

Tukio hilo bichi kabisa lilitokea Juni 16, mwaka huu , Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo chanzo kinasema , wadada hao walikuwa wakirekodi sinema ambayo haijajulikana jina lake . “Ni kweli walikuwa wakirekodi filamu , lakini kuna muda walizinguana ila watu wanasema bado wanakasirikiana kutokana na ile ishu ya kunyang’ anyana mwanaume . “Joti ( Lucas Mhuvile – yule komediani wa Kundi la Orijino Komedi ) alikuwepo eneo la tukio na ndiye aliyewapatanisha, ” kilipasha chanzo hicho. Joti alipotakiwa kuzungumzia ishu hiyo , alikiri kutokea lakini kwenye kurekodi filamu huku akikataa kufafanua.
“We’ jua kuwa ilikuwa filamu , si ugomvi serious,” alisema Joti . Lulu hakupatikana kuzungumzia ishu hiyo lakini Husna alipopatikana alisema : “Tulitofautiana kikawaida tu kama wanawake lakini hatukufika kwenye mambo ya kupigana. ”