TAMBUA JINSI YA KUACHA KUJICHUA (PUNYETO)KWA WANAWAKE NA WANAUME



Hebu niambie...umeshawahi kujichua? Mara ngapi? Bado unaendelea na mchezo huo? Vipi, umewahi kusikia watu wakizungumza kuhusu suala hilo? Najua unaona aibu, hasa kama una tabia hiyo. Usiogope rafiki yangu, leo nitazungumza na wewe taratibu halafu mwisho kabisa nitakuacha na tabasamu la nguvu!
Ndugu zangu, wakati mwingine kuna mambo magumu kidogo ambayo baadhi ya watu wanayaonea aibu, lakini yanaendelea kuwa tatizo kwa watu wengi. Leo tutazungumza. Amini usiamini, asilimia 90 ya wanaofanya mchezo huo, hawapendi hata kidogo. Kila wanapomaliza kujiridhisha huahidi kuacha, lakini baada ya saa kadhaa kupita, wanarudi kule kule. Kama una tabia hiyo, utakuwa unanielewa vizuri zaidi juu ya kile ninachokizungumzia hapa. Hebu twende tukaone.


KUJICHUA NI NINI HASA?
Kwa Kiingereza tendo hili linaitwa ‘’ likiwa na maana ya kupiga punyeto. Hapa nimetumia kwa ulaini kabisa; kujichua. Lugha nyepesi na rahisi kufikika kwa wengi ni kujiridhisha! Ni kitendo cha mtu kujichezea kimahaba huku akivuta hisia za mapenzi kwa mtu ambaye yupo mbali naye hadi anapomaliza haja zake.
Namna ya ufanywaji inategemea zaidi na jinsi ya mazoea. Wapo wanaotumia vifaa bandia (artificial) na wengine vifaa halisi kama aina mbalimbali za matunda ambazo zinafanana na sehemu pacha!
Wengine wanatumia njia wanazojua wenyewe, lakini wanaume wengi wanatumia sabuni lengo hapa ni moja tu, unatakiwa kufahamu kwamba namaanisha kujiridhisha.


INAWEZEKANAJE KUJIRIDHISHA?
Ni rahisi sana kumaliza tendo la huba kwa kujifanyisha mwenyewe. Silaha kubwa inayotumiwa na waathirika ni kuwavutia hisia watu wa jinsi pacha wakati tendo husika likiendelea kufanyika.
Habari mbaya kwa watu wenye mchezo huu ni kwamba, kwanza wakishaanza, inakuwa vigumu sana kuacha. Inashindikana kwa sababu ni jambo la aibu. Si rahisi kupata ushauri kutoka kwa watu maana ni aibu pia kumweleza rafiki yako juu ya mchezo huo. Kutokana na hilo sasa, kinachotokea ni kwamba ‘waumini’ wa mchezo huu wanaendelea kuwa watumwa kwa maisha yao yote. Hapa chini tutaona kwa undani jinsi tatizo hili linavyoumiza vichwa vya wengi.
Ni kweli hutaki kuwa mtumwa wa mchezo huu hatari? Zipo athari nyingi sana rafiki yangu ambazo nitazieleza hapa chini.


CHANZO NI NINI HASA?
Jambo la kushangaza ni kwamba, hakuna mdau wa mchezo huo ambaye amefundishwa jinsi unavyofanywa. Wengi wameanza wenyewe, tena wengine bila kujua nini kitakachotokea, lakini baada ya matokeo kuonekana, ndiyo mwanzo wa kutopea huko.
Kwa vijana wa kiume, wengi huanza tabia hii wakiwa kwenye umri wa kubalehe. Mara nyingi hutokea asubuhi wakati wa kuamka, usiku wakati wa kulala au bafuni wakati wa kuoga.
Kwa kawaida, mtu anapokuwa katika sehemu ya utulivu kwa maana ya kupumzika, wakati mwingine mkono unaweza kutembea huku na huko kwenye mwili na mwisho wake bila kutegemea mhusika anajikuta ameshaingia kwenye mchezo huo.


Huwa kama mzaha, akiwa hajui hatma yake, lakini msisimko anaoupata ndiyo unaomchanganya na mwisho wake anashangaa kila kitu kimemalizika. Unajua atakachosema? Sikia: “Mh! Kumbe ndiyo mwisho wake ni hivi? Lakini kama nimesikia starehe hivi...”


Hiyo hutokea pia wakati wa kuoga, ambapo wakati wa kujisugua kwa dodoki, msisimko ukitokea, madhara yanakuwa kama nilivyoeleza hapo juu.


Wenye umri mkubwa au wa kati, huanza tabia hii hasa baada ya kuanza mchezo wa kuangalia video za kikubwa wakiwa peke yao. Kwa sababu wanachotazama kinahusisha msisimko wa mapenzi, basi bila kutarajia hujikuta tayari!
Hii inafanana pia na kwa watoto wa kike, vyanzo nilivyoeleza hapo juu pia husababisha kwa karibu sana.


Sababu nyingine ni kunyimwa au kutotoshelezwa kimahaba na mwenzake.Wengi imewagusa, lakini kuna makundi mawili; wapo waathirika ambao wanatamani kuachana na utumwa huu na wengine wameathirika zaidi, kiasi kwamba hawana mpango wa kuacha.




Wengine wameenda mbali zaidi, kwa vile hawafikirii kuachana na mchezo huu, wamefikia hatua wanasema kwamba hakuna madhara kwa mtu anayejichua! Watu wanatetea wazi wazi, kwamba kujichua hakuna madhara. Sikia rafiki yangu, hata anayevuta sigara anajua kwamba ina madhara kwa afya yake, lakini ili kujifariji, atajenga hoja kwamba, haimdhuru na badala yake inamsaidia sana kuondoa baridi na haina kilevi.


Wakati mvuta sigara akisema hivyo, mlevi naye atakuja na hoja kwamba, pombe inamsaidia sana kupunguza mawazo. Kila mmoja atatetea upande wake. Ni jambo la kawaida kabisa.


Nikiwa naelekea kuendelea na mada yetu, rafiki yangu mpendwa kama wewe ni ‘muumini’ wa tabia hiyo, unatakiwa kufahamu kwamba unafanya jambo HATARI sana, si tu kwa afya yako, kisaikolojia na dhambi ya uzinifu ambayo hiyo itatokana na uhusiano wako mwema na imani ya dini yako, NDOA yako ipo/itakuwa hatarini.


Nadhani mnakumbuka wiki iliyopita nilieleza maana ya kujichua, namna tendo linavyofanyika na jinsi mtu anavyoanza mchezo huo bila kutegemea. Sasa rafiki, hebu tuendelee kwenye namna tatizo linavyokua.


UKUAJI WA TATIZO
Mwathirika akishazoea, hufanya tendo hilo kama sehemu ya maisha yake. Alianza bila kujua matokeo yake, lakini sasa amejikuta akianza kuupenda na idadi ya ufanywaji wa tendo huanza kupanda, baada ya siku tatu, siku mbili, kila siku na hatimaye kwa siku zaidi ya mara moja.
“Kaka Shaluwa, najichukia sana, yaani nimekuwa mtumwa kabisa wa kufanya huu ujinga.
Kwa siku nafanya mara mbili au zaidi, lakini si chini ya hapo,” alisema rafiki mmoja, aliyenipigia simu baada ya kusoma sehemu ya kwanza ya mada hii wiki iliyopita.
Ukweli ni kwamba, mfanyaji kwa vile ameshapata ‘mteremko’ wa kutimiza haja zake, kwanza ataanza kuwadharau wanawake/wanaume, kwamba hawawezi kumtisha, kwa sababu ana njia za kujifurahisha mwenyewe.
Pili, hufikia hatua ya kuwachukia watu wa jinsia pacha, akiwaona kama ‘wanaringa’ hasa kama atakuwa amemshawishi kimapenzi na kukatawaliwa.


ATHARI ZAKE
Zipo athari nyingi sana ambazo mwathirika anaweza kuzipata kwa kuendekeza mchezo huu. Hapa nataka nizungumze kwa herufi kubwa kabisa kwamba, ndugu zangu usidanganyike kwamba hakuna madhara kwa kufanya mchezo huu.
Yapo MADHARA makubwa sana ambayo yanapatikana kwa mchezo huo. Achana na propaganda za mitaani, zenye utafiti hewa.
Sikia nikuambie rafiki yangu, hasa wewe ambaye unafanya mchezo huo. Upo kwenye hatari kubwa ya kushindwa kufurahia mapenzi, kwa vile mazoea ya kiungo siri chako ni kwenye vitu ‘artificial’ zaidi ya ‘natural’.
Mwanaume aliyezoea kujiridhisha mwenyewe, akikutana na mwanamke, hana muda mrefu sana, kila kitu kinamalizika.
Siyo hivyo tu, uwezo wa kurudia tendo unakuwa mdogo au unakosekana kabisa. Kinachotokea ni kwamba, kiungo siri chake kinakuwa kimeshazoea, aina nyingine ya ‘hali ya hewa’ hivyo kinapokutana na sehemu siri za kike, ambazo ni laini na zenye ute mwepesi, inakuwa rahisi kumaliza ‘biashara’ mapema wakati wateja bado wanahitaji!
Kiungo siri cha mwanaume huwa kigumu, hivyo kusababisha maumivu kwa mwanamke kutokana na sugu aliyoitengeneza bila kujua. Kwa kawaida viungo siri vyote ni laini sana na vinatakiwa kubaki katika hali hiyo ili kuleta msisimko wenye usawa.
Mazoea yoyote tofauti na yale ambayo yanatakiwa hupunguza msisiko na kusababisha mmoja wa washiriki wa tendo la ndoa kubaki na kiu na mwenzake.


“Najuta kuufahamu huu mchezo, kila siku ninapokutana na mume wangu, ananiacha nikiwa sijatosheka. Kiukweli tangu amenioa, sijawahi kufurahia tendo la ndoa. Nilianza huu mchezo zamani sana, tangu nikiwa kidato cha tano.


“Kuna rafiki yangu mmoja nilikuwa nakaa naye bweni moja alinifundisha. Sikujua kama madhara yake ni makubwa kiasi hiki. Ilikuwa ni shule ya wasichana tupu, kwa hiyo akanidanganya kwamba tuachane na wanaume tujichue...kumbe alikuwa ananisaga!” hii ni sehemu ya ushuhuda mwingine wa mchezo huo.


Athari nyingi ambayo mtu anaweza kuipata kwa kujichua ni kumaliza ‘kazi’ mwenyewe bila hata kwenda kazini. Akipita mtu wa jinsi pacha, ambaye ana mvuto, kazi inaishia hapo hapo!


UPO KUNDI GANI?
Uko wapi rafiki yangu? Nazungumza na wewe ambaye unafanya mchezo huo, bado unataka kuendelea nao au unatamani kuacha? Shika maneno yangu, kwamba ni HATARI kujichua, halafu weka nia ya kutaka kuacha huu utumwa, kisha vuta subira hadi wiki ijayo katika sehemu ya mwisho ambayo haitaacha kitu.


MFADHAIKO
Mtu ambaye anaendekeza kazi hii, hupata mfadhaiko. Anayepata mfadhaiko, huwa mwepesi sana wa kuwa na matamanio kwa jinsia ya upande wa pili.


Si ajabu mtu mwenye mchezo huo, kutembelea akimwangalia mwanamke kuanzia Magomeni hadi Manzese! Amefadhaika. Ameshazoea kumaliza kazi nzima akiwa peke yake, kwa hiyo raha yake inabaki kuwa katika picha tu na si kitu halisi.


Macho yanakuwa juju juu, si kwa kupenda, ni kwa sababu tayari ameshaathiriwa na tatizo hilo. akitoka hapo, ujue moja kwa moja faragha, anaanza mambo yake. Kelele nyingi, kumbe yupo peke yake!


Mfadhaiko hauishii hapo, hata akiwa kwenye vyombo vya usafiri au mkusanyiko wa watu, mwathirika huweza kumaliza ‘kazi’ kwa macho tu, tena wakati mwingine bila kuwa na taarifa. Anakuja kugungua baadaye sana, kwamba kumbe kila kitu kilishafanyika bila hiyari yake.


KUSHINDWA TENDO LA KAWAIDA
Mwenye mchezo huo, pamoja na uhodari wake wa kujifurahisha akiwa peke yake, anapokutana na mwenzi wake faragha, kazi inakuwa si ya kiwango cha kuridhisha. Kuna athari nyingi ambazo hujitokeza.


Kwanza, anakosa ujasiri, hayupo tayari kuandaliwa, kumuandaa mwenzake. Kishazoea kufanya kila kitu haraka haraka, tena kwa kutumia hisia zaidi kuliko uhalisia wa tukio lenyewe.


Anakuwa goigoi, anachelewa kuwa tayari, hata akiwa tayari anafika safarini mapema zaidi. Mbaya zaidi, akifika hawezi kuanza safari nyingine. Hata kama akianza, kuna uwezekano mkubwa wa kuishia njiani.


Baadhi yao, hubaki wakiwa baada ya wahusika wao kuwagomea katikati ya safari. Zipo athari nyingi zaidi ya hizo, kutegemea na namna tatizo lilivyokomaa na aina ya jinsia.


KUFEDHEHEKA
Baada ya hayo hapo juu kujitokeza kwenye ndoa/uhusiano wa mwathirika, kinachofuata sasa inakuwa ni kufedheheka. Kwa bahati mbaya sana, unaweza kufanya siri mchezo wako, lakini athari zikawa wazi kwa mwenzako.


Hata kama hatagundua chanzo cha tatizo, lakini atagundua kwamba huna msisimko, huwezi kazi au vyovyote vile. Wengi husema kwa hisia, humaanisha kwamba hakuna wanachopata kutoka kwa wenzao, lakini mambo yakizidi kuwa hovyo, wanafunguka: “Mwenzangu kila siku unaniacha na kiu, una tatizo gani?”


Kauli hiyo rafiki yangu, inatosha kabisa kukufanya ushindwe kazi moja kwa moja. Unajua nini? Utaanza kuwaza: “Kumbe siwezi kitu...halafu mwenzangu ameshagundua. Nitafanyaje mimi? Mbona nahadhirika?”


Ndugu yangu, ikifikia hapo utakuwa unamkimbia mwenzako na kwenda chemba kumaliza biashara zako mwenyewe. Furaha ya moyo itatokea wapi? Kama ndiyo mnaishi kinyumba au mpo ndani ya ndoa ndiyo kabisaaa!
Umeona kazi hiyo?


UNATAKA KUACHA?
Hakuwa dawa kubwa sana ya kuacha mchezo huu. Najua wengi walikuwa na hamu ya kutaka kusikia, wataachaje huu mchezo. Ndugu zangu.Usitarajie kwamba nitakuja kuingia kwenye nafsi yako na kukuambia ACHA KUJICHUA! Ndugu zangu, nitawapa dondoo chache sana, lakini kubwa ni kwamba ATHARI nilizotaja hapo juu zinatosha kabisa kukubadilisha!


Hebu nikuulize, utakuwa na hamu ya kuendelea na haya mambo kama ndoa yako itakuwa hatarini? Nani atakubali kufedheheka? Nani atakubali kupoteza heshima yake? Bila shaka hakuna. Pitia dondoo zifuatazo;


(i) Badilisha utaratibu wa kulala, lala kifudifudi, badala ya chali (rejea maelezo yangu ya awali kuhusu chanzo cha tatizo)
(ii) Acha kuangalia mikanda ya kikubwa ukiwa peke yako.
(iii) Kaa mbali na simulizi zinazohamasisha mapenzi, mazungumzo ya aina hiyo na kampani za watu wanaopenda kusimulia mambo ya faragha.


(iv) Acha mazoea ya kujishika sehemu zako za siri.
(v) Fanya mazoezi ya viungo angalau robo saa tu kwa siku.
(vi) Juu ya yote haya, FUTA kabisa mawazo ya jambo hilo. AMUA kwa dhati ya moyo wako, tambua na ogopa athari ambazo unaweza kuzipata, kisha ACHA KABISA mchezo huo ili kulinda heshima yako na kujipa furaha ya maisha