Batuli afunguka..."Sijawahi kumpenda mwanaume kama nilivyompenda Mtunis"



KWA mara nyingine, staa wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf  ‘Batuli’ amemwaga data za kimapenzi akidai hajawahi kumpenda mwanaume kama alivyompenda Nice Mohammed ‘Mtunis’.
 
Akizungumza na mwandishi wetu hivi karibuni, Batuli alisema licha ya kuwa walimwagana na staa huyo lakini hatokuja kupenda mwanaume kama alivyompenda Mtunis.
 
“Nilivyompenda Mtunis ni ngumu sana kumpenda mwanaume mwingine kama hivyo na kwa kawaida kupenda huwa ni mara moja tu mengine tutadanganyana,” alisema Batuli.
 
Hivi karibuni Batuli aliripotiwa kutikisa ndoa ya Mtunis ikidaiwa kuwa bado ana uhusiano naye lakini cha ajabu mtoto wa kike hakuonesha dalili zozote za kukanusha taarifa hizo.