Madaktari nchini Canada wameingia katika matitizo makubwa baada ya kukosea na kumkata mwanaume mmoja sehemu ya uume wake na kupunguza kwa urefu wa inch 1 (sentimeta 2.5).
Kwa mujibu wa QMI la Canada, mwanaume huyo anadaiwa kufika hospitali
akihitaji matibabu baada ya kuumia bahati mbaya wakati wa tendo la ndoa
na kupata mshituko hivyo kulazimika kufanyiwa upasuaji ili kumsaidia
kuituliza mishipa iliyokuwa hatarini.
Lakini baada ya kumaliza tiba aligundua kuwa amekatwa sehemu ya uume wake na madaktari wakadai ilikuwa bahati mbaya.
Kufuatia tukio hilo, anadai alishindwa kufanya mapenzi kwa muda wa
miaka miwili hivyo mke wake ambaye jina lake halikutajwa na vyombo vya
habari vya Canada, aliamua kuachana nae.
Uamuzi wa mwanamke huyo ulimvuruga zaidi mwanaume huyo ambaye ameamua
kufungua mashitaka dhidi ya madaktari waliomfanyia upasuaji.
Mwanaume huyo anadai fidia ya $155, 000 kwa uzembe uliofanywa na
madaktari hao kwa kuwa inaelezwa hawakufuata taratibu zote za awali
kabla ya kumfanyia upasuaji.
“Hii imenifanyia madhara makubwa katika maisha yangu zaidi ya siku niliyoumia miguu yangu na kushindwa kutembea.”