mikoani. Vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) vimefanikiwa kushinda kata nyingi katika jiji la Dar es Salaam
na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuongoza mabaraza ya madiwani katika
halmashauri za manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke.
Mbali ya kusimamia mabaraza hayo, pia Ukawa unaweza, kwa
mara ya kwanza, kuongoza halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.
Tangu mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa mwaka 1992, CCM
imekuwa ikishinda kata nyingi na hivyo madiwani wake kuunda halmashauri, lakini
mwaka huu imepokonywa kata nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili
iliyopita baada ya Ukawa unaoundwa na vyama vya NLD, CUF, Chadema na
NCCR-Mageuzi kunyakua ushindi katika kata hizo.
Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi huo yanayoendelea
kutangazwa Ukawa umenyakua viti 53 vya udiwani katika majimbo ya Kinondoni,
Ukonga, Ilala, Segerea, Temeke, Kibamba, Kawe, Ubungo, Mbagala na Kigamboni wakati
CCM ikipata viti 38.
Moja ya Halmashauri ambazo Ukawa wataziongoza ni ya
Kinondoni ambako umetwaa kata 22 kati ya 34. Katika halmashauri hiyo yenye
majimbo ya Kawe, Ubungo, Kibamba na Kinondoni, Chadema imenyakua kata 17, CUF
imeshinda kata 6, na CCM imetwaa kata 9 huku yakisubiriwa matokeo ya kata
mbili.
Halmashauri ya Ilala yenye majimbo ya Ilala, Ukonga na
Segerea, matokeo yanaonyesha kwamba Chadema ina kata 19, CCM kata 15 na CUF
kata mbili. Madiwani wa kata hizo ndio watakutana kuteua meya na naibu meya wa
halmashauri ya Ilala.
Halmashauri ya Temeke inayoundwa na majimbo ya Temeke,
Kigamboni na Mbagala ina jumla ya kata 31. Katika jimbo la Temeke CCM ina kata
7, Chadema 5 na CUF 1; Kigamboni: CCM kata 6, Chadema 2 na CUF 1, wakati
Mbagala CCM kata 7 na CUF tatu.
Aidha, upinzani umefanikiwa kutwaa majimbo sita kati ya
10. Majimbo hayo na majina ya wabunge wake kwenye mabano ni Kawe (Halima Mdee –
Chadema), Kinondoni (Maulid Mtulia – CUF), Temeke (Abdallah Mtolea – CUF),
Ukonga (Mwita Waitara –Chadema), Ubungo (Saed Kubenea – Chadema), Kibamba (John
Mnyika- Chadema).
Waitara amepata ubunge baada ya kumbwaga aliyekuwa meya
wa Ilala, Jerry Slaa (CCM); Mtolea amemshinda Abbas Mtemvu (CCM); Mdee
amemwangusha Kippi Warioba (CCM), na Kubenea amemshinda aliyekuwa meya wa jiji
la Dar es Salaam, Didas Masaburi (CCM).
Mnyika amembwaga Fenella Mkangalla (CCM), Mtulia
amemshinda Idd Azzan (CCM). Bonna Kaluwa wa CCM ndiye mbunge wa Segerea,
Faustine Ndungulile wa CCM amefanikiwa kutetea jimbo la Kigamboni sawa na Mussa
Hassan Zungu aliyetetea jimbo la Ilala.
Matokeo ya mikoani
Jimbo la Ndanda lina kata 16; CCM (15), Chadema (1);
Tandahimba: kata 30, CCM (10), CUF (16), Chadema (1); Kalenga: kata ni 15, CCM
(13), Chadema (3); Iringa Mjini kata 18, Chadema (14), CCM (4); Isimani kata
14, CCM (11) Chadema (3); Ushetu kata 20, CCM (20); Serengeti kata 30, CCM
(12), na Chadema (18).
Jimbo la Dodoma Mjini kata 41, CCM (34), Chadema (6);
Mpwapwa lina kata 13, CCM (13); Kibakwe kata 18, CCM (18); Mbozi kata 11, CCM
(7), Chadema (4); Mtwara Mjini kata 18, CUF (8), CCM (7), Chadema (3); Mwibara
kata 12, CCM (7), Chadema (2), TLP (2) na CUF (1); Bunda Mjini kata 14, CCM
(10) na Chadema (4); Bunda Vijijini kata 7, CCM (5) na Chadema (2).
Handeni Mjini kata 12, CCM (11), CUF (1); Handeni
Vijijini kata 21, CCM (20), Chadema (1), Kilindi kata 21, CCM (20) kata moja
haijafanya uchaguzi; Vunjo kata 16, NCCR (8), CCM (4), Chadema (4); Sikonge
kata 17, CCM (14), Chadema (3); Kahama Mjini kata 20, CCM (19) Chadema (1).
Momba kata 14, CCM
(8), Chadema (6); Mbeya Vijijini kata 29, CCM (21), Chadema (7); Kisarawe: CCM
(14), Chadema (2), CUF (1); Nanyumbu CCM (15), CUF (2), na Bagamoyo kata zote
11 zimechukuliwa na CCM.