi Oktoba mwaka huu, huenda ukasogezwa mbele kutokana na kutokamilika kwa mchakato wa rasimu ya mabadiliko ya Katiba.
 
Kauli hiyo ameitoa kwenye mkutano wa majumuisho ya ziara yake ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Tanga.
 
Alisema kulingana na hali ilivyo hivi sasa ambapo Bunge la Katiba halijakamilisha kazi zake, ni dhahiri kwamba uwezekano wa kufanyika kwa uchaguzi huo kwa kutumia Katiba mpya haupo.
 
“Kwa mfano, wabunge endapo wataamua wapitishe kwamba katiba itambue serikali 3 ni lazima kwanza itungwe katiba ya Tanganyika ambayo itaainisha taratibu zitakazotoa mwongozo wa uchaguzi…hata kama itabaki kama ilivyo …. bado muda wa kuandaa huo utaratibu wa uchaguzi wa serikali za mitaa hautatosha kwa sasa”, alisema.
 
Aidha aliongeza, “Nimeona niliseme hili japo kwa ufupi kwamba uchaguzi huu huenda utalazimika kusogezwa mbele kutokana na kutokamilika kwa mchakato wa Rasimu ya mabadiliko ya Katiba“, alisema.
 
Katika hatua nyingine, Rais amewataka Maofisa Kilimo kwenye halmashauri kujiendeleza kitaaluma na kuwa mabingwa waliojikita katika taaluma ya mazao yanayostawi kwenye maeneo yao badala ya kuyashughulikia kwa ujumla mazao yote yanayolimwa na wananchi.
 
Alisema utekelezaji wa agizo hilo utaongeza mavuno kwa zao husika, utapanua wigo wa uzalishaji pamoja na utaalamu katika kushughulikia zao, aina ya zao na kuleta tija katika sekta ya kilimo.
 
Alisema hatua ya maofisa kilimo kuendelea kujishughulisha kwa ujumla na mazao yote yanayostawi bila kuwa na lengo la kusimamia mazao maalumu, kunaifanya sekta hiyo kudumaa na hivyo kushindwa kuwakwamua kiuchumi wananchi.
 
“Nimegundua kwamba watu wetu wengi hawana utaalamu uliobobea…hata maofisa kilimo wetu hawana taaluma maalumu zilizojikita kwenye aina ya mazao mengine zaidi ya mpunga na mahindi, hatua ambayo inawasababisha washindwe kusimamia vizuri uzalishaji wa mazao mengine ambayo yangeweza kuwakwamua kiuchumi wakulima kwenye halmashauri husika,” alisema.
 
Aliongeza, “Kwa hiyo ni jukumu lenu viongozi wa halmashauri kuwachukua maofisa kilimo wenu na kuwapeleka SUA kwa ajili ya ku-specialize (kujikita) kulingana na vipaumbele vyenu vya mazao kwa sababu sio wote wanao ubingwa katika kila zao…tukifanikiwa kwenye hilo tutapata mafanikio zaidi”, alisema.
 
Aidha aliwataka viongozi kwenye mkoa wa Tanga kuhakikisha shughuli za kilimo zinajikita kwenye uzalishaji endelevu wa mazao ya matunda na mboga, kwa kuwa mkoa huo uko katika fursa nzuri kiuzalishaji zaidi ya mazao ya nafaka.

Dayna Nyange asimulia jinsi anavyoshambuliwa na Mashabiki kwa Lugha Chafu baada ya kuamua Kujichubua


Mwimbaji wa kike Dayna Nyange amezungumzia jinsi alivyokutana na changamoto nyingi baada ya kuamua kubadili rangi ya  ngozi yake na kuwa nyeupe.
 
Akiongea katika The Jump Off ya 100.5 Times Fm, Dayna ameeleza kuwa amekuwa akikosolewa na watu wengi huku wengine wakitumia lugha mbaya dhidi yake lakini yeye ameipokea vizuri kwa kuwa anaamini ni watu wanaompenda.
 
“Ni sawa kwa sababu mimi naamini ni watu wangu wa karibu na ni watu ambao wananipenda ndio maana wanakuwa wanasema japo wengine wanatumia kauli mbaya. Lakini pia ni sawa kwa sababu mimi najua hao ni binadamu na kila binadamu anajua jinsi ya kupresent kwa mtu vile ambavyo anajisikia kwa hiyo ni mimi kutumia tu akili nakipokeaje.” Amesema Dayna Nyange.
 
Ameeleza kuwa yeye anaamini hakuna kitu ambacho aliwahi kukifanya kabla kikawa gumzo au tatizo kwa watu na ndio maana watu wanaamua kulichukulia hili kama tatizo kubwa.
 
Mwimbaji huyo alitangaza uamuzi aliouchukua kufuatia changamoto hizo alizokutana nazo ingawa anaamini kila mtu anauhuru wa kufanya maamuzi kama alivyoamua yeye.
 
“Kwa hiyo mimi naweza kusema ni sawa, inawezekana kweli nimekosa. Lakini mimi kama binadamu pia nina maamuzi yangu na nina sababu nyingi tu za kufanya kile ninachokifanya. Japo nimesikia maneno mengi sana mpaka Lol..’nimeacha.!
 
“Siwezi kusema kuwa nimeacha kabisa lakini nimetoka kule nilikokuwa, sasa hivi narudi kuwa Dayna yule ambaye mnataka awe. Japo pia binadamu pia mnakitu kimoja, sifieni kile kilicho bora kabla hakijakuwa sio.” Ameaongeza.

Rose Ndauka Amkimbia Mumewe


Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka hivi karibuni aliamua kumkimbia mumewe Malick Bandawe, kisa mfungo wa Ramadhani ambapo sasa anaishi Kigogo na mama yake mzazi. 

Akipiga stori na mwanahabari wetu, Rose alisema amelazimika kwenda nyumbani kwao ili kumpisha mumewe atimize nguzo hiyo ya Uislam bila kipingamizi kutokana na kutokufunga ndoa.
 
“Mimi sifungi hivyo nimeona pia ni jambo la busara kumpa nafasi mwenzangu kwa ajili ya kufanya ibada hiyo, mwezi ukiisha nitarudi na maisha yetu yataendelea kama kawaida,” alisema Rose ambaye awali alikuwa akiishi na mumewe huyo Tandale jijini Dar.