Miongoni mwa makosa yanayofanyika mtandaoni ni hili lijulikanalo kama “Phishing” ambapo kosa hili limekuwa likidumu na kukua kwa kasi sana katika nchi mbali mbali.
Nchi
mbali mbali zimechukulia uhalifu huu kuwa ni hatari kwani unaweza kuwa
na madhara makubwa kwa mtendewa ikiwa ni pamoja na kupelekea kumfilisi
mtu, kupata taarifa za watu kinyume na sheria au makubaliano na hata
wakati mwingine kupelekea kuleta madhara mengine kama kutumika
kuhatarisha mifumo mbali mbali.
Kwa
kuzingatia hili nchi mbalimbali zimekuwa na sheria kali dhidi ya
uhalifu huu , huku nchi za afrika kupitia umoja wa wataalam wa maswala
ya usalama mtandaoni wamekubalina kuanzisha kamati yenye watu maalaum
itakayoangazia macho uhalifu huu na kutoa taarifa huku hatua
zikichukuliwa.
Makampuni
ya Ati-vurus nayo yametoa uzito kwenye hili na kuhakikisha wanaunda
nyezo madhubuti za utambuzi wa aina hii ya uhalifu na mara kwa mara
wakiwasilisha ripoti zao.
Changamoto
bado zipo kutokana na upungufu wa uelewa kwa wananchi mbali mbali juu
ya uhalifu huu inayo sababisha waathirika kueendelea kuwa wengi kila
kukicha.
Uchunguzi
umeonyesha mara nyingi panapokuwa na jambo linalo fuatiliwa na wengi,
wahalifu nao hujipenyeza hapo na kuanza kusambaza aina hii ya uhalifu.
Kwa
upande wa Tanzania, Serikali imekuwa ikizungumza mara nyingi na
kutoa tahadhari mbalimbali juu ya uharifu wa kimtandao.
Ni
vizuri tukakumbushana kuwa Tanzania imesha kamilisha rasimu ya sheria
za mitandao ambazo zitatoa fursa kwa wahalifu kushughulikiwa ipasavyo na
hivi karibuni TCRA nayo ilizungumzia mpango wake wa kushughulikia
watumiaji vibaya wa mitandao. Hili likiwa linafuatia kampeni yao ya Futa
delete kabisa.
Wakati
hili linajiri, kumekuwepoa na wimbi la wahalifu wa uhalifu huu wa
"Phishing" ambao hudukua na kuchukua akauti za mitandao za watu na
kuanza kusambaza taarifa zitakazo wawezesha kupata taarifa za wengine
na mara nyingine wanatengeneza akaunti feki za mitandao wakitumia majina
ya watu maarufu na kuanza kuzitumia vibaya.
Waharifu
hao wamekuwa wakitumia majina ya watu mashuhuri na kutumia watu
ujumbe wakiwataka wabonyeze link ili kujiunga na huduma kama Vikoba, Pia
wamekua wakituma ujumbe wakiwataka watu wafungue tovuti n.k
TAHADHARI:
Kila mmoja anapaswa kuwa makini na unapo hisi ya kuwa unaweza ukawa
muathirika wa uhalifu wa huu kimtandao basi badilisha neno la siri na
siku zote jiepushe kujibu au kufuata maelekezo yatakayo kutaka ufanye
kitu Fulani.